Zanzibar inaangamizwa, wazanzibari taabani

Zanzibar inaangamizwa, wazanzibari taabani

Kwa chuki hapan sina. Nawaona ndugu zangu. Hila jamaa lazima wachange.

Mimi nilikaa nao sana nje ya nchi nilipokuwa nikisoma na niliwaona jinsi wanavyojituma kwa kufanya kazi huku na kule hususan wale wasio na elimu. Halafu maisha ya nje sio kama ya kwetu usipofanya kazi huli na huwezi kuishi. Ukirudi nchini jaribu kufika znz kwenye construction sites na kwenye maeneo ambayo informal sector economy imetamalaki uwaone jinsi akina mama wa kizanzibari wanavyobeba zege na wanaume wanavyohangaikia maisha. Sikatai unaweza ukawakuta watu wachache pengine asubuhi wamekaa kwenye kijiwe kakn huwezi jua mishe zake baada ya hapo zikoje. tunapoangalia jambo ni vyema tukaliangalia kwa uhalisia na kwa proper perspective bila ya kuleta bias za kulazimisha uamini jambo kinyume na uhalisia. Evidence matters alot.
 
Mkuu,hali ya Zanzibar imetengenezwa kwa makusudi,"Divide and Rule"...,wameambiwa kuwa mwanarabu atarudi...
Mwaka jana nilitembelea visiwa vya Unguja niliburudika sana kule jambiani nikatoka hotelini nikaenda kukaa na wenyeji tukawa tunapeana mawili matatu..nikawaona ni watu wakarimu sana hawana makuu nikawa najiuliza mbona kwenye vyombo bya habari tuna aminishwa sivyo?!
 
Mara nyingi kwenye siasa haswa huwa tunapingana sana.
Tunapingana,pale inapokuwa hatukubaliani,lakini katika hili uko sawa,kwani hali ya Zanzibar inasababishwa na wazanzibari wenyewe,ijapokuwa wazanzibari wameshaonyesha nia yao ya kuikataa CCM 2015,lakini bado wapo wanaoamini propaganda za "Mwanarabu atarudi""
 
Mwaka jana nilitembelea visiwa vya Unguja niliburudika sana kule jambiani nikatoka hotelini nikaenda kukaa na wenyeji tukawa tunapeana mawili matatu..nikawaona ni watu wakarimu sana hawana makuu nikawa najiuliza mbona kwenye vyombo bya habari tuna aminishwa sivyo?!
Wazanzibari ni watu wakarimu sana,ukarimu wao ndio umewafanya waungane na watu waiowafikiria ni ndugu zao,kumbe vile vile ulikuwa ni mtego wa kutawaliwa na mkoloni wa wa Kiafrika,Ukarimu wao umewafanya wawe mabwege...,siasa zinaharibu mila na dasturi za watu wa Zanzibar,...nimefurahi kuwa umeliona hilo..
 
Hizi siasa za chuki hazifa katika taifa hili.
 
Una maana gani unaposema mkoloni mweusi?.
 
Hizi siasa za chuki hazifa katika taifa hili.
Hawa wanasiasa hasa wale wa CCM Zanzibar,wanaharibu taifa zima la Tanzania,wanaharibu umoja na muungano uliopo kati ya Wazanzibari na Watanzagayika watu ambao walikuwa wameungana kijamii kabla ya huu muungano wa kisiasa uliooletwa na Karume na Nyerere,..

Hivi sasa Mznzibari anamuona Mtanganyika adui,Mtanganyika anamuona Mzanzibari mbaguzi,hali ilikuwa sio hivyo hapo mwanzo,hata hayo mapinduzi ya 1964 ni watu kutoka Tanganyika ndio walikuja kuwasaidia ndugu zao wa Zanzbari kumuondoa Sultani...
 
Una maana gani unaposema mkoloni mweusi?.
imhotep,CCM inavyoung'ang'nia na kuulinda huu Mungano hakuna tafauti na wakoloni walivyokuwa wakiyang'ang'ania mataifa waliyoyatawala,Pale wafrika walipoamua kuwa hawataki tena kutawaliwa wakoloni walifanya kila mbinu na hila wasiondoke katika yale mataifa wanayoyatawala,walitaka wawatawale wafrika milele...,Kuna nchi mkoloni aliondolewa kwa mtutu wa bunduki..

Utawala wa CCM hauna tafauti na mkoloni
 
Last edited:
Nimecheka sana!! sasa wewe unafikira Final solution iwe nini?
Acha wazanzibari wajitawale wenyewe,kimawazo,kifikira,kiuchumi,kisiasa,...ikitokea kuwa hivyo,Zanzibar,Tanzania kwa ujumla itapiga hatua sana kimaendeleo ya kijamii,na kiuchumi kama wanasiasa wataitumia Zanzibar vizuri...

Mkuu kama warabu waliweza kuifanya Zanzibar iwe "Ecolomical Power" kwa miaka hiyo,kwanini sisi waafrika tusiweze,Kisiwa kama cha Mauritius kilichopo mbali sana na bara la Afrika kimeweza kupiga hatua kimaendeleo mpaka hivi sasa kiko karibu kuwa "First world" kwanini Zanzibar isiweze...

Wanasiasa wa CCM waache kufikiri,kuamua kwa hisia,maamuzi na fikira ziwe za uhalisia,tutafika kama taifa...
 
Mkuu kama warabu waliweza kuifanya Zanzibar iwe "Ecolomical Power" kwa miaka hiyo,kwanini sisi waafrika tusiweze
Mimi ninavyojua kipindi hicho Zanzibar ilikuwa inategemea bidhaa nyingi kutoka mainland Africa, kama pembe za ndovu ngozi za chui na watumwa na vingine vingi, huo muda umeshaenda leo labda zanzibar ifanywe free port ili bidhaa ambazo mainland africa inazihitaji kuja kuzinunua.
 
Kipindi hicho Zanzibar ilikuwa "Free port",kama ilivyo Dubai sasa,muda haujaenda,hivi sasa Dunia imekuwa ndogo zaidi,hebu fikiria "episode" baada ya Mzambia kwenda kununua Gari Dubai,kwasababu ni mbali anakuja kununua gari Zanzibar,....Wakati wa Utawala wa Salimini Amour nilikuwa nawaona watu nchi mbali mbali,Wangola,Wazambia nk wakija Zanzibar kununua Bidhaa.

Mkoloni alichokifanya akatangaza kitu kinachotoka Zanizbar kuingia Tanganyika lazima kilipiwe ushuru tena,matokeo yake wageni wakaacha kuja Zanzibar kwani kibiashara hailipi..Vipi kwani Mkolooni angeliachia tu ile hali ikaendelea!!?? nani angalifaidika?

Tungefanikiwa na kufaidika sote wa Tanganyika na Wazanzibari,Mfano Mgeni akitaka kuja Zanzibar lazima apitie Bara,mgeni atataka alipe malazi,chakula,labda atakwenda bar,alipe usafiri wa kwenda na kurudi nk,nk nk,kutakuwepo mzunguko wa pesa,watanzaia watafaidika na huo mzunguko wa pesa ,serikali itakusanya kodi nk,nk...Ni sawa na Hongkng na China Mailand

Mkuu hayo ndio matatizo tuliokuwa nayo waafrika tayari umeshakata tamaa kabla hata hujatekeleza unayotaka kuyafanya " Eti muda umeshaenda" sio muda ulioenda ni mawazo yetu ndio yameenda,wafrika hatuangalii "with big Picture"...sioni sababu kisiwa cha Maurituius kifanikiwe sisi,tusifanikiwe,..

Logistical Zanzibar iko pazuri sana kibiashara kwa upande wa Afrika Masahariki na Kati,lakini kwa sabau ya siasa mbovu,siasa sisizo na malengo,siasa za Ku-contoll ndio zinatufikisha hapa tulipo kila mtu anamchukia mwenzake kwasaabu ya njaa
 
Last edited:
Mwaka jana nilitembelea visiwa vya Unguja niliburudika sana kule jambiani nikatoka hotelini nikaenda kukaa na wenyeji tukawa tunapeana mawili matatu..nikawaona ni watu wakarimu sana hawana makuu nikawa najiuliza mbona kwenye vyombo bya habari tuna aminishwa sivyo?!

Ni île hali ya siasa, utasikia vijiweni ya kuwa jamaa wavivu , ilhali huyo msemaji anadaiwa na mzenji Mwenye duka au kaajiriwa na mzenji kwenye kiwanda Cha matofali, au île kauli ya mtu wa bara hawezi kumiliki ardhi , mi nimekaa zenji n'a naweza kusema kuwa mzee SEPETU ni mbara Ila ana nyumba , ardhi n.k kule zenji, wapo wengi tu Kama hao.
Watu wa bara (nakusudia mikoani ) wakija miji ya PWANI , (ukitoa DSM) huwa sio Sana kujichanganya na wenyeji wa maeneo yale(Hilo nimelishuhudia mwenyewe nikiwa zenji), kwa hio hâta kama kusoma tabia ya mtu basi itakuwa no vigumu Sana.
Niliwahi kusema kuwa siasa ya Tanzania ni copy and paste ya ile ya Zanzibar (ngoma ikipigwa Zanzibar....).
Kwa uvivu , hamna jamii au Kabila lisilo n'a watu wavivu, kikawaida WASWAHILI wa asili (watu wa mwambao) tunaonekana wavivu Jambo ambalo sio la kweli.
 
Back
Top Bottom