Zain africa challenge 2010 na vyuo vyetu TZ. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zain africa challenge 2010 na vyuo vyetu TZ.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kigogo, Mar 7, 2010.

 1. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,534
  Likes Received: 1,542
  Trophy Points: 280
  Dahh nimekaa natazama kipindi cha Zain Africa challenge kati ya University of Ghana na University of Arusha,kwa kweli ni aibu vijana wetu hawana uelewa wa mambo kabisa yaani wanabaki kubun buni tu majibu...I felt very bad and disturbed
   
 2. Katoma

  Katoma Senior Member

  #2
  Mar 7, 2010
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  laugh out loud.
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Mar 7, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,534
  Likes Received: 1,542
  Trophy Points: 280
  yaani kuna kijana alikuwa ananichekesha maana yeye jibu lake analolijua no PASS kwa kila swali..dahhh
   
 4. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Shida ya wanafunzi wa kiTanzania ni kuwa hawana "general knowledge".

  Ukimwuliza mambo ya darasani anaweza akajaribu kidogo, tena isiwe kwa kuzungumza, labda aandike!!

  Mfumo mzima wa elimu unahitaji kuangaliwa upya. Watoto hawapewi elimu kuhusu mambo ya nje ya darasa. Halafu na hii tabia sijui ni waziri yupi wa elimu aliingiza kuondoa tamthilia (literature) zisizokuwa za kiTanzania/ Afrika wakati dunia nzima inasoma Shakespeare mTanzania si ajabu anasikia jina "Shakespeare" kwa mara ya kwanza kwenye filamu!! Au Sherlock Holmes.

  Najua kuna watakao sema ni ukoloni mambo leo, lakini sikubaliani na dhana hiyo, kujua kuhusu mila/ tamthilia za utamaduni tofauti na wa kwako kuna saidia sana kufungua macho na kupanua mawazo.

  Bila mabadiliko vyuo vya Tanzania kwenye mashindano kama hayo unayozungumzia vitaendelea kuwa wasindikizaji tu
   
 5. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2010
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,734
  Likes Received: 336
  Trophy Points: 180
  Siyo kila taasisi hapa Tanzania inayojiita Chuo Kikuu ni Chuo Kikuu kweli. Baadhi kusema ukweli ni dignified high schools. Reading culture imepotea kabisa miongoni mwa wanafunzi. Hata magazeti hawasomi achilia mbali tamthilia na maandiko mengine yanayoelimisha. Sasa hiyo general knowledge wataipata wapi? They are a mirror reflection of what we have created.
   
 6. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #6
  Mar 8, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Tatizoo la uelewaa wa wanafunzi wa Tanzania hasa elimu ya juu inachangiwa zaidi na mitaala na wafundishajii husika..

  Nimeshuhudiaa mara nyingi wafundishaji wakikosa mifano halisia ya hapa nchini kuendana na somo achilia mbalii ufundishajii wa kukaririi..

  Inaaumaa sana wanafunzi wengi wa elimu ya juu nchini kuwa na upeo mdogo wa general issues kutokana na mfumo wa elimu ana wafundishajii ambaoo wanaegemeaa kukaririsha notes zao kwa wanafunzi huku wakitumia muda mdogoo kujiandaa katika ufundishajiii..

  Mawazo mgando ya viongozi wa elimu ya juu nchini na walimu husika pamoja na kutokufikri nje ya box katika kutoa elimu ni sehemu tuu ya changamoto kubwa katika elimu yetu ya juu nchinii.
   
 7. JS

  JS JF-Expert Member

  #7
  Mar 8, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,067
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  I did watch that programme jana kwa kweli it was embarrasing. Mfumo wa kufundishia ni mbovu hapa nchini kwetu na wanafunzi wenyewe hawajitumi wanasubiria vya darasani tu. it really hurts and pains so much
   
 8. B

  Bao3 JF-Expert Member

  #8
  Mar 8, 2010
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 318
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Zamani wakati tupo secondary tulikua na debating clubs. Wanaojitia wanajua kuharibu mitaala ya elimu wakafanya wanavyojua wao ikawa hakuna cha debate wala nini kwenye sec.schools. Sasa ukimwona huyo form six aliejoin chuo utajisikia huruma sana jinsi anavyoanza kusimama na kutoa hoja. Sijui tutaanzia wapi kurudisha tena uwezo wa wanafunzi wetu hapa bongo.
   
 9. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,935
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Hata hao UDSM,MHUMBILI,MZUMBE nk nao walikuwa na utumbo huohuo.Kwa hiyo hili ni tatizo la vyuo vyote.hakuna cha mwenye afadhali.
   
 10. B

  Bao3 JF-Expert Member

  #10
  Mar 8, 2010
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 318
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ndio maana nikasema tatizo ni foundation za wanafunzi. Huko walikotoka hawajapikwa vya kutosha. Kuna post humu kwamba professor wa Biology pale UDSM wanafundisha wanafunzi wao kiingereza,ujue hali ni mbaya mno!
   
 11. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #11
  Mar 8, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 970
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 45
  Mkumbuke kabla ya mashindano wanaandaliwa na kupewa maswali kibao,na hawa wanafunzi wanachaguliwa na chuo husika naamini ni wale ambao wako juu, tujiulize kwanini vyuo vyetu vinatia aibu hivyo? Mtakubaliana na mie ukiangalia wanafunzi wa vyuo vya kenya, Uganda, malawi na West Africa utagundua wanafunzi wetu hakuna kitu kabisa, kwa watawala wanaona hilo sio tatizo hata kidogo
   
 12. B

  Babu Ubwete Senior Member

  #12
  Mar 8, 2010
  Joined: Jan 26, 2008
  Messages: 169
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii programu nakumbuka bunge la mwaka jana Mchungaji Rwakatare(MB) aliwahi kuuliza swali bungeni juu ya upeo wa elimu ya vijana wa kitanzania lakini Naibu waziri aliiponda hii zain Africa challenge kama sio kitu cha kujua vijana wa vyuo vyetu hakuna kitu. Ni kwa nini miaka inavyozidi kwenda product ya graduates inakuwa ya kichovu?
   
 13. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #13
  Mar 8, 2010
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 19,299
  Likes Received: 9,767
  Trophy Points: 280
  Wanifanya nilie kabisa mkuu..
  Yaani nikikumbuka enzi hizo za debate clubs..sasa hivi nawauliza wadogo zangu wananiambia hakunaga kitu kama hicho!Inaudhi lakini...how do we even have members of parliament who can not present proposals and expect maendeleo??!
  Nalia...pole!
   
 14. B

  Bao3 JF-Expert Member

  #14
  Mar 8, 2010
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 318
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  We acha tu, enzi hizo ilikua mtu unadebate,unapingana na mtu kwa hoja,baada ya debate mpo marafiki na mnaenda mpirani bila shari wala kununiana. Ilikua inatufundisha mengi sana kupitia such things. Lakini siku hizi hao wanaoenda kututungia sheria wakitofautiana kwa hoja basi ni visasi mtupu!
   
 15. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #15
  Mar 8, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,935
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Kwa aibu tunayopata.ni bora kutoshiriki hayo mashindano.
  Yani ni maumivu..............
   
 16. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #16
  Mar 8, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,484
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mnapeleka vibogoyo wasioeza kutafuna, wao kumeza tu na wengine ni vijoni visomo ambao ni myopic hawana upeo mpana wa mambo anuai, sasa mnategemea nini? Huenda hata hio chance yenyewe wengine imepatikana kwa kujuwana au kupenyeza rupia..sasa mtakula jeuri yenu ya kuzaliwa watz.
   
 17. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #17
  Mar 8, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Wapo busy na Mamushka!!
   
 18. n

  nndondo JF-Expert Member

  #18
  Mar 8, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Sasa jamani wana JF inamaana michango yetu inaishia kulalamika tu na bado tunajiita great thinkers? let us do something, kosa ni la jamii nzima kuthamini makaratasi, paper country badala ya uwezo wa mtu, Chuo kikuu cha DSM walimu wanafundisha darasani kwa kiswahili, kitengo cha biashara kwa mfano, walimu wenyewe hawajawahi kujua soko linasema nini wao wenyewe wamefaulu kwa kupendelewa kwa Ukabila na sasa Udini, na ndio hao kila siku wanateuliwa na Rais huku mara huku, na sisi wengine tunabaki kuwashangilia sasa motivation ya kuwa tofauti iko wapi? Tunacheka lakini hilo shindano lina influence kubwa sana katika soko la ajira kwa sasa. Mwaka jana bungeni mama Getrude Lwakatare ali raise hiyo issue, sikuamini waziri mkuu huyo huyo Pinda anayesifiwa akamjibu kihuni tu, eti hao wakenya ni Kiingereza tu barua zao tunaziona maofisini hawana lolote. Tazama hiyo wizara ya elimu ilivyo kichekesho, wabunge wamejaa vihiyo wa Elimu, ma rural medical aiders, watu wasio na shule tumewaita madaktari tunawasaidia kutufisadi, na hata hao wanafunzi Tazama vyuo vilivyoshupalia MBA wanafunzi mamia kwa mamia, tazama hizo curriculum zinavyotia kinyaa. Narudia tena kusema kwamba tutajidanganya na makaratasi tutapata mpaka PHd, lakini tutarudi sokoni na kuajiriwa kama ma cleaners na ma messengers. Hizo shule za kata uchafu mtupu halafu maghembe anajitia kupiga kelele eti watu wake wamwambie kwa nini wanafunzi wamefeli, je ni watoto wangapi wa wakubwa tunasikia walifeli chuo kikuu hicho hicho kisicho na elimu na walimu wanaotakiwa kusimamia maadili wakampasisha na leo hii wamepewa vyeo. Kuna elimu hapo ya nchi? ndugu zangu, sisi tusomeshe watoto wetu kwa mfumo tofauti ili waje kuwa mabwana wa hao watwana wanaozalishwa leo na system yetu mambo ya kitaifa yametushinda tujali ya binafsi sasa
   
 19. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #19
  Mar 8, 2010
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,851
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145

  Bila ya red kubadilishwa tutafika mahali nchi nzima ni mambumbu tuuuuuu
  Shame on those leaders!!!:mad:
   
 20. p

  pareto 8020 Member

  #20
  Mar 9, 2010
  Joined: Mar 7, 2010
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi naomba nianze kwa kuwatetea vijana wetu...kushindwa kwao kujibu maswali vizuri mbele ya kadamnasi ya watazamaji wa TV karibia Afrika nzima,hakumaanishi kwamba vijana wale hawana uwezo. Mara nyingine tension ya kuwa quizzed mbele ya TV waweza kuingia kiwewe,na hio sio kwao tu,wapo watu wazoefu waliowahi kujikanyaga kwenye kujibu maswali (mfano Obama wakati wa moja ya debate zake na bibi Clinton wakati wa primaries za US aliwahi kuchemsha). Labda huko nimekwenda mbali,tuangalie humuhumu kwenye jamii forum ni wangapi wanahofu ya kujikanyaga kwa hoja zao kiasi kwamba wanaamua kushiriki katika mijadala kwa kutumia majina ya bandia~mimi nikiwa mmoja wao).

  That said nirejee kwenye hoja ya msingi kuhusu kushuka kwa viwango vya elimu. Nakubaliana na wote kwamba ni kweli viwango vyetu vimeshuka na responsibility ya kushuka viwango hivyo ni makundi (3).
  1) serikali (kwa kutoweka na kusimamia viwango vya elimu-hali hii imepelekea mashule kutokuwa na waalimu bora; vitabu vya kufundishia; maabara za sayansi na miundombinu inayofaa.

  2) Jamii (kwa kushindwa kutoa kipaumbele