Truth Well Told
Member
- Oct 26, 2013
- 31
- 13
Hakuna pesa Tanganyika inadaiwa.
Ninyi hamjui kuhusu mgao mnaoupata kila mwezi. Hamjui huduma ambazo mumezipata kwa miaka 50 na leo watu wenu wanaweka wazi kabisa kuwa muungano uliendeshwa na kodi za Watanganyika.
Vunjeni muungano mdai machodhani kama hamtajikuta mnauza kisiwa chote.
Tumewaambi siku nyingi kuhusu gharama za muungano. Leo maji yamewafika shingoni mnalalamika kuhusu udogo.
By the way ninyi vijana wa Tanganyika mliokosa mikopo iulizeni serikali yenu kwanini mkose mikopo ili hali pesa za kodi za baba zenu zinakwenda ZNZ kwa mikopo ya wananfunzi wa 1) Kusoma bila kurudisha mikopo 2) Kupewa hata nafasi zenu kwasababu tu ya uzanzibar..
Eto hawataki muungano wakati wapo Dodoma! thubutu nani asiyependa sh ya Tanganyika!
Wanajiandaa kuongeza wajumbe waje kwenye bunge la katiba badala ya kuwakataza, huku uvunguni mwa vitanda wanapiga domo hawataki muungano.
Tumechoka kusikia kelele zenu tuna mambo mengi ya muhimu. Hatuwezi kuishi kwa kuwabeba mkicheza msewe halafu mnataka vyeo na ajira. This time around pasu pasu kama hamtaki njiaa nyeupee bandarini rudini mkaijenge znz ya pembe za ndovu na watumwa. Znz iliyokuwa inagawa sambusa barabarani na mapilau katika vituo vya mabasi, znz yenye neema.
Tuwabebe halafu mtukane! ebo! leo mnasema bila haya hamjiwezi! mkiondoka hapo mumechukua posho mnaelekea bandarini na matusi. Posho za Mtanganyika! tumechoka kelele na midomo yenu.
Tatizo leni si muungano ni jingine linalohitaji kampeni ya Lowasa.
He he hee! Misaada!... kama Znz itachwa iwe huru kabisa kiuchumi yaani kupata misaada...
Sijakusoma Mkuu,
Ina maana Zanzibar inaidai Tanganyika?
He he hee! Misaada!
Sicheki nchi kupata misaada, ila kutaka uhuru ili ipate misaadasasa hapo kinakuchekesha nini!? Kwani ni lini hiyo Tanganyika aka JMT iliacha kupata misaada toka nje tangia ipate ule "uhuru" wake!?
Zanzibar iache unyanyasaji wa raia wenye asili ya Bara.
Sicheki nchi kupata misaada, ila kutaka uhuru ili ipate misaada
Mwenyekiti wa kamati yako kasema hamtaweza kwasababu mapato yenu ni bilioni 240.
Hapo hakuna bajeti ya ulinzi, mambo ya ndani, elimu ya juu achilia mbali mishahara na mambo mengine
Jiulize kwa bajeti ya znz ya bilioni 700 na mapato ya bilioni 240 pengo linazibwa na nani.
Nikuulize tume ya warioba mumechangia kiasi gani?
Bunge la katiba mtachangia kiasi gani.
Kelele kila siku mnanyonywa wakati ni kupe wakubwa.!
siyo six wala 4 hiyo ni udom anayoitolea masimbulizi.
Mwiba, gombesugu,
..Zanzibar ni ndogo kieneo na kiuchumi.
..kuitia ktk muungano na Tanganyika ni kutafutana ubaya na lawama.
..haya mambo tumekuwa tukiyasema kwa muda mrefu sana hapa JF.
..tunaposema hayo wengine mnafikiria tumeamua kuwavunjia heshima lakini huyo mwakilishi kasema ukweli.
..labda nikupeni mfano mdogo: kabla ya mapinduzi Znz majimbo ya uchaguzi yalikuwa hayazidi 30. sasa hebu angalia wakati huu tuna muungano Znz ina majimbo mangapi ya uchaguzi? majimbo yameongezwa Znz ifanane-fanane na Tanganyika.
cc Nguruvi3, Barubaru
Mkuu Nguruvi kumbe na Wewe unatukanaga yaani wazanzibar ni kupe futa kauli yako mkuu.
