Zamani ilikuwa raha

pia kulikuwa na biashara ya yomboo
 
kulikua na maneno maarufu kama
kristobe
damdam
mzeemeko
doletupu
komredi
makaburu
 
Watu wa zamani mlipata shida sana. Sijui hata mlikuwa mnatongozaje wakati kulikuwa hakuna simu... Inawezekana pia mlikuwa mnachapiana sana.. Na ndio pengine mkafikia hatua ya kutunga ule msemo kuwa "kuchapiwa ni siri ya ndani"

Wakati ule mkifunga shule unaambiwa likizo kwa bibi, mjomba babu, au baba mkubwa na ilisaidia sana kuweka familia pamoja....hakukuwa na hizi mobile phones hivyo kama ni nyumba au kijiji jirani mtoto unatumwa au kama ni jambo zito inabidi mfunge safari. Watu/familia zilikuwa karibu sana kwani zilikuwa zinaonana uso kwa uso, tofauti na sasa tunapigiana simu na mtu anakuambia yupo salama kumbe ana hali mbaya.....mobile phones zimerahisisha sana mawasiliano na mambo mengine ila imetupunguzia sana kukutana hasa kwa ndugu na majirani. tunakutana kwenye misiba na harusi tu.....vinginevyo ni mwendo wa mobile phones.....nafikiri kutembeleana kulidumisha upendo na mshikamano zaidi...ila sasa hivi tuna excuse za kutosha...tuko busy, foleni za magari, kwenda kwa mtu lazima uweke appointment, budget ya kutembeana haitoshi,n.k!
 
Kipindi Edward Moringe(R I P amen) akiwa Waziri mkuu alipofanya opereshen kwa wahujumu uchumi watu walitupa pesa zao sio leo EPA mnawabembeleza warudishe na Escrow kubeba kwa sandarusi!
Waliohujumu kwa kufungia sukari stoo ili wapandishe bei waliimwaga sukari mtoni.
 
Thats true !! nilikuwa nimedunduliza na kuchanga pesa mwaka mzima zikafika $ 57 !! duuh wakati wa Opereshen hujumu uchumi eti wanyumbani wakanilazimisha nizichome moto !!iliniuma sana !! maana nilijinyima mda mrefu hatimae nikageuza pesa masizi na majivu !!
 
Reactions: BAK
Zamani tulikuwa tuna hudhuria ma beach party kila wiki ilikuwa buruudaniii sana
 
siku za sikukuu kulikuwa na tamaduni za kupeana chakula hasa pilau, kama mimi ni mkristo na ni krismass lazima pilau ipikwe na niwagawie jirani zangu hasa ambao sio wakristo, na wao vileviile ikifika sikukuu yao wanafanya hivyo hivyo....

Hii hadi kristmass ya mwaka jana nimefanya, na pasaka hii ntafanya. Huwa nanunua kuku nampa anachinja, analeta anapikwa twala, na yeye sikukuu zake hivyo hivyo, so atleast mimi nipo zamani kwa hili..!
 

Kwani hili shairi wamelitoa kwenye mtaala wa sasa?! Maana mimi nilikuwa nalichukulia kama kipimo cha mtu aliyepatia elimu ya msingi Tz.
 
Kwenye sikukuu ya saba saba umesema kweli mkuu, ilikuwa ni sherehe kubwa mkienda huko uwanjani mnakula miwa balaa. Kwenye magari nilikuta STC ndio zinaishilia, ilikuwa tukiona gari yenye TX basi tunajua ni gari ya mzungu
 

Asante sana mkuu nimeipenda kwelikwel!
 
-Kuangalia sinema kwenye projector kuuubwa kijijini mida ya jioni hasa zile sinema ya Chack Norris na Rambo na kiingilio ilikuwa shilingi tano hadi kumi

-Wakati Pepe Kalle anatumbuiza pale Diamond Jubilee, kulikuwa hakuna utamaduni wa kukaa kwenye siti kama sasa hivi maana afya zetu hizo zilikuwa safi siyo sasa miili imejaa chips mayai
 

Kokolikoo, Maxi priest, Athumani Digadiga, (na huyu wa juzi Super Faby na Queen Vero)
 
Ahante sana, miaka hiyoooo 80's.......
Kweli ilikuwa raha sana, hata vitabu tulivyokuwa tunasoma vya akina asha na rozi vilikuwa vizuri sana, yuo can't compare kwakweli...... "rafiki ni bora kuliko mwanasesere"

Somo la jiografia lilikuwa poa sana, by that time darasa la nne tu unaijua mikoa yote ya Tanzania, mkoa gani unalima mazao gani n.k sasa hivi sidhani kama watoto wanafundishwa hivi vitu.

Manjagata unakikukmbuka kitabu cha jiandae kumaliza elimu ya msingi, zile atlasi, ndani unakutana na Tanzania- sura ya nchi, yaakisha mambo ya tanzania, inafuata afrika mashariki, then afrika na mwisho dunia, mwanafunzi unaelewa kwa undani tanzania kuna nini, afrika mashariki kuna nini, afrika kuna vitu gani hadi dunia


 
Last edited by a moderator:
Zamani sema kulikuwa hakuna ngoma tuu ndio uzuri wake,,ukiugua zako kaswende unapiga mitishamba kesho unadunda kitaa na raizoni.
 
Umeona eeh....

siku hizi sijui watu wanafuturia wapi, nakumbuka tulikuwa tumepanga nyumba ya waislam, tulikuwa tunafuturu mwanzo mwisho utadhani na sisi tumefunga, siku za sikukuu iddi au christmas ilikuwa hakuna ubaguzi mnashirikiana kupika na kula pamoja kama ndugu jamani, haya mamba hayapo tena nowdays, kweli zamani ilikuwa raha


Zamani kweli raha,

Kipindi ikifika Ramadhani watu wanafutari nje na kila mpita njia anaweza kukaa na akala na majirani wote munakua pamoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…