Zanzibar: Aliyembaka binti yake mwenye miaka chini ya 13 aachiwa huru, kwa ushahidi kuwa binti ni mzoefu

Zanzibar ubakaji ulishahalalishwa sema wanazuga tu kutokana na mambo ya haki za binadamu.
Kwa sheria zipi wakati kuna aheria zinazopitishwa na Baraza la wawakikishi na sheria zinazopitishwa na bunge zinafanyakazi? Wamehalalisha kwasheria zipi?
 
Hao TAMWA wanajielewa? Kama walikuwa na ushahidi nje na ule wa DPP ni kwanini hawakupeleka?

TAMWA hawajui kwamba mahakama husikiliza na kuamua kesi kulingana na ushahidi uliopelekwa mbele yake?

Halafu, kesi za jinai, ni wajibu kwa DPP kuthibitisha bila shaka, beyond reasonable doubt, kwamba mtuhumiwa katenda kosa. Yaani, siyo kazi ya mahakama, serikali, wananchi, wanaharakati, Wala mtuhumiwa kuthibitisha kwamba mtuhumiwa katenda jinai.

Halafu, shtaka la kubaka huwa linathibishwa na ushahidi Kwanza, kwamba mwathirika aliingiliwa yaani uu me wa mtuhumiwa uliingia. Halafu pili, uliingia bila ridhaa.

Kama mwathirika ni mtoto, basi inasadikika kwamba ridhaa haikuwepo.

Sasa nilitarajia, angalau, TAMWA watueleze na walete uchambuzi wa kina kuhusu namna mtuhumiwa alivyomuingilia muathirika, namna ushahidi ulivyokusanywa, jinsi mashahidi walivyojieleza, namna mtuhumiwa alivyojitetea nk yaani waeleze hatua kwa hatua.

Vinginevyo hizi ni blaablaa tu za kutaka kuingilia Uhuru wa mahakama, na kufanya harakati uchwara ili kupata pesa za mabeberu.
Mkuu, mbona umeandika Kama vile wewe ndiye PANGA LA SHABA mwenyewe?
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI​

TAMWA Zanzibar Hairidhishwi na Hukumu ya Kesi zinazohusu Ukatili wa Watoto.

Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA, ZNZ) haikuridhishwa na hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Wete Mkoa wa kaskazinia Pemba kwa kumuachia huru mtuhumiwa aliyembaka mtoto wake wa kumzaa.

Hivi karibuni TAMWA Zanzibar imepokea taaarifa kwamba mtuhumiwa Salim Khamis Ali maarufu “Panga la Shaba” (43) mkaazi wa Taifu shehia ya Kinyasini aliyembaka mtoto wake wa kumzaa huko Pemba ameachiwa huru kwa madai kuwa taarifa za daktari zimeonesha kwamba mtoto huyo ni mzoefu kwa maana ya kuwa ameshatenda tendo la ngono hapo awali.

Tukio hilo liliripotiwa katika kituo cha polisi Wete tarehe Desemba 6/ 2019 na kufunguliwa jalada namba IR471/2019 ambapo jalada hilo lilieleza kwamba Salim Khamis Ali anatuhumiwa kumbaka mtoto wake wakike aliye chini ya umri wa miaka 13.

Kwa mujibu wa hakimu wa Mahakama ya Wete Mkoa Kaskazini Pemba, Abdalla Yahya Shamhuni, ni kwamba mtuhumwa alitenda kosa Novemba 30, 2019 saa 3:00 usiku katika eneo la Taifu, ambapo bila ya halali mtuhumiwa huyo alimuingilia mtoto huyo huku akijua kuwa ni mtoto wake wa kumzaa, jambo ambalo ni kosa kisheria kwa mjibu wa kifungu cha 143 (1) (4) cha Sheria namba 6 ya mwaka 2018, Sheria ya Zanzibar ambapo kesi hiyo ilipewa nambari RM 4/2020.

Hakimu huyo alibainisha kwamba baada ya kukamilika kwa upelelezi kesi hiyo, Mahakama imemuachia huru mtuhumiwa tarehe Desemba 7/2020 kwa kile kinachodaiwa ushahidi wa daktari ulionyesha kuwa muathirika aliwahi kuingiliwa hapo awali.

“Katika maelezo yake daktari alieleza kuwa muathirika ni mzoefu. Hivyo basi baada ya kupitia vyema ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashitaka mahakama imeona kwamba mtuhumiwa si mkosaji wa kosa hilo na inamuachia huru chini ya kifungu cha 220 cha sheria namba 7 ya mwaka 2018 sheria ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,” alisema Shamhun”.

TAMWA Zanzibar inaomba mahakama na Serikali kuangalia athari inayowapata waathirika kabla ya kutoa hukumu, kwani kitendo cha baba mzazi kumwingilia mwanawe ni kosa la jinai hasa kwa vile mtoto huyo ni mdogo anayestahiki kulindwa na taifa.

Kwa mujibu wa sheria za nchi ikiwemo sheria namba nne ya 2005 ya kumlinda mtoto mwari na watoto wenye mzazi mmoja na sheria ya adhabu ya namba 7 ya 2018 ni kwamba mtoto chini ya miaka 18 hana ridhaa ya kufanya maamuzi ya kimapenzi bila ya ushawishi na kubakwa, hivyo baba mzazi huyo anastahiki kupewa adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine.

Hivyo hatua ya kumuachia huru Mzazi huyo inapaswa iangaliwe tena upya kwani inaweza kurudisha nyuma juhudi za kupinga ukatili wa kijinsia pamoja na kujenga taifa lenye vijana waliosoma na wenye kujiamini katika kuleta maendeleo ya nchi.

Kuwaachia huru watuhumiwa kama hawa inapelekea ongezeko la matukio ya udhalilishaji hapa Zanzibar kwasababu watuhumiwa hawaogopi na kuendeleza vitendo hivyo vinavyoathiri maisha ya watoto na wanawake kwa jumla.

Aidha TAMWA, ZNZ inapenda pia kuishauri Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wake katika kuandika ripoti za kidaktari ili kuwa nyeti katika masuala ya kijinsia na hivyo kutokuita watoto wadogo wazoefu kwenye mausla ya kujamiiana.

Dkt. Mzuri Issa
Mkurugenzi,
TAMWA, ZNZ
Daaah hii inaitwa kiama....yaani kumzini bintiyo Tena wa miaka 13 alafu mahakama inamuachia huru?? Hapana Hilo haliwezekani
 
Mkuu kwani kama hayupo UNDER AGE haesabiki kama amebakwa.??
....Mkuu, akiwa zaidi ya Miaka 18 angalau Mtuhumiwa anaweza kuepuka Hukumu Kali dhidi akidhibitisha kwamba angalau walifanya kitendo kwa CONSET ya Watu Wazima Wawili. Angalau inaweza kumsaidia.
Hapo pa kucheza na Underage hakuna Mjadala. Ni Hukumu moja kwa moja....
 
Kwahiyo daktari alijua kuwa waliokuwa wakimwingilia siku za nyuma ni watu wengine sio mzazi wake?

Je, kama dogo alishawahi kufumuliwa ni ruhusa kuendelea kumfumua bila kujali umri wake?

Je, kumla binti yako ambaye ni under 13 ruksa?

Hapa albadili imehusika kumtoa nje mbakaji
Hiyo ni sintofahamu
 
Back
Top Bottom