Zamani ilikuwa raha


Mkuu umenitia simanzi sana, juzi kati nimempeleka mtoto hospitali ana UTI nikapewa paracetamol 5..dah hali tete sana mungu atusaidie.
 
Kwenye atlas umenikumbusha kitambo kweli kuna mchezo wa kutafuta miji tulikuwa tunacheza 'mtu anataja mji/sehemu wengine mnatafuta.'

Nitafutieee....... Unamwambia kamji kadogo kabisa kako pembeni mwa ramani, atasota huyo.....was very wonderful days
 
waliofeli ndio walienda private schools, ilikuwa aibu mtu kusoma pte school. leo ni sifa kusoma au kusomesha pte schools.

au wana-repeat. na ndo maana "Wanafunzi shule ya msingi baadhi walikuwa wananyoa ndevu."

 
siku za sikukuu kulikuwa na tamaduni za kupeana chakula hasa pilau, kama mimi ni mkristo na ni krismass lazima pilau ipikwe na niwagawie jirani zangu hasa ambao sio wakristo, na wao vileviile ikifika sikukuu yao wanafanya hivyo hivyo....

jirani yetu mama Abdallah siku za eid sinia la mahamri lilikuwa linaletwa tena kwa upendo mwe!
 
Hahahahahaha lol! Siku kuna wali na maharage hata hutaki kucheza mbali na nyumbani 🙂🙂

Siku hizi ndo hamna raha wakati huo kila kitu kilikuwa kinasisimua kwani havikuwa vinapatikana kila mahali kama leo. Wali wa maharage ulikuwa mtamu kuliko chipis mayai/kuku leo, hata uji usio na chochote ulikuwa mtamu kuliko uji wa asali leo
 

Yaani unawajua marais wa nchi Zote, miji mikuu ya nchi zote, na kila nchi inalima zao gani la biashara
 
Walimu walikuwa wanathaminiwa na Serikali haya mambo ya kusikia walimu hawajalipwa mabilioni ya pesa zao halali hayakuwepo kabisa, siku hizi unasikia wanaidai Serikali bilioni 16 halafu Serikali inataka kuwadhulumu mchana kweupe kwa kudai haidaiwi na walimu!!! Ngoja waje mafisadi wa Richmond waseme wanaidai Serikali $110 million, serikali hii dhalimu itaunga mkono kwamba ni kweli inadaiwa. Ngoja waje wakwapuzi wakwapue bilionu 200 za walipa kodi pale BoT Serikali hii dhalimu itakuwa mstari wa mbele kudai zile si pesa za umma.

Yaani unawajua marais wa nchi Zote, miji mikuu ya nchi zote, na kila nchi inalima zao gani la biashara
 

siku hizi watu wanafuturia Hyatt, dining kwao, na hii ya kufuturisha zamani siikumbuki
 
gazeti la Sani lilikuwa likitoka anakuwa nalo mtu mmoja tu shule nzima, but mtapokezana by the time linakufikia kuna pages zishaota ukungu, zingine zomelowa maembe, mate, kamasi etc
 

Kabisa mkuu.. Yaani leo form iv hata nchi za Africa hajui walau mini mikuu na viongozi kumi hawezi kitaja kabisa....
 
Dah! Chezeya Moringe Sokoine weye!!!! Niliwahi kuambiwa miaka hiyo pamoja na nchi yetu kuwa maskini dhahabu ilikuwa haijaanza kuvunwa, gesi haijagunduliwa lakini shilingi yetu ilikuwa na nguvu sana duniani $1 ilikuwa sawa na shilingi 5 na pound moja ya kwa mama (UK) ilikuwa sawa na shilingi 20 yetu sasa hivi ni midabwada mitupu shilingi yetu imeshuka utadhani ni dollar ya Zimbabwe.

 
kutoka dodoma kwenda mwanza usafiri ulikuwa ni wa train tu, na inabidi u-book ticket mwaka mzima
 
Duuh nimecheka sana na pia nimekumbuka mambo mengi sana
 
Kabisa mkuu.. Yaani leo form iv hata nchi za Africa hajui walau mini mikuu na viongozi kumi hawezi kitaja kabisa....

Siyo form IV tu, Mkuu hebu mkamate yeyote aliyeko chuo kikuu mweke kati akutajie nchi 20 na marais wake kama ataweza!! Hii ni aibu kwa nchi yetu!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…