weli hatutaki muungano na mafuta yetu hivi hamjui? au mnataka kuendelea kutunyonya? na kutuibia rasilmali zetu za mafutana bahari kuu?
Hizi ndizo hoja zinazotakiwa kwenye Muungano. Kwa maana nyingine, serikali ya Zanzibar haitaki serikali tatu wakati pia wanadai serikali mbili zinawanyonya!. Hoja iliyojificha hapa ni kuwa, Wazanzibar hawataki muungano. Finito.
Siyo jambo la kushangaza kusikia hoja kama hii kisiasa kwa sababu serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaongozwa kwa kiasi kikubwa na sera za CCM ambapo serikali mbili ndiyo sera yake na pia Salimin Awadhi Salimin ni mwakilishi kupitia tiketi ya CCM.
Hakuna haja ya kuwa na muungano kama hakuna manufaa endelevu kwa wananchi wake. Swala la kuwa kwenye muungano ambapo msingi wake mkuu ni siasa halina mashiko hata kidogo katika dunia ya sasa inayonyambulishwa kiuchumi zaidi.
Bila kujali anachokisema ni sera ya CCM, fact always fact hasa katika uhalisia wa jambo ambalo linahusisha uchumi. Watanganyika lazima tuuangalie muungano kiuchumi zaidi na katika uchumi ndipo tunapata gharama za serikali tatu halafu vile vile kuna kuchangia gharama za EAC achilia mbali regional economic, political and security cooperation schemes with other nation. Hizi ni gharama kubwa sana na sidhani kama Watanzania wanapata value for their tax money.
Kwa nini tusiachane na Zanzibar na tukakutana nao katika SADC kama member nation kitu ambacho ni political and economic sense kuliko kung'ang'ania kuwa na nchi ambayo haiwezi hata kulipa 10% ya gharama za Muungano.
Kiuchumi Tanzania itanufaika sana kuwa mwanachama wa SADC zaidi ya kuwa na muungano na Zanzibar na hasa iwapo watanzania watatumia ipasavyo nafasi hii kwa sababu ukiangalia total population and GDP kwa kila nchi inakupa wastani wa per capital $2,080.
Copy Barubaru chama gombesugu THE BIG SHOW ...................
Mwiba, gombesugu,
..Zanzibar ni ndogo kieneo na kiuchumi.
..kuitia ktk muungano na Tanganyika ni kutafutana ubaya na lawama.
..haya mambo tumekuwa tukiyasema kwa muda mrefu sana hapa JF.
..tunaposema hayo wengine mnafikiria tumeamua kuwavunjia heshima lakini huyo mwakilishi kasema ukweli.
..labda nikupeni mfano mdogo: kabla ya mapinduzi Znz majimbo ya uchaguzi yalikuwa hayazidi 30. sasa hebu angalia wakati huu tuna muungano Znz ina majimbo mangapi ya uchaguzi? majimbo yameongezwa Znz ifanane-fanane na Tanganyika.
cc Nguruvi3, Barubaru
Ngongo,
Sina hakika kwa undani zaidi na hayo matamshi ya huyo Bwana Kiongozi kama alivyonukuliwa na hilo jarida.
Insha Allah,tunafuatilia hizi khabar kwa utuvu...lakini nakhis yakuwa hayo ni mazungumzo tu ya kisiasa,kwa maana nyingine ni coded words za sisi kukwambiani nyinyi Watanganyika yakuwa huo Muungano hatuutaki tena,ushitushinda kwa mangi ya ulaghai na dhuluma!?
Hicho ni kipimo changu tu binafsi kiduchu kwa kuanzia,lakini tarejea tena hapa barzan kadri mnakasha utakavyoendelea.
Labda Mufti Barubaru,atakapopata fursa ya kujongelea hapa barzan yawezakuwa ana mangi ya kutujuza...maana yeye ni mbobefu wa mahisabu na takwimu hizo za fedha za kuendesha huo "Muungano".
Lakini pia tujikumbushe japo kiduchu,yakuwa kabla ya hizo Serikali tatu,italazim pia turejee nyuma kiduchu na kujikumbusha madeni ya Serikali ya Muungano/JMT,ambayo inadaiwa na Serikali ya Zanzibar!?
Sijawahi hata siku moja kuona member/s yeyote au hata thread yeyote humu JF,ikikumbushia zile "enzi za Mwalimu"; wakti Tanganyika na Serikali ya Muungano vikiwa taabani kiuchumi,na zikitegemea pita kiasi senti/akiba ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar-SMZ ili kujikimu na kujiendesha!?
Mnakumbuka yakuwa wakti ule wa ile vita ya Nyerere dhidi ya Uganda,SMZ iligharamia kwa kiasi kikubwa mno ile vita ambayo binafsi Wananachi wa Zanzibar wala Serikali yao haikushirikishwa kikamilifu kwenye yale maamuzi dhaifu ya Nyerere kungia vitani baada ya kumchokoza kwa makusudi yule mpuuzi Idd Amin kwa miaka kadhaa!?
Mnakumbuka pia,SMZ ililazimishwa na Nyerere kutumia akiba yake takriban yoote kugharamia yale yaliyoitwa ati "mapambano ya ukombozi wa nchi za Afrika"!?
Niwia radhi Mkuu,hapa silalamiki asilan,lakini ni muhimu pia kiduchu kujikumbusha fadhila,ihsan na madeni mangi mno dhidi ya hiyo Tanganyika aka JMT...ambayo(madeni dhidi ya JMT) mpaka kesho hayajawahi kuzungumziwa hata na Viongozi wowote wa ngazi za juu,na hatujui sababu ni ipi!?...labda woga,ubinafsi,uchu wa madaraka,vitisho au upumbavu wa fikra!?
Ahsanta.
Ndugu yangu ukiongelea muungano hutasikia mzanzibar akiongelea gharama hata siku moja.Wataongea tu, hakuna namna.
Kwa sasa tuna serikali mbili, serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Muungano -ambayo kimsingi inahusika na mambo ya Tanganyika na yale ya Muungano. Kama mwenyekiti anasema kuwa Zanzibar haina uwezo wa kuchangia Serikali ya Muungano endapo kutakuwa na serakali tatu, maana yake amekiri kuwa hata sasa hivi Tanganyika ndio inalipa 'bills' zote. Sasa huo unyonyaji aoimba Maalim Seif unatoka wapi?
Na siku zote tumekuwa tunasema hapa, madai ya pasu kwa pasu yasishie kwenye kuepeana nafasi za kazi peke yake, kila upande wa Muungano uwalipe watu wake.
Wasipokuwa makini hii inakula kwao, maana Tanganyika wamechoka kuitwa wakoloni, sasa watadai serikali moja au tatu.
wanataka nafasi za sawa za wabunge hizo tuwape ila tukija kwenye uchangiaji iwe 50 kwa 50 hawawezi watoke
Kila nchi ikusanye ushuru wake na pia kila nchi iweke viwango vyake vya kodi nyama,nyanya na mazao yote yanayotoka bara kwenda zanzibar yatozwe kodi sio wanakuja huku nakuchukua mazao halafu wanatufanya watu watanganyika bei inapanda
bidhaa watakazoingiza huku zitozwe kodi nchi yetu sio jalala wawe na mamlaka yao ya mapato na sisi tuwe na yetu tuone kama wataweza hata kujilipa mishahara ukifikiria juzijuzi jengo lao la baraza la wawakilishi limejengwa kwa fedha za muungano wanashindwa hata kujenga jengo la chombo chao kinachotumika kutunga sheria
Kila nchi iwe na shirika lake la umeme na walipe na pia kwa sababu kila nchi ina mamlaka yake ya kusimamia usafiri wa majini kila nchi ilipe kodi zake
kila mtu asiruhusiwe kumiliki ardhi kwenye nchi isiyo yake wala kumiliki majengo
baada ya hapo ndio tutajua nani anamnyonya mwenzake anayetaka kurudi inabidi aombe kwa kukubali masharti atakayopewa
Watapata msaada toka oman..
Achana nao wajinga hao znz mukiwachie itakuwa kama dubai
Yes, nilikuwa nina maana hiyo na nimebadilisha. Thanks kwa dokezo.Huwezi kula keki ukabaki nayo. Ninaamiini unapohitimisha kwa kutamka Tanzania una maana ya Tanganyika?
Ninakubaliana na point yako lakini huoni kuwa kuna matatizo mbele kwa sababu kama wameishasema hawawezi hata kulipia 10% ya mchango wa muungano ina maana hakuna faida ya kuwa na muungano kwa Tanganyika.Mawazo yangu ni kuwa huyu Bw Salmini anatetea sera ya Chama chake bila kuangalia mengine au anatuthibitishia kuwa wakati wote Tanganyika ilkuwa 'inaumia'. Pengine mapato yao yamefunikwa kwa kuwa ndani ya mfumo wa serikali mbili. Lakini pamoja na hayo kwa muundo wowote ule utatengenezwa utaratibu wa kugharamia uendeshaji wa serikali na vyombo vyote vya dola.
Tulieni! kasemea mwenzenu kuwa bajeti ya ulinzi na usalama ni trilion 1.3 ninyi bajeti ni 240bilioni. Lini Tanganyika itaitegemea znz. Leo tuna ushahidi kuwa kwa miaka 50 tumekuwa tunawalipia gharama halafu mnadai vyeo na nafasi za kazi.Kweli Zanzibar ni ndogo kieneo ila kiuchumi sidhani kama ilikuwa hivyo ila baada ya huu Muungano ndio mmetutilia ufukara na kutufanya tuwe watu duni sana ,mnataka tuwe tunategemea kila kitu kutoka huko Tanganyika na ndio kama inavyoonekana katika hoja zenu ,nyie nchi ndogo sijui uchumi wenu mdogo ,hebu ulizia na katafute historia ya Zanzibar ,Zanzibar wakati kabla ya Muungano ilikuwa vipi na ilitoa msaada kumsaidia nani ? Yakhe huu Muungano ukifa leo basi nakuhakikishieni machogo ,hautapita muda mrefu tutawasaidia tena tutawasaidia kwa ari na mori na moyo wa jeuri ,huko Tanganyika hamna kitu mmekalia kuti kavu. lazima mtapigana mapanga tu !
Hakuna pesa Tanganyika inadaiwa.Huyu Salimin Awadhi anachokiongea ata hakijuwi ni mbumbumbu wa kutupwa kabisa., kwani zanzibar hapo awali ilipoungana na Tanganyika zikawa nchi 2 huru lini ulisikia Zanzibar ina madeni inadaiwa na tanganyika kwenye Muungano zaidi ya kwamba sasa Tanganyika ndio inadaiwa hela nyingi sana na Zanzibar? fedha za benki kuu hadi leo.,
Kama Zanzibar hawawezi kuchangia serikali ya Muungano njia nyengine basi ni kuvunjwa Muungano ili Zanzibar iwe huru hayo madeni ya michango yaweze kuepukika kabisa.,
Milioni mbili kwa mwezi ndio zinamsumbua huyu Salmin Awadh.,