Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,346
- 26,143
Kweli kabisa, sisi tunawabembeleza wao hatutaki
Iko wazi kabisa kuwa ili kuulinda mfumo huu wa Muungano wa Serikali mbili,Zanzibar imekuwa ikijichomoza kila uchao kama nchi kamili. Kutokana na vuguvugu la mara kwa mara kutoka kwa Wazanzibari,CCM na Serikali yake imekuwa ikiharakisha kuwapa wanachopinga ili kuulinda mfumo wa Muungano uliopo. Ni kama Wazanzibari hubembelezwa na kupendelewa.
Iko wazi kuwa, Zanzibar ina wananchi wathubutu.Wananchi wanaoweza kusema kile wanachokiamini.Wananchi ambao wanaweza kumkosoa yeyote iwe kule kule Zanzibar au katika ngazi ya Muungano. Ipo mifano mingi ya akina Mzee Moyo,Shamhuna,Maalim Seif,Jussa na wengineo. Hawa hawapepesi macho wanapotaka kusema ukweli wanaouamini kuwa hivyo.
Ndiyo maana sasa Zanzibar wana bendera yao,wana wimbo wao wa Taifa,wana vitambulisho vyao vya ukaazi,wana mizinga yao ya sherehe mbalimbali za kitaifa,wana majeshi yao kama JKU na KMKM,wana Katiba yao inayowatambulisha kama nchi kamili na kadhalika na kadhalika. Nasema,wenzetu wa Zanzibar,pamoja na kuwa na Serikali yao tangu siku ya kuanza Muungano, wanaendeleza mapambano yao ya kutaka 'uhuru kamili' wa Zanzibar yao.
Sasa Zanzibar imebaki na dukuduku kubwa moja: ushirikiano wa kimataifa. Zanzibar inataka kuwa huru kujumuika kimataifa,kuingia katika mikataba ya kimataifa kama Zanzibar na kukopa kama Zanzibar,kwa kutaja machache. Kwa hali ilivyo hivi sasa na kung'ang'aniwa kwa mfumo huu wa Muungano wa Serikali mbili,Zanzibar haiko mbali kupata nguv kamili kama Taifa linalojitegemea. Ushirikiano wa kimataifa tu ndiyo ndoto iliyobaki kwa Zanzibar.
Tanganyika yetu iko wapi na itarudi vipi?
Au sio chukua tano hizo, ila unapingana na mwenyekiti...Tanganyika unayoiuliza iko wapi? aliiua Nyerere. Kuidai hivi sasa ina maanisha fikra za Nyerere zife na si zidumu tena.
Ni Watanzania wangapi leo hii wanaoweza kupinga fikra za Nyerere kwa makusudi kabisa?
Kuirudisha Tanganyika ni kuzidi kumpeleka mbali na utakatifu mwenyeheri Nyerere.
Muujiza wa kumfikisha Nyerere kuwa mtakatifu unakuwa rahisi sana nchi ikitoka kwenye serikali mbili ikawa moja. Itakuwa ni muujiza wa Nyerere umetimia, kuitawala nchi yenye zaidi ya asilimia 98 Waislaam na kuiingiza kwenye Serikali moja isiyo na dini.
Kumbuka, serikali ya Zanzibar ina dini na dini yake ni Uislaam na kadhi wanae.
Kufanya nchi iwe na Serikali tatu ni kuiuwa ndoto ya wanaompenda Nyerere awe mtakatifu. Linawezekana hilo?
Mimi natamani hata muungano usiwepo kama inawezekana, ikishindikana basi hizo tatu ndio pendeleo langu. Nakuhakikishieni na hilo ndilo pendeleo la Waislaam walio wengi.
Eti mkipitisha serikali tatu Jeshi litachukua uongozi wa nchi!!! Bullshit!!...wazanzibari wanataka nchi yao,watanganyika nao sasa wanataka nchi yao na ccm wanataka wabiki na tanzania...watanganyika na wazanzibari wakichukua nchi zao,je ccm watabaki na nini?...kumbe ndo maana ccm wanayapinga maoni ya wananchi wa Tanganyika na Zanzibar!!!???..
Kweli kabisa, sisi tunawabembeleza wao hatutaki
Eti mkipitisha serikali tatu Jeshi litachukua uongozi wa nchi!!! Bullshit!!
Hivi zanzibar ikijitenga na tanganyika ikajitenga nani atalipa deni la taifa? Au tutaligawa nusu kwa nusu
Hivi zanzibar ikijitenga na tanganyika ikajitenga nani atalipa deni la taifa? Au tutaligawa nusu kwa nusu
faizaFox inaonekana wewe ni mtoto wa Aboud Jumbe, kama vile una hasira ya kudumu na Nyerere!!
Tanganyika hatuna nia ya kuikolonaizi ZNB, bali wenzako MaCCM wanalazimisha jambo lisilowezekana!!
ZNB ikichachamaa labda MaCCM wataona ukweli, na Tanganyika ipange muungano bora na ndugu zetu!!
Msimtukane Nyerere bure ,aliyeomba muungano ni Karume!!
Hivi zanzibar ikijitenga na tanganyika ikajitenga nani atalipa deni la taifa? Au tutaligawa nusu kwa nusu
Tambua Nyerere na karume waliasisi Muungano kwa lengo la kuja Kuwa na Serikari moja tu , vile vile walitarajia muungano utakuwa Ukiboreshwa kulingana na wakati . Sasa imekuwa Kinyume na matarajio ya Nyerere Ndio Maana Haya ya Watanganyika kuzinduka kutaka Nchi Yao yameanza, lakini Kama misingi ya awali ingefuatwa Leo hii kero za muungano ingekuwa ni Historia .Hivi sasa Zanzibar amevunja katiba anajiamulia mambo yake atakavyo, wamegoma kulipa Gharama za muungano kwa Miaka 47 sasa ! Hakuna anayethubutu kuwauliza Jambo Viongozi Wa Tanganyika wanawaogopa sana Wazenji hawana Sauti Zanzibar hususani Waziri Mkuu Hana chake hawezi kukomandi chochote Zanzibar ! Ujue wao chao ni chao pekee ikiwemo Ardhi , lakini cha Tanganyika ni cha Wote kisha wanapewa na Pesa ya kuwaliwaza pamoja na matumizi mengine . Ukweli Uchumi wa Tanganyika haukuwa Sababu ni kulemewa na zigo la Kuilea Zanzibar .Tanganyika unayoiuliza iko wapi? aliiua Nyerere. Kuidai hivi sasa ina maanisha fikra za Nyerere zife na si zidumu tena.