Zakazakazi: Yanga sio Mabingwa mara 29 na Simba sio Mabingwa mara 22

Anaandika Zakazakazi,

YANGA SIYO MABINGWA MARA 29 NA SIMBA SIYO MABINGWA MARA 22

Hii ni changamoto kwa wadau wote wa soka nchini Tanzania; wachambuzi, waandishi wa habari, mamlaka za soka na serikali kwa maana ya wizara ya michezo na baraza la michezo.

Fanyeni utafiti na mje na majibu sahihi maana siku zinavyozidi kwenda, uongo unakuwa ukweli kwa sababu watu wanaamini yasiyo sahihi.

Ligi ya Tanzania ilianza mwaka 1965 ikiitwa Klabu Bingwa ya Taifa. Hadi mwaka huu, 2023, ni miaka 58. Maana yake kuna mabingwa 58 wanatakiwa kuwepo.

Sasa kama Yanga ni mabingwa mara 29, Simba mara 22 maana yake hawa wawili peke yao wamechukua ubingwa mara 51.

Katika misimu 58, imebaki misimu 7 pekee ambayo wamechukua wengine.

Hao wengine ni wafuatao.

Cosmopolitan -1 (1967)
Mseto -1 (1975)
Pan African - 1 (1982)
KMKM - 1 (1984)
Majimaji - 3 (1985, 1986 na 1998)
African Sports - 1 (1988)
Malindi - 2 (1989 na 1992)
Pamba - 1 (1990)
TZ Prisons - 1 (1999)
Azam FC - 1 (2014)

Jumla 13

Ukijumlisha na zile 51 za Yanga na Simba, unapata 64...inawezekanaje?

Ligi iliyochezwa miaka 58 inakuwaje na mabingwa 64...hesabu za wapi hizo?

Timu zilizotajwa hapo ndiyo mabingwa wa Tanzania wanaotambuliwa na CAF na FIFA, na ndiyo walioshiriki Klabu Bingwa/Ligi ya Mabingwa Afrika katika miaka husika.

Ndiyo maana nilianza kwa kutoa changamoto kwa wadau.

Tembeleeni tovuti za CAF na FIFA muone ni timu zipi ziliiwakilisha Tanzania kwenye Klabu Bingwa/Ligi ya Mabingwa Afrika kuanzia 1965.

UKWELI
Yanga ni mabingwa mara 22 na Simba mara 21.

22+21= 43 - Yanga na Simba
43+13=56 - Jumla (kati ya 58)

NB: Kuna misimu miwili (1970 na 2003) Tanzania hakukuwa na bingwa.

Ndiyo maana unapata mabingwa 56 katika misimu 58.

Itaendelea...

Soma sehemu ya pili hapa

Soma sehemu ya tatu hapa

Soma sehemu ya nne hapa

Soma sehemu ya tano hapa

Soma sehemu ya sita hapa

Soma sehemu ya saba hapa

Soma sehemu ya nane hapa

Soma sehemu ya tisa hapa
Mimi nimemsikia huyo zaka,nataka kumwambia yeye ahesabu atakavyo haitusumbui,al mradi sisi ni mabingwa mara 30,amesema pia kuwa eti huo ushindi wetu ni sawa na kufaulu mtihani wa mocco,namjibu mtihani wa mocco huwa hauna cheti,lakini ushindi tulioupata sisi una makombe 30,yapo makao makuu ya yanga,hatuhedabu ubingwa kwa kuandikwa kwenye tovuti ya fifa au caf,tunahesabu ubingwa pale tunaponyanyua kwapa na kubeba kombe
 
Inaonekana mwaka 1993 Simba anapofika fainali ya CAF, kulikuwa na mashindano mengine ya Abiora.

Ulikuwa ni mwaka ambao una mashindano mengi sana

Asante kwa kunijuza ndio naskia kwako.
Bingwa wa kombe la washindi mwaka alikuwa
Nimeshuhudia utetezi wa nguvu sana kwenye huu mjadala.

Wengine wameonesha kukubali ligi mbili kuunganishwa na kutaka washindi wa ligi zile za mwanzo kabla hazijaunganishwa waendelee kuhesabiwa ushindi wao

Wakati Simba ilipocheza CAF Cup walisema ambayo saizi ni Caf confederation, walisema ile aliyocheza Simba ni Abiora kwakua CAF Confederation Cup imeanza 2004.

Ngoja tuendelee kumsikilizia aje na Makala nyingine huwenda hayo unayoyasema akayaweka
Ebu pitia hiyo link hapo chini.

 
Muulizeni Zaka Za Kazi.

Kama Ligi Kuu ilianzishwa mwaka 1965,

Je Yanga SC (iliyo anzishwa mwaka 1935) na
Simba SC (iliyo anzishwa mwaka 1936)..zilikuwa zina fanyanini wakati wote huo wa miaka 30?


Jibu langu:-

Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania lilikuwa affiliated na CAF kuanzia mwaka 1965.

Ndipo hapo Shirikisho la soka Tanzania likaanza kujitambua kama siku yake ya kuzali.

Lakini lilikuwa likifanya kazi tangu hapo awali basi nankutotambulika kihalali kama mashirika ya soka mengine ya ulimwengu.
Naunga mkono hoja
 
Back
Top Bottom