Zambia yaikacha Tanzania mradi wa Bomba la Gesi na Mafuta, yasaini makubaliano ya Ujenzi na Nchi za Angola na Namibia

The Sunk Cost Fallacy 2

JF-Expert Member
Nov 8, 2022
7,382
8,437
Habari zenu wadau.

Miaka 3 iliyopita Zambia ilitiliana saini na Tanzania kujenga Bomba la Pili yaani Tazama 2 ili kusafirisha Mafuta na gas.

Aidha kukokuwa na Makubaliano ya Ujenzi wa Bomba kingine la kusafirisha Mafuta safi ya kula kutoka Bandari ya Dar Hadi Lusaka.

Kutokana na uswahili,ubabaishaji,urasimu na kujivuta vuta kwa Tanzania kwenye kufanya maamuzi ,Wazambia wamelazimika kuitosa Tanzania.

Hivi Sasa wamesaini Makubaliano ya Ujenzi wa mabomba ya kusafirisha Mafuta na gas kutoka Nchi za Angola na Namibia.

Kiukweli Viongozi wa Tanzania hii huwa wanakera Sana kwenye kufanya maamuzi sijui Nchi za kijamaa huwa Zina shida gani.

Tunakoelekea hata Uganda na Kenya zitaghairi kufanya utekelezaji wa ujenzi wa mabomba ya kusafirisha gas Hadi kwenye Nchi zao na kutafuta alternative.

Viongozi wa Tanzania jifunzeni kuwa aggressive kutafuta fursa na kutumia fursa zinapojitokeza..Kwa mwendo huu Ni lini Tanzania itahufaika na kuwepo eneo la kimkakati kwa kupakana na Nchi Nyingi?

Tanzania inatakiwa kufahamu kwamba tuko kwenye ukimwengu wa ushindani na fursa iliyopo Tanzania inapatikana na Nchi nyingine pia.

Juzi tuu hapo Mozambique wamekanza kusafirisha gas Yao Ulaya na Nina hakika watajenga Hadi LNG huku Tanzania tukiendelea na kubishana na kuzozana kuhusu hiyo miradi kusiko na tija.

Just imagine tukianzaga lini kuzungumzia Chuma Cha Liganga na mchuchuma toka nazliwa na Sasa naenda uzewni Hakuna Cha Maana kinafanyika wakati Uganda hapo Wana Chuma na Kuna wawekezaji wanachimba na kutengeneza bidhaa za chuma.

Kiukweli ujamaa ni dhana mbovu Sana aisee yaani unafanya watu wanakuwa mandezi, kubali kataa 👇

Screenshot_20221121-071721.png
Screenshot_20221121-071109.png
 
Tumeacha pesa na nafasi za ajira vimeondoka kwa pamoja, ila sijui kwanini umeiita Tanzania hii ya sasa nchi ya kijamaa..

Ujamaa ulibaki kwenye makaratasi tu, hii ya sasa ni chukua chako mapema, na hata ujenzi wa hilo bomba inawezekana umeshindikana kwa sababu wajanja huko serikalini hawakupewa mgao wao wa 10%
 
Tumeacha pesa na nafasi za ajira vimeondoka kwa pamoja, ila sijui kwanini umeiita Tanzania hii ya sasa nchi ya kijamaa..

Ujamaa ulibaki kwenye makaratasi tu..
Bado mawenge na undezi wa kijamaa upo ndio maana unaona Viongozi hawako aggressive wapo wapo tuu wanajua Maendeleo huletwa kwa miujiza Kama wanavyowekaga makongamano ya kuombeana and such upuuzi.

Hatuna hata economic intelligence kuangalia wenzetu wanafanyaje na sie tufanyaje.
 
Tanzania inaitaji mabadiliko ya mifumo. tunafanya kazi kwa mazoeya sana... acha nihishie apa mwanasheria wangu kasafiri
Uko sahihi Sana mkuu,just imagine tuna nickel na Cobalt Like Kabanga na Mahenge ila imekuwa story za nenda Rudi..

Zambia tayari wame make deal na itakuwa mzalishaji mkubwa zaidi Afrika 👇
 

Attachments

  • Screenshot_20221121-071608.png
    Screenshot_20221121-071608.png
    128.5 KB · Views: 5
Umekuwaje tena? Wakati tukiambiwa mama amejifungua nchi, iliyokuwa imefungwa na awamu ya 5, tumeikosaje fursa hiyo adhim? Na hilo mliangalie.
Mama peke yake haitoweza,ukiangalia juzi alikaa na mabakozi kuwaambia kazi Yao sio kupaki buttocks tuu huko Bali kuifungua Nchi..

Yaani mabakozi wa China,Korea na Kenya ndio wanajitahidi kutafuta fursa Tanzania wengine Ni mizigo hawaelewi hata Cha kufanya.
 
Uko sahihi Sana mkuu,just imagine tuna nickel na Cobalt Like Kabanga na Mahenge ila imekuwa story za nenda Rudi..

Zambia tayari wame make deal na itakuwa mzalishaji mkubwa zaidi Afrika
Mkuu tuna resource nyingi sana ambazo kimsingi aziendani na kasi na maendeleo tuliyonayo. kwa africa ni nchi chache sana zenye uthubutu mfano botswana
 
Mkuu tunapaswa kuwaunga mkono wote wanaohtaji katiba mpya ili hayo mabadiliko ya mifumo yapatikane
kweli mkuu katiba ndio suluhisho la kudumu kwani litatoa dira na mwongozo wa rasilimali tulizo nazo na namna tunavyoweza kunufaika kwa pande zope mwekezaji serikali pamoja na wananchi wake kwani kutakuwa na uwazi wa mikataba..
 
Mkuu tuna resource nyingi sana ambazo kimsingi aziendani na kasi na maendeleo tuliyonayo. kwa africa ni nchi chache sana zenye uthubutu mfano botswana
Ndo hizo resources sasa wanabwagiwa wachina,waarabu etc bila mpangilio
 
Back
Top Bottom