Zamani ilikuwa raha

Mengine kupimwa mimba! Nesi maalum analetwa kutuminya matumbo.... Hivi siku wanapimwa kweli? Elimu ya kujitegemea, sayansi kimu... Unamaliza std 7 unajua kushona, kufuma, kupika. Kufinyanga vyungu, kusuka mikekana bado unafaulu vizuri darasani bila tuition wala kununua mitihani. Kipindi cha uhujumu uchumi kina mama wakafukia pair za vitenge vya Congo na mawigi.... Tv ya inchi 14 ikaokotwa imetupwa Morocco ivi vilikuwa vikasoro vidogo lakini maisha yalikuwa poa na wazazi walimudu kuzaa watoto 10+ jaribu leo uone....
 
Enzi hizo ilikuwa raha sana,pedi hazikuwepo na mdada anaenda mawinguni anachafuka wanafunzi wanamcheka badala ya kumsaidia
 
Kulikuwa na kitengo maalumu cha magari kikijulikana kama Ufundi - KUMM yaani ufundi wa Kuendeleza Magari Mabovu ambapo magari yote ya serikali yaliyochoka kabisa yalikuwa yanapelekwa ili kuangalia namna ya kuyafufua
 
watu wa zamani ni mahir kutongoza live kuliko kizazi hiki cha kiduku mkuu

Kutongozana ni barua iliyokuwa inaandikwa: Maria mpenzi salamu sana je hujambo, kama hujambo ndiyo furaha yangu kubwa. nikuonapo moyo wangu hushtuka, sili silali kwa ajili yako, kila siku nakuota wewe. naomba uwe mke wangu. ukinijibu nitafurahi sana. barua hii ukimaliz kusoma ichane wazazi wasiione. Akupendaye kwa moyo wote, Yohana.
 
Suruali za jeans hazikuwepo kulikuwa na suruali za codrai na surual za mabuga luuu, ndo zilikuwa fashion.

Unazikumbuka suruali ziliandikwa ZICO na Michael Jackson? Zilipendeza ukivalia na kiatu kama mokasini au raba mtoni.
 

Dada kipenzi cha moyo wangu salaam,

Mimi ni bukheri Wa afya hofu na mashaka juu yako uliye mbali ya upeo Wa macho yangu! Nilalapo nakuota Wewe, nibywapo maji nakuona ndani ya kikombe cha maji! Ila tulikuwa waongo! Tulikuwa tinashindana kuwaangusha akina FaizaFoxy, Madame B, Evelyn Salt, Preta.'Mwisho Wa siku mnafanya sensa nani kaangusha mbu.ny za uhakika! Pia tulikuwa hatujui kuwapiga wapenzi wetu. Matoto ya siku hizi eti yanawapiga utafikri yamewatolea mahali mengine mpaka yanawachinja!!
 
5+n=7
n ni? Hesabu za buibui darasa la pili zilikuwa ngumu sana.
 
Kulikuwa na jarida moja inaitwa sani. Lilikuwa linazunguka kijiji kizima kundi la vijana zaidi ya kumi wanalisoma kwa wakati moja. Akina Bob mazishi kipepe mzee meko walikuwa burudani
 
kulikuwa na upendo wa hali ya juu kati ya mwalimu,mwanafunzi na mzazi.
mwalimu akikuagiza matunda, mayai,mbogamboga unamletea
 
Yeah nawakumbuka
Minnie the jinx, Rodger the Dodger, Dennis the Menace hahaaa na kulikuwa na vi comic novel vya Bounty nimesahau jina..... Good old days
Mkuu unakumbuka kitabu adventurers of tintin kitabu hicho walikuwa nacho watoto wa kishua a tu
 
 
bora ningekuwa wa zamani tu skuizi vurugu mechi mtindo mmoja!
 
Reactions: ram
Nakumbuka kulikuwa na bendi nyingi za dansi, kulikuwa na Tabora jazz, DDC Mlimani park, tancut almas, yaani bendi zilikuwa nyingi nyingi sana zenye ladha ya kimuziki wa Kitanzania haswa, na wengi wetu tulikuwa tunacheza kwenye vumbi ukumbini hahahahaha

Wanamuziki walikuwa wanavaa mavazi fulani kung'aa ng'aa na mapozi fulani niliyapenda sana
 
...zamani bana,mtu kwao wakipika pilau au wali marage basi mtaani hata akikuchokoza utakiwi kumfanya chochote,ukimtania anafuta urafiki anakwambia na usije kwetu[kumbe kwa ajili ya wali ndondo]
...zamani bana kuoga mpaka ushikiwe fimbo au uwambiwe unaenda town.
....zamani raha kweli sikuku kama iddi,xmas,mwaka mpya,pasaka lazima ununuliwe nguo na lazima lipikwe pilau la kuku au la bata,na soda kreti na picha mtapigwa.
..zamani bana ilikuwa ikifika jumatatu kwenda shule full kusingizia kuumwa,kumbe unajua kuna kusoma table 1 mpaka 12 hahah
 
Mkuu Nyerere alikuwa anaheshimiwa na kuogopewa sana. Ilikuwa sio rahisi kusema baya lolote dhidi yake hadharani. Iliaminiwa kwamba ukimsema vibaya anakusikia. La msingi alisimamia maadili ya viongozi na nchi kwa ujumla. Sasa hivi hovyo tu. Ukivaa miwani myeusi wewe ni usalama wa taifa
 

Hhaahhhaa...Kibanga ampiga mkoloni
Mfalme ana masikio marefu kama ya punda
Tola anakula Gizani
Gulioni Katerero
Du...Rosa Mistika
 
Hahahaaa...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…