Mwenyekiti wa kamati yako kasema hamtaweza kwasababu mapato yenu ni bilioni 240.
Hapo hakuna bajeti ya ulinzi, mambo ya ndani, elimu ya juu achilia mbali mishahara na mambo mengine
Jiulize kwa bajeti ya znz ya bilioni 700 na mapato ya bilioni 240 pengo linazibwa na nani.
Nikuulize tume ya warioba mumechangia kiasi gani?
Bunge la katiba mtachangia kiasi gani.
Kelele kila siku mnanyonywa wakati ni kupe wakubwa.!
Mapato ya Tanganyika ni kiasi gani?Kwanini tusiweze mwanzo tuliwezaje hadi sasa tushindwe kwani nyinyi bajeti yetu munaishi vipi si kwa misaada toka kupata kwenu uhuru ndo maana nasema munajitia upofu musonao, sisi tu munaitizama bajeti yetu lakini yenu kimyaa tena basi kwa upumbavu wenu munaona kama sisi hatujui kama munaomba kwa kwa kutumia jina la TANZANIA na si kwa Tanganyika na si hamjui kwamba hamjui ni wizi tuu nitakupa kidokezo ukisoma ibara ya kwanza 1(a) 1977 inasema TANZANIA NI JAMHURI HURU ILIYOUNGANA sasa chochote ambacho kinaombwa kwa kwa jina la Tanzania ni cha wote na kile ambacho munaomba kwa Tanganyika ni cha kwa Tanganyika peke yake UNLESS STATED OTHERWISE (TANZANIA IS TANGANYIKA.)TUACHIWEEEE TUPUMUWEE 50 YRS IS ENOUGH.
Kama watoto wanasoma hujui wanasomeshwa na nani, kama unawasha umeme hujui unalipiwa na nani, kama unapata mshahara hujui chanzo chake na kama unaalikwa Dodoma na kupewa pesa nusizojua zinatoka wapi wewe ni KUPE.Mkuu Nguruvi kumbe na Wewe unatukanaga yaani wazanzibar ni kupe futa kauli yako mkuu.
Si kweli, hakuna mzanzibar anayethubutu kudai nchi yake.Mimi sipendi kubishana na kichwa maji., ww ungekuwa mzalendo wa kweli na unaipenda nchi yako kwanza ungesimama kidete ukaidai Tanganyika yako kama tunavyoidai sisi Zanzibar yetu, ili utoke katika utumwa wa mkoloni mweusi.
Zanzibar kuwa na uwezo ama kutokuwa na uwezo kuichangia serikali ya muungano si muhimu tn kwa sasa na imeshapitwa na wakati., Muungano ni jambo la hiyari sisi tumeamua kuidai nchi yetu. Historia inaonyesha Zanzibar ilikuwa nchi huru ambayo ikijiendesha mambo yake kwa salama kabisa kabla ya kuungana na Tanganyika.
Kinachowauma Tanganyika leo ni kuona zanzibar inadai mamlaka yake iliyokuwanayo hapo awali na ndo sasa munatafuta sababu na visingizio ambavyo kutokana na muda sasa ni kama ''Kujamba Mtoni'' we will not stop mpaka bendera ya Zanzibar ipepee UN. Kwanini Tanganyika muumie kwa Zanzibar kudai mamlaka yake? Kwanini mutunganganie na hatuwataki?.
Zanzibar ilitoa herufi 3 na Tanganyika heruf 3 tukatengeneza neno Tanzania. Kwaiyo sisi tunadai zanzibar yetu nyinyi rudieni jina lenu la awali Tanganyika msikubali utumwa wa kijinga jinga., mulipaswa na nyinyi kuwa mstari wa mbele kudai mamlaka ya Tanganyika yenu.
Tuachieni pilau yetu ndio chakula wanachokula watu wenye fedha duniani nyinyi pigeni ugali wenu na madagaa pamoja na viazi vitamu ule msimu ukifika .,,