ZAMBIA: Upinzani kumshtaki Rais Edgar Lungu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Chama kikuu cha upinzani Zambia kimewasilisha hoja ya kumfungulia mashtaka Rais wa nchi hiyo Edgar Lungu, kikimtuhumu kukiuka katiba ya nchi hiyo. Hayo yameelezwa na Ofisi ya Rais katika mji mkuu Lusaka.



Hoja hiyo ya chama cha United Party for National Development, UPND, ilisainiwa na theluthi moja ya wabunge wote katika bunge la Zambia lililo na viti 166, lakini itahitaji kuungwa mkono na theluthi mbili ya wabunge ili kupitishwa.

Msemaji wa Rais amesema hoja hiyo ni muendelezo wa kile alichokiita 'njama zilizoshindwa za chama cha UPND', kumuondoa madarakani rais Edgar Lungu, ambazo amesema hazitafika popote. Hoja ya chama cha UPND inasema Rais Edgar Lungu alikiuka katiba ya nchi, pale alipokaidi kuyakabidhi madaraka kwa Spika wa Bunge, baada ya upinzani kuanzisha kesi kortini kupinga ushindi wake.


CHANZO: DW
 
Back
Top Bottom