Zanzibar Hatarini zaidi

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Written by raha // 07/09/2012 // Habari // 19 Comments


UZANZIBAR BASI…SASA NI UTANZANIA. Ule ukoloni wa Tanganyika kutaka kuimeza zanzibar na kuwa nchi moja wazidi kupamba moto. Kwa taarifa tulizozipata ambazo si rasmi mpaka sasa kunatetesi kuwa Wazir wa nchi ofisi ya Rais Mwinyi Haji Makame anataka kupeleka mswada barazani wa kukifuta kitambulisho cha Uzanzibar ili kukipitisha kitambulisho cha Mtanzania kufanya kazi zanzibar.

Hii ni ile mikakati serikali ya umoja wa kitaifa na sera ya chama cha ccm kutoka serikali 2 kuelekea 1.na nchi iwe ni moja nakuwa TANZANIA. Kampeni ya kukikaribisha kitambulisho hicho ishanza na Dr shein kuwataka wazanzibar wajitokeze kwa wingi kuvichukua. JAMANI HIVI TUNAENDA MBELE AU TUNARUDI NYUMA,KWA KWELI NAKUMBUKA MANENO YA AMIR WANGU SH MSELLEM ..KATIKA VYAMA VYETU TUNAEKEWA MAKUMBI NA BADO TUNACHAGUA HAYO HAYO.

Tunaposema ukweli watu wanaumia kuwa sasa SIASA NA VYAMA TUWEKE PEMBENI TUWE PAMOJA na MAAMIR WETU TUKOMBOE NCHI YETU. WAZANZIBAR MUKO TAYARI KUVIKATA VITAMBULISHO VINAVOTOKA TANGANYIKA ILI TULINDE HESHMA NA HADHI YA NCHI YETU.


Imetolewa na JUMIKI.



logo.png
 


Chama CHA MAPINDUZI hakiwezi kuongoza TENA; Viongozi wake hawawezi kuhamasisha WANANCHI hata kidogo bila Wananchi kuwa na DUKUDUKU lao;

Sasa VITAMBULISHO vya TAIFA DR. SHEIN na SERIKALI yake YASHINDWA kuwaelezea Wananchi wa Zanzibar UMUHIMU wa VITAMBULISHO vya TAIFA

Ma-AMIR WAMEWEZA KUWAELEZEA WANANCHI NIA YA SERIKALI YA CCM na IMEWAELEZEA NIA YA SERIKALI SIO NZURI KWA UPANDE WA ZANZIBAR

Sasa Wananchi Wa Zanzibar Watagomea... Ni nani wa kulaumiwa HAPO? UBUTU WA serikali KUU... Rais wa Jamhuri ya Muungano Kikwete yeye anaenjoy

Safari za Ndege na kumbeba ZITTO KABWE... Kweli Hawajui ni nini kinachoisakama NCHI? Rais Hasemi Chochote hata akisema hawamsikilizi?

INASIKITISHA...
 
Haya yetu macho, hakuna kitu kibaya kama nchi kuunganishwa kwa uadui na nchi nyingine, uniting to fight a common enemy Tanganyika. Mkimaliza hapo mtarudi kule kule mlikotokea.
 
itakuwa nafuu kwa wazenji maana kainji kao kenyewe kadogo, ngoja waje wayajaze mabonde na milima ya huku bara...
 
..huyu mtoa hoja ni mbinafsi.

..anataka wa-Tanganyika wazuiwe kufanya kazi Zanzibar.

..hivi yuko tayari wa-Tanganyika nao wawazuie wa-Zanzibar kufanya kazi na kujipatia rizki ktk ardhi ya Tanganyika??
 
B ila shaka kitambulisho cha Utanzania hakija kubalika zanzibar kwa kuwa Zanziabr pia wana vitambulisho vyao vya Uzanzibari. Kama ni nchi moja kwanini kuwe na vitzmbulishio karibu sabini?. Iko tatizo hapa hapa. Wazanzibari wana vitambulisho vyao na watanganyika wawe na vyao. Sisi wazanzibari tunajitambulisha kote ulimwenguni kama wazanzibari kwanza baadae n dio tanzania kwa shinikizo wala sio hiari.
Wazanzibari wanataka nchi yao huru. Tatizo ni ukoloni. Tunaweza kudumisha uhusiano wetu tukiwa mbalimbali kuliko hali ilivo sasa hivi.
 
written by raha // 07/09/2012 // habari // 19 comments


uzanzibar basi…sasa ni utanzania. Ule ukoloni wa tanganyika kutaka kuimeza zanzibar na kuwa nchi moja wazidi kupamba moto. Kwa taarifa tulizozipata ambazo si rasmi mpaka sasa kunatetesi kuwa wazir wa nchi ofisi ya rais mwinyi haji makame anataka kupeleka mswada barazani wa kukifuta kitambulisho cha uzanzibar ili kukipitisha kitambulisho cha mtanzania kufanya kazi zanzibar.

Hii ni ile mikakati serikali ya umoja wa kitaifa na sera ya chama cha ccm kutoka serikali 2 kuelekea 1.na nchi iwe ni moja nakuwa tanzania. Kampeni ya kukikaribisha kitambulisho hicho ishanza na dr shein kuwataka wazanzibar wajitokeze kwa wingi kuvichukua. Jamani hivi tunaenda mbele au tunarudi nyuma,kwa kweli nakumbuka maneno ya amir wangu sh msellem ..katika vyama vyetu tunaekewa makumbi na bado tunachagua hayo hayo.

Tunaposema ukweli watu wanaumia kuwa sasa siasa na vyama tuweke pembeni tuwe pamoja na maamir wetu tukomboe nchi yetu. Wazanzibar muko tayari kuvikata vitambulisho vinavotoka tanganyika ili tulinde heshma na hadhi ya nchi yetu.


imetolewa na jumiki.



logo.png
wa zanzibar ni wabinafsi, zanzibar hakuna rasilimali yeyote ya maana zaid ya karafuu, lakini wamekuwa na gubu ilhali wao ndio wamewekeza zaid huku bara

wa zanzibari wamepewa fursa kubwa kisiasa na ki uchumi, kisiasa wanaweza kupata nafasi yeyote bara lakini mtu wa bara hawezi kupata hata ujumbe wa mtaa

ki uchumi na kijamii ni rahisi mzanzibari kupata eneo na hata kufanya biashara huku bara kuliko m bara kwa zanzibar

lakini ukipita mitaani zanzibar ni kila siku maneno hayaishi unakuta stika zinasema 'zanzibar tuachwe tupumue' 'usiseme muungano ni mkataba tuuu' kwenye maskani ni uchochezi kila uchao

mimi naona wazi wakati umefika, kura ya maoni ipigwe kwa uhuru na haki then ikionekana haja ya kuvunja muungano na uvunjwe ili mpinduane pinduane kama madagaska, leo ustadh juma kawa rais kesho maalim hussein keshokutwa tunawakatia umeme na mlivyo na kiburi mtauzwa mchana kweupe
mtarudishwa enzi za usultani

shauri zenu na fikra zenu!
 
wamejazana udom kwanini wasisome na kufanya kazi zanzibar universty kama hawatutaki kwanini wanang'ang'ania huku bara warudi kwao na waseme hatutawataki watanganyika ndio tutawaheshimu lakini lawama zote wanatoa na hali wamejazana huku
 
wamejazana udom kwanini wasisome na kufanya kazi zanzibar universty kama hawatutaki kwanini wanang'ang'ania huku bara warudi kwao na waseme hatutawataki watanganyika ndio tutawaheshimu lakini lawama zote wanatoa na hali wamejazana huku

wewe jamaa mjinga sana hivi hujui kua hata mtakatifu nyerere kua alisoma makerere uganda? Je nae alikua mganda?

Heb njoo utembee zanzibar utoe ushamba mana naona uko mbali sana kwenye vijiji vya mkoa wa dodoma huko ambako watu hata gari kwao ni ajabu.

Ujue tu kuna wageni kibao wanaosoma udom ambao si watanzania je nao waondoke?

Istoshe udom imejengwa kwa fedha ya jamhuri ya muungano ya tanzania hivyo basi wazanzibari wana haki kufaidi nguvu zao.
 
Mtabe,

..sasa kama nyinyi mko huku Tanganyika, kwanini mnatuzuia tusije Zanzibar??

..sisi hatuna tatizo ikiwa mtapenda kuvunja muungano, tatizo ni haya mambo yanayoleta chuki miongoni mwa wananchi.
 
Last edited by a moderator:
..huyu mtoa hoja ni mbinafsi.

..anataka wa-Tanganyika wazuiwe kufanya kazi Zanzibar.

..hivi yuko tayari wa-Tanganyika nao wawazuie wa-Zanzibar kufanya kazi na kujipatia rizki ktk ardhi ya Tanganyika??

Ni wabinafsi tu hawa...wanabahati Malecela angechukua nchi kipindi ile saa hii lugha ingekuwa nyingine...wakishiba wali wa Shinyanga tu uamsho unaanza..
 
Kuna kitu kinafurahisha sana,

Kuna baadhi ya nchi wanamsimamo mkali dhidi ya nchi zingine utasikia ma-zionist nk, lakini ukienda kwenye ubalozi wa zionist hao hao wamepanga msululu wakitaka viza. sikatai u-zionist lakini kama unaukataa u-zioninist ukiwa nje kidogo tena nchini kwako kwanini utake viza uende ukaji- subscribe kule ndani kabisa yani kwenye backborne yenyewe? kweli sipati jibu.
 
B ila shaka kitambulisho cha Utanzania hakija kubalika zanzibar kwa kuwa Zanziabr pia wana vitambulisho vyao vya Uzanzibari. Kama ni nchi moja kwanini kuwe na vitzmbulishio karibu sabini?. Iko tatizo hapa hapa. Wazanzibari wana vitambulisho vyao na watanganyika wawe na vyao. Sisi wazanzibari tunajitambulisha kote ulimwenguni kama wazanzibari kwanza baadae n dio tanzania kwa shinikizo wala sio hiari.
Wazanzibari wanataka nchi yao huru. Tatizo ni ukoloni. Tunaweza kudumisha uhusiano wetu tukiwa mbalimbali kuliko hali ilivo sasa hivi.

Hapo kwenye red wakati mnajitambulisha huko ulimwenguni mnakuwa mnapeperusha bendera ya taifa lipi na pasipoti hipi?.
Kazi kwelikweli kumlea mtoto wa kambo jamaa mmoja aliniambia kuwa kama mke anakuja na mtoto wa kambo kumfahamu vizuri na kumweka katika mstari ulionyooka sharti mama mtu akupe manual yake kama ya TV ukaisome kwa makini ujue volume ilipo channel uziset vipi na mambo kadhawakadha kabla shughuri pevu haijaanza.
 
Matatizo yapo kwenu wabara. Ndugu zetu nyinyi mumaktaa kuwafahamu wazanzibari. Huu ukaidi wenu ndio unawasukuma wazanzibari kudai nchi yao. Hamuna lugha ya upole. Mawaziri wenu, ambassadors wenu, viongozi wenu na hata walalahoi wanawadharau sana wazanzibari. Wazanzibari wamechoshwa na udanganyifu na kuburuzwa na serikali ya Tanganyika kwa jina la muungano. Basi wakati umefika. Muungano kuvunjika ni kama kufa. Kila mtu atakufa na muungano pia unakufa. Sasa hivi muungano upo ICU(coma).
 
Falconer,

..lakini mbona ni nyinyi toka zama zile mnatuita vichogo? je hiyo siyo dharau?

..wewe unaweza kuchangia hoja zako hapa JF, wakati mimi Mtanganyika siruhusiwi kuchangia mzalendo.net au zanzinet. je, huo siyo ubaguzi??

..halafu mnataka kuleta vitambulisho ili kuwanyima ajira wa-Tanganyika wanapokuwa Zanzibar. wakati huohuo Tanganyika imepokea wa-Zanzibari wanaokadiriwa kufikia 350,000. je, huo siyo ubinafsi??

..wa-Zanzibari mkiacha dharau, ubaguzi, na ubinafsi, basi bila shaka mtaweza kuishi vema ndani ya muungano huu.
 
Falconer,

..lakini mbona ni nyinyi toka zama zile mnatuita vichogo? je hiyo siyo dharau?

..wewe unaweza kuchangia hoja zako hapa JF, wakati mimi Mtanganyika siruhusiwi kuchangia mzalendo.net au zanzinet. je, huo siyo ubaguzi??

..halafu mnataka kuleta vitambulisho ili kuwanyima ajira wa-Tanganyika wanapokuwa Zanzibar. wakati huohuo Tanganyika imepokea wa-Zanzibari wanaokadiriwa kufikia 350,000. je, huo siyo ubinafsi??

..wa-Zanzibari mkiacha dharau, ubaguzi, na ubinafsi, basi bila shaka mtaweza kuishi vema ndani ya muungano huu.
Hiyo ipo kwenye DNA Mkuu usiwape wanasayansi kazi kwa ajili ya jumuiya ya watu Milioni 1.
Vitambulisho hawata vikataa, vitagombewa ka vitumbua vya Temeke Wailes. Kwani umeshasikia wakidai Passport yao!
Unaweza kudaia kitambulisho cha kuingia nyumbani kwenu! Vya bandarini wamekataa hawataki kusikia habari hiyo
Wanataka Tanzania iwe yao na ZNZ iwe yao, the time has come LET ZNZ GO!
 
Back
Top Bottom