Zanzibar 2020 Zanzibar: Hali si shwari. Vurugu zaibuka na watu kadhaa wanadaiwa kujeruhiwa vibaya

msokela

JF-Expert Member
Apr 18, 2018
585
500
KILICHOTOKEA MICHEWENI, ZANZIBAR

Watu walikuwa na mkutano wa Jimbo la Micheweni wamemaliza saa 12 watu wakaanza kurudi majumbani.

Kuna wanachama wa ACT, Shumba Mjini wakapita katika kijiji cha Kwale Kijiji ambacho kina CCM wengi.

Kilichotokea CCM wakawachokoza ACT wakaanza ugomvi wakaja Polisi. Usiku huu mabomu yanaendelea na Askari wanazidi kumiminika. Watu wanapigwa sana

Mpaka sasa kuna wengine wako hospitali Micheweni wengi wameumizwa.

View attachment 1602557

ILANI: Video niliyoipata haifai kukaa hapa kwani inatisha
Mbona Kama nachezewa picha hapa ili kuogopesha wananchi Kama sisi tupo.
 
1000 digits

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
4,830
2,000
Zanzibar kuna jambo lawezatokea, mwaka huu.

Kikwete aliturudisha nyuma sana aliposhindwa kuheshimu Uchaguzi wa Zanzibar na kukubali Jecha kufuta ucbaguzi kinyume cha sheria.
CCM wakashinda kwa hila wakati Shein alipaswa kuwa Makamu wa Rais na nchi ikasonga mbele na Wazanzibari wakaendelea kuwa wamoja.

Sasa wananchi wa Zanzibar albao Kiuhalisia wana maisha Magumu sana huku Viongozi wao wanaotokana na Chama cha mapinduzi wakijineemesha na kutumia Jeshi la Polisi kuwatesa wananchi.
Tuliombe Jeshi la Polisi kuacha kutumia Risas kuwabeba CCM.

Siku watakapogundua kuwa CCM ni hatari kwa kila mwanadam hata kwao wenyewe ndipo watakapoona kuwa walichelewa sana kuachana na siasa za uonevu.

Wanaoumizwa na Amani kuvurugika Zanzibar Sio Mabilionea waliojificha Chini ya CCM bali ni polisi wenyewe wanaojiingiza kwenye uhasama na wananchi na kujikuta wakifarakana na kila mtu.

Hivi kweli kuna askari wadogo kwenye jeshi lolote anayetumia akili yake na kutafakari amaweza kuvuruga jamii ili Mtoto wa Rais ,Hasan Mwinyi aliyekaa kwenye Uwaziri kwa miaka 25 na kuishi maisha kama Peponi tangu kuzaliwa ,eti awe Rais kwa dhulma ?

Askari anayeweza kuwaua watu ili tu Mwinyi apate Urais atakua anajipandikizia laana kubwa san a Duniani na Ahera. Hata Mungu atakua anamcheka huyo askari. Hata shetani na uovu wake hajafikia kiwango cha ubaya wa askari wanaowatetea walioshiba na kuwadhulumu wenye njaa .

Polisi tambueni tu kuwa Mwinyi hana alichokosa zaidi tu ya uroho na ubinafsi wa roho za binadam wasio mcha Mwenyezi Mungu kukosa shukrani na kuridhika hata angepewa dunia nzima nado haridhiki.
Polisi wanapozidi kukubali kutumiwa na raia wahalifu waliojificha chini ya CCM wajue kuwa wanawagawa wazanzibari na wanatengeneza Chuki kubwa sana badala ya umoja. WanaCCM kwa uhalifu wao wanatumia madaraka yao kuwaamrisha askari kuwaumiza wananchi ili tu kulinda maslahi yao na madarka yao.

Mfano ni Kule chato WanaCCM na wauaji wakubwa waliotaka kumuua Lisu miaka mitatu iliyoputa waliendeleza uhuni wao lakini hatukusikia kuwa wamekamatwa wala kutafutwa zaidi ya maneno ya kusema amani bila vitendo.
 
1000 digits

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
4,830
2,000
Vikosi vyetu vya ulinzi viko busy na uchaguzi huku wakiacha ndugu zangu wa nanyamba kitaya wakiuawa na magaidi...
CCM wameona Bora uchaguzi kuliko maisha ya raia wao wa kusini

Kama kuna watu watakuja lupata laana kubwa sana ya kila damu inayokwagika hapa Tanzania ni Popepole na Bashiru.

Hawa watu Waliopata umaarufu Mkubwa kupitia Katiba Mpya weshindwa kushauri Mh. Rais wakati wanajua kuwa Rais wetu siao Mwanasiasa.
Aliwaweka kwenye nafasi hizo akitegemea kuwa wangemsaidia katika suala la katiba mpya na umuhimu wake katika kujenga mifumo imara ya nchi.
Nchi zote ambazo majeshi yanajiingiza kwenge siasa zinakua na mfumo dhaifu katika ulinzi wa watu na mali zao.
Ni rahisi adui kujiunga na wale wanaoonewa na kuweza kufanya hujuma. Hili ni yatizo kwenye nchi zisizo na demokrasi ya kweli.

Bashiru ni msomi mbobevu kwenye suala zima la Sayansi ya Siasa ,anajua wazi kuwa Demokrasia na utawala bora zina misingi na kanuni zake ambazo zijajenga amani .Hata hivyo ameshindwa kumshauri Rais kwa hilo.
Vitabu vya dini vinasema ukijua Jambo jema halafu ukashindwa kulitenda basi kwako litahesabiwa kuwa ni dhambi.
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
25,800
2,000
baadhi ya wapemba huwa wazuri sana kwenye kuharibu uchaguzi wakiongozwa na seif sharrif Hammad washaanza vituko vyao,Usishangae ACT WAZALENDO kujitoa uchaguzi Zanzibar
 
AGITATOR

JF-Expert Member
Apr 7, 2019
974
1,000
KILICHOTOKEA MICHEWENI, ZANZIBAR

Watu walikuwa na mkutano wa Jimbo la Micheweni wamemaliza saa 12 watu wakaanza kurudi majumbani.

Kuna wanachama wa ACT, Shumba Mjini wakapita katika kijiji cha Kwale Kijiji ambacho kina CCM wengi.

Kilichotokea CCM wakawachokoza ACT wakaanza ugomvi wakaja Polisi. Usiku huu mabomu yanaendelea na Askari wanazidi kumiminika. Watu wanapigwa sana

Mpaka sasa kuna wengine wako hospitali Micheweni wengi wameumizwa.

View attachment 1602557

ILANI: Video niliyoipata haifai kukaa hapa kwani inatisha
Hii ndio hasa wanachotaka wapinzani, shame on you. Tunu ya Amani lazima ilindwe kwa gharama yoyote.
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
148,406
2,000
KILICHOTOKEA MICHEWENI, ZANZIBAR

Watu walikuwa na mkutano wa Jimbo la Micheweni wamemaliza saa 12 watu wakaanza kurudi majumbani.

Kuna wanachama wa ACT, Shumba Mjini wakapita katika kijiji cha Kwale Kijiji ambacho kina CCM wengi.

Kilichotokea CCM wakawachokoza ACT wakaanza ugomvi wakaja Polisi. Usiku huu mabomu yanaendelea na Askari wanazidi kumiminika. Watu wanapigwa sana

Mpaka sasa kuna wengine wako hospitali Micheweni wengi wameumizwa.

View attachment 1602557

ILANI: Video niliyoipata haifai kukaa hapa kwani inatisha
Naiomba PM tafadhali
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
148,406
2,000
Hapo watawakamata ACT tu, polisi atakaejiroga kuwakamata CCM ataogelea hadi tanga
JamiiForums1130837909.jpg
 
zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
1,260
2,000
jamani ndugu zetu wa zanzibari punguzeni presha hizi ni siasa tu ugomvi wa nini jamni, sasa kama siasa ni kukatana mapanga basi bora tusiwe na uchaguzi. sisi watanzania hatupendi kuona mtanzania mwenzetu hata mmoja anamwaga damu kwa ajili ya siasa....hakuna sababu....haswa vijana acheni mizuka ya bangi mtakufa buree
 
mugah di mathew

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
3,234
2,000
KILICHOTOKEA MICHEWENI, ZANZIBAR

Watu walikuwa na mkutano wa Jimbo la Micheweni wamemaliza saa 12 watu wakaanza kurudi majumbani.

Kuna wanachama wa ACT, Shumba Mjini wakapita katika kijiji cha Kwale Kijiji ambacho kina CCM wengi.

Kilichotokea CCM wakawachokoza ACT wakaanza ugomvi wakaja Polisi. Usiku huu mabomu yanaendelea na Askari wanazidi kumiminika. Watu wanapigwa sana

Mpaka sasa kuna wengine wako hospitali Micheweni wengi wameumizwa.

View attachment 1602557

ILANI: Video niliyoipata haifai kukaa hapa kwani inatisha
Usalama wa Zanzibar ni kumtangaza maalimu kuwa mshindi
 
mambio

JF-Expert Member
Mar 4, 2017
1,165
2,000
Vikosi vyetu vya ulinzi viko busy na uchaguzi huku wakiacha ndugu zangu wa nanyamba kitaya wakiuawa na magaidi.

CCM wameona Bora uchaguzi kuliko maisha ya raia wao wa kusini
Umeelewa alicholeta mleta mada?
Na ulichokiandika wewe umekielewa?
 
gigabyte

JF-Expert Member
May 27, 2015
1,611
2,000
Hahaha watanzania kwa kuzusha, sasa hapa vurugu ziko wapi?! Majeraha kama hayo hata Dispensary ya ikulu yapo.

Mtu anachukua picha hospitali analeta humu, anatia watu taharuki.

Hata ukienda Tandale Hospitali watu wanaokuja na majeraha madogo madogo kama hayo wapo, sasa jeraha linahashiria kwamba kuna vurugu?!

Kesho nami nitapiga picha hapa emergency room Muhimbili na nitaleta humu na kusema Dar es salaam hali siyo shwari kabisa.

Hapo nini kinasema kwamba kuna vurugu Zanzibar?!
Acha ujinga na wewe.ulitaka akuletee mkanda mzima wakila tukio kwani ni filamu hiyo.Hiyo picha kaonyesha tu sehemu kidogo kama kielelezo wala sio ndo tukio zima.Unachotakiwa kufanya nikufwatilia kwenye vyanzo vingine ili ujiridhishe kwamba je ni kweli vurugu zimetokea au hazijatokea nasio kukomalia picha kana kwamba ndo habari yenyewe.Au wewe ulitaka uwekewe picha ya watu wanakatwa shingo ndo ufurahi kua kweli kuna vurugu zimetokea.Unakwama wapi kuelewa mambo madogo kama hayo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom