Zanzibar inaangamizwa, wazanzibari taabani

aleesha

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
835
Reaction score
1,215
Zanzibar, pengine inapitia kipindi kigumu kama au kuliko kipindi cha baada ya mauwaji ya mwaka 1964. Chuki, Ubaguzi vimeshika kasi mithili ya utawala wa Dkt. Salmin Amour.

Zanzibar, chuki na hasama kadhalika ubaguzi vimetamalaki kila eneo.

Zanzibar, kadi ya ccm imenasibishwa na uraia.
Zanzibar, elimu na taaluma sio kigezo cha mtu kupata kazi bali kadi ya ccm (Jembe) kwa lugha yao wenyewe ndio imechukuwa nafasi hiyo.

Asikudanganye mtu, Zanzibar hali si shwari kuna Joto, kuna fukuto, moto unachemka ndani kwa ndani. Wananchi wa Zanzibar wamejiinamia kila mmoja ana kilio chake cha ugumu wa maisha. Kwa hakika raia ambao wengi wao ni vijana wamekata tamaa kwa ukali wa maisha.

Nikiri katika uhai wangu, kwa mara kwanza nashuhudia mawingu ya giza yakimwaga vuke la joto lililo ambatana na njaa kali ya maisha katika ardhi iliyojaa neema ya visiwa hivi vyenye historia pana katika bahari ya Hindi. Zanzibar imeemewa, Wazanzibari wamesakamwa na tonge chungu ya viburi vya watawala wasiojali vilio vya RAIA wanyonge waliojaa utiifu na wapole katika nchi yao.

Kama kuna kiongozi ambae aliingia madarakani kwa furaha huku akiridhiwa na Wazanzibari wote (jambo ambalo katika historia likefanyika mara moja tu) basi ni Dkt. Shein pekee (2010-1015).

Mwaka 2010 hukuweza kumtambua nani ni mfuwasi wa CCM wala CUF wote walishangiria ushindi bila ya kinyongo. Maalim Seif alisema "hakuna mshindi wala mshindwa washindi ni Wazanzibari"

Dkt. Ali Mohammed Shein aliingia madarakani (2010-2015) aliikuta nchi imepiga hatua kubwa ya umoja na mshikamo alikuwa akiiongoza serikali ya Umoka wa Kitaifa (SUK) ambayo imekuja kwa matakwa ya Wananchi wenyewe kuamua kuunganisha nguvu za umoja na kuimarisha mshikamano kwa lengo la kusahau yalopita ili tuweze kupiga hatua za maendeleo. Kwa bahati mbaya, chama kimekuwa kizito kwake kuliko utaifa wake. Amerejesha nyuma nchi kwa zaidi ya miaka 50.

Ameyakusanya yote yaliyopita kwa pamoja na kuwalisha Wazanzibari. Katika hali ya mshangao Wananchi waliojiinamia wangali wanajiuliza ndiye yeye huyu Dkt. Ali Mohammed Shein au ni mwengine? Kwa tafsiri ya haraka unaweza kusema huyu ndio kingozi alofeli zaidi kuliko wote waliomtangulia.

Mimi naamini, ipo siku atakuja kuyajutia haya katika maisha yake isipokuwa sijui kama majuto yake yatakuwa na maana tena. Muda ndio utakao twambia na ukweli ndio utakao bakia na historia utakuja kusimulia.
 
Cuf maalim lini mnahamia chadema angalau kuiboost kidogo tena!
 
Siku Wazanzibar watakapoacha kubaguana na kuanza kuheshimiana yote haya yataisha.
 
Last edited:
Mambo mawili. Kwanza Serikali ya Zanzibar inaendeshwa na kikundi cha watu wachache sana hao ndio kila kitu na ndio wana control uchumi wa Zanzibar (pesa ya utalii na karafuu) na hawajali ni nani amekula ama amekufa njaa. mmoja ni mtumishi wa Umma na anamiliki shirika la ndege Sheni kimyaaaa. Yaliyowahi kutokea Zanzibar kisiasa kwa uhalisia ule ule ndio yanakuja Tanganyika. Ni kiasi cha muda mdogo tu.
 
Mkitaka kupiga hatua msikubali kutenganishwa.kuna mijitu ipo huku bara kazi yao ni kuwajengea chuki na kuwagawa ili waendelee kuwatawala vizuri.msijali nguvu walizonazo jiungeni muwe na umoja wataogopa sana. Poleni ndugu zetu.
 
Zanzibar, pengine inapitia kipindi kigumu kama au kuliko kipindi cha baada ya mauwaji ya mwaka 1964. Chuki, Ubaguzi vimeshika kasi mithili ya utawala wa Dkt. Salmin Amour.

Zanzibar, chuki na hasama kadhalika ubaguzi vimetamalaki kila eneo.

Zanzibar, kadi ya ccm imenasibishwa na uraia.
Zanzibar, elimu na taaluma sio kigezo cha mtu kupata kazi bali kadi ya ccm (Jembe) kwa lugha yao wenyewe ndio imechukuwa nafasi hiyo.

Asikudanganye mtu, Zanzibar hali si shwari kuna Joto, kuna fukuto, moto unachemka ndani kwa ndani. Wananchi wa Zanzibar wamejiinamia kila mmoja ana kilio chake cha ugumu wa maisha. Kwa hakika raia ambao wengi wao ni vijana wamekata tamaa kwa ukali wa maisha.

Nikiri katika uhai wangu, kwa mara kwanza nashuhudia mawingu ya giza yakimwaga vuke la joto lililo ambatana na njaa kali ya maisha katika ardhi iliyojaa neema ya visiwa hivi vyenye historia pana katika bahari ya Hindi. Zanzibar imeemewa, Wazanzibari wamesakamwa na tonge chungu ya viburi vya watawala wasiojali vilio vya RAIA wanyonge waliojaa utiifu na wapole katika nchi yao.

Kama kuna kiongozi ambae aliingia madarakani kwa furaha huku akiridhiwa na Wazanzibari wote (jambo ambalo katika historia likefanyika mara moja tu) basi ni Dkt. Shein pekee (2010-1015).

Mwaka 2010 hukuweza kumtambua nani ni mfuwasi wa CCM wala CUF wote walishangiria ushindi bila ya kinyongo. Maalim Seif alisema "hakuna mshindi wala mshindwa washindi ni Wazanzibari"

Dkt. Ali Mohammed Shein aliingia madarakani (2010-2015) aliikuta nchi imepiga hatua kubwa ya umoja na mshikamo alikuwa akiiongoza serikali ya Umoka wa Kitaifa (SUK) ambayo imekuja kwa matakwa ya Wananchi wenyewe kuamua kuunganisha nguvu za umoja na kuimarisha mshikamano kwa lengo la kusahau yalopita ili tuweze kupiga hatua za maendeleo. Kwa bahati mbaya, chama kimekuwa kizito kwake kuliko utaifa wake. Amerejesha nyuma nchi kwa zaidi ya miaka 50.

Ameyakusanya yote yaliyopita kwa pamoja na kuwalisha Wazanzibari. Katika hali ya mshangao Wananchi waliojiinamia wangali wanajiuliza ndiye yeye huyu Dkt. Ali Mohammed Shein au ni mwengine? Kwa tafsiri ya haraka unaweza kusema huyu ndio kingozi alofeli zaidi kuliko wote waliomtangulia.

Mimi naamini, ipo siku atakuja kuyajutia haya katika maisha yake isipokuwa sijui kama majuto yake yatakuwa na maana tena. Muda ndio utakao twambia na ukweli ndio utakao bakia na historia utakuja kusimulia.

Acha kulalamika, toa ushauri kama unayoyasema ni kweli
 
Halafu shangazi yenu kaja kujishaua Tanganyika na harakati uchwara badala ya kwenda kusaidia nduguze
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]swadaka njema huanzia nyumbani!yeye ameanzia kwa jirani.[emoji125][emoji125][emoji125]
 
Wazanzibari na Watanzania wote kwa ujumla wameregea kupita kiasi, Nidhamu za wogo zainawasumbua.

Bila ya kubadilikia wataendelea kunyanyaswa na CCM kwa miaka mingi mbele.
 
Back
Top Bottom