Zanzibar: Aliyembaka binti yake mwenye miaka chini ya 13 aachiwa huru, kwa ushahidi kuwa binti ni mzoefu

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,384
2,000
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI​

TAMWA Zanzibar Hairidhishwi na Hukumu ya Kesi zinazohusu Ukatili wa Watoto.

Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA, ZNZ) haikuridhishwa na hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Wete Mkoa wa kaskazinia Pemba kwa kumuachia huru mtuhumiwa aliyembaka mtoto wake wa kumzaa.

Hivi karibuni TAMWA Zanzibar imepokea taaarifa kwamba mtuhumiwa Salim Khamis Ali maarufu “Panga la Shaba” (43) mkaazi wa Taifu shehia ya Kinyasini aliyembaka mtoto wake wa kumzaa huko Pemba ameachiwa huru kwa madai kuwa taarifa za daktari zimeonesha kwamba mtoto huyo ni mzoefu kwa maana ya kuwa ameshatenda tendo la ngono hapo awali.

Tukio hilo liliripotiwa katika kituo cha polisi Wete tarehe Desemba 6/ 2019 na kufunguliwa jalada namba IR471/2019 ambapo jalada hilo lilieleza kwamba Salim Khamis Ali anatuhumiwa kumbaka mtoto wake wakike aliye chini ya umri wa miaka 13.

Kwa mujibu wa hakimu wa Mahakama ya Wete Mkoa Kaskazini Pemba, Abdalla Yahya Shamhuni, ni kwamba mtuhumwa alitenda kosa Novemba 30, 2019 saa 3:00 usiku katika eneo la Taifu, ambapo bila ya halali mtuhumiwa huyo alimuingilia mtoto huyo huku akijua kuwa ni mtoto wake wa kumzaa, jambo ambalo ni kosa kisheria kwa mjibu wa kifungu cha 143 (1) (4) cha Sheria namba 6 ya mwaka 2018, Sheria ya Zanzibar ambapo kesi hiyo ilipewa nambari RM 4/2020.

Hakimu huyo alibainisha kwamba baada ya kukamilika kwa upelelezi kesi hiyo, Mahakama imemuachia huru mtuhumiwa tarehe Desemba 7/2020 kwa kile kinachodaiwa ushahidi wa daktari ulionyesha kuwa muathirika aliwahi kuingiliwa hapo awali.

“Katika maelezo yake daktari alieleza kuwa muathirika ni mzoefu. Hivyo basi baada ya kupitia vyema ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashitaka mahakama imeona kwamba mtuhumiwa si mkosaji wa kosa hilo na inamuachia huru chini ya kifungu cha 220 cha sheria namba 7 ya mwaka 2018 sheria ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,” alisema Shamhun”.

TAMWA Zanzibar inaomba mahakama na Serikali kuangalia athari inayowapata waathirika kabla ya kutoa hukumu, kwani kitendo cha baba mzazi kumwingilia mwanawe ni kosa la jinai hasa kwa vile mtoto huyo ni mdogo anayestahiki kulindwa na taifa.

Kwa mujibu wa sheria za nchi ikiwemo sheria namba nne ya 2005 ya kumlinda mtoto mwari na watoto wenye mzazi mmoja na sheria ya adhabu ya namba 7 ya 2018 ni kwamba mtoto chini ya miaka 18 hana ridhaa ya kufanya maamuzi ya kimapenzi bila ya ushawishi na kubakwa, hivyo baba mzazi huyo anastahiki kupewa adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine.

Hivyo hatua ya kumuachia huru Mzazi huyo inapaswa iangaliwe tena upya kwani inaweza kurudisha nyuma juhudi za kupinga ukatili wa kijinsia pamoja na kujenga taifa lenye vijana waliosoma na wenye kujiamini katika kuleta maendeleo ya nchi.

Kuwaachia huru watuhumiwa kama hawa inapelekea ongezeko la matukio ya udhalilishaji hapa Zanzibar kwasababu watuhumiwa hawaogopi na kuendeleza vitendo hivyo vinavyoathiri maisha ya watoto na wanawake kwa jumla.

Aidha TAMWA, ZNZ inapenda pia kuishauri Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wake katika kuandika ripoti za kidaktari ili kuwa nyeti katika masuala ya kijinsia na hivyo kutokuita watoto wadogo wazoefu kwenye mausla ya kujamiiana.

Dkt. Mzuri Issa
Mkurugenzi,
TAMWA, ZNZ
 

Sandali Ali

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
3,803
2,000
Kwahiyo daktari alijua kuwa waliokuwa wakimwingilia siku za nyuma ni watu wengine sio mzazi wake?

Je, kama dogo alishawahi kufumuliwa ni ruhusa kuendelea kumfumua bila kujali umri wake?

Je, kumla binti yako ambaye ni under 13 ruksa?

Hapa albadili imehusika kumtoa nje mbakaji
 

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
11,357
2,000
Kwa mujibu wa hakimu wa Mahakama ya Wete Mkoa Kaskazini Pemba, Abdalla Yahya Shamhuni, ni kwamba mtuhumwa alitenda kosa Novemba 30, 2019 saa 3:00 usiku katika eneo la Taifu, ambapo bila ya halali mtuhumiwa huyo alimuingilia mtoto huyo huku akijua kuwa ni mtoto wake wa kumzaa, jambo ambalo ni kosa kisheria kwa mjibu wa kifungu cha 143 (1) (4) cha Sheria namba 6 ya mwaka 2018, Sheria ya Zanzibar ambapo kesi hiyo ilipewa nambari RM 4/2020.
Kwa kuzingatia aya hii, anawezaje kuachiwa huru hata kama ni "mzoefu"
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom