ZAIN Tanzania: Network ina matatizo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ZAIN Tanzania: Network ina matatizo?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sajenti, Feb 2, 2010.

 1. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #1
  Feb 2, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Wandugu kwa muda wa siku takribani 3 sasa mawasiliano katika mtandao wa Zain ni tabu tupu ukipiga simu mtu anapokea chini ya dakika moja simu inakatika katika mazingira ya kutatanisha au net work hakuna.

  Mwanzo nilidhani ni simu yangu tu huenda iko na shida , lakini nikagundua hata jamaa zangu wanne hapa ofisini kwangu they are facing same problem.

  Kwa kweli mtandao wenu haujatulia kabisa, hebu rekebisheni mnatukera sana wakati mwingine mtu unapiga simu muhimu kabisa mtandao unakuzeveza...
   
 2. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  itakuwa ni hapo ofcn kwenu ndio kuna shida.....mbona sehemu zingine tunapeta
   
 3. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #3
  Feb 3, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu

  Kwa wale watumiaji wa Zain haswa kwenye upigaji wa simu , watakuwa wameona tofauti Fulani kwa siku za karibuni sijui tatizo ni nini kwa sababu hata sijapewa ujumbe wowote kwenye simu yangu ya mkono kwa njia ya sms wala kwenye anuani yangu ya barua pepe .

  Kwanza ni unapopiga simu inachukuwa muda kidogo zaidi ya sekunde kadhaa kabla ya kuunganishwa na yule unayetaka kuwasiliana nae kwa wakati huo , muda huo ukisikiliza ni matangazo Fulani Fulani hivi , kabla ya kushituka mara nyingi nimekuwa nakata simu kufikiri labda
  simu haziendi huko ninapopiga .

  Pili ni suala la kupiga simu halafu simu hiyo kuunganishwa na mtu ambaye hujampigia hili suala limenisumbua sana kwa kipindi cha wiki 1 iliyopita haswa ninapopigia simu mteja wa VODACOM ,lakini nimeona tofauti Fulani mfano huyu ambaye ninempigia nimemuunganisha kwenye
  Huduma ya PAMOJA , ambao sijawaunganisha kwenye huduma hii naweza kuwasiliana nao vizuri sema tatizo ndio hilo kuchelewa kuunganishwa .

  Tatu ni kukatika kwa mawasiliano ya Mtandao mara kwa mara , Baadhi ya maeneo ya Jiji la dare s salaam , mtandao wakati mwingine haupatikani kabisa na ukiwa sehemu za Chuo kikuu cha Dar pia kuna shida hiyo .

  Naomba wahusika wa zain wachukulie swala hili kwa umakini sana haswa hilo la pili ambapo mtu anaunganishwa na mwingine bila ya yeye kutaka imeleta shida sana kwa baadhi ya watu ikiwemo mimi .

  Mwisho ni kuomba kampuni hii iwe inatoa taarifa kwa wateja wake kama kuna shida yoyote na mtandao wao kwa sababu wengine kama mimi nimeshasajili namba yako ya simu nikaweka taarifa zangu zote za muhimu sioni sababu ya kwanini nisipewe taarifa kama mtandao una shida hiyo
  ni haki yangu ya msingi kabisa kama mteja
   
 4. s

  sumar Member

  #4
  Feb 7, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hizi kampuni zote za simu ni wababaishaji na Zain wamezidi. Jamani toeni huduma safi ya mawasiliano. Hizi promotion zenu za ajabu ajabu angalau basi tuambieni kama ni biashara nyengine kabisa. Biashara ya bahati nasibu. Pata potea. Tena wala si bure.

  Zamani nikipata air time za bure kila baada ya muda kutoka zain. Ghafla zimepotea. Kama mwezi uliyopita nilipokea simu kutoka zain nikifahamishwa kwamba nimeshinda silver card. Nikaombwa nu. ya sanduku langu la posta.

  Nikawapa na mpaka leo hamna kitu. Sijui mjanja keshaichota. Haya yalimtokea na mwenzangu. Alishinda gold card, na mpaka leo ana cheki posta bila ya mafanikio.Piga maulizo nu 100. BUREE! Adha tupu.

  Zain acheni ubabaishaji. Toeni huduma ya simu. Khalas. Bahati nasibu ifanyeni vingine.

  0784 759 758
   
 5. N

  Ngala Senior Member

  #5
  Feb 7, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Zain hakuna matata ukinisoma hapa natumia kilonga longa chenye zain siiijui kompyuta wala nini. Nikifungua tu JF inakuwa hewani japo juzi kati JF ilidoda kwa muda.

  Take my word Zain ni Nambari wani chama cha kijani kinafaatia w/end njema na enjoy Zain mtandao bora zaidi
   
 6. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #6
  Feb 7, 2010
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Wewe utakuwa afisa masoko wa tigo, zantel, vodacom au sasatel

  Mbona zain inapatikana vizuri sana bana
   
Loading...