Zamani vs kisasa

chaUkucha

JF-Expert Member
May 28, 2012
3,382
1,212
e93c311570a2b8de683e39e927407cd5.jpg

1. Zamani mtu akiokota makopo eti kawehuka but siku hizi ni dili.

2. Zamani mtu akivaa nguo iliyochanika eti fukara au kichaa but Siku hizi kununua nguo iliyokwisha chanika eti fasheni.

3. Zamani suruali zilivaliwa kwenye vitovu (mayenu) but siku hizi zinavaliwa chini ya makalio na boxa chafu kama tambara la kudekia choo cha walevi.

4. Zamani ilikuwa mtu akijifungua kwa operesheni ilikuwa ni bahati mbaya sana but siku hizi watu wanaomba wajifungue kwa operesheni sijui wanalinda nini mie
sijui.

5. Zamani kwenye maigizo sehemu ya mwanamke aliigiza mwanamke but siku hizi sehemu ya mwanamke anaigiza mwanaume sasa sijui wanatangaza nini hapa.

6. Zamani ..........but..........endeleza
 
Zamani raha,unakunywa vidonge tuwili tutatu gono kwishaaa,mhh lakini leo ukiikanyaga unakunywa vidonge maisha yako yote na kifo juu..
Siku hizi dawa nyingi wanatengeneza kibiashara hawataki watu wapone kabisa magonjwa kwa sababu wakipona kabisa na magonjwa kuisha viwanda vya madawa vitakufa
 
Zamani wanaume walikuwa wanaoa wanawake, siku hizi wanaume wanaoa wanaume wenzao na wanawake wanaolewa na wanawake wenzao
 
Zamani wanaume walikuwa wanaoa wanawake, siku hizi wanaume wanaoa wanaume wenzao na wanawake wanaolewa na wanawake wenzao
Kuna wanaume wanaolewa na wanawake pia, sasa kijana wa miaka 24 kuishi na mwanamke wa miaka 50 jamani si laana hiyo.
 
Zamani ukiwa na mtoto wa kike ilikuwa ni Changamoto kubwa kimalezi hasa anapofikia 15 hadi 20

Lakini leo ukiwa na mtoto wa kiume ni changamoto kubwa ya kimalezi hasa unapomuona ameanza kupiga piga picha kabinua midomo, mara kabinua makalio na kutupia Mtandaoni.

Tayali unaanza kuwa na wasiwasi mwanangu si riziki.
 
1. Zamani wachezaji mpira walikuwepo ila mpira ulikua haulipi siku hizi mpira unalipa wachezaji hakuna

2. Zamani shule zilikua chache wasomaji wengi siku hizi shule nyingi wasomaji wachache
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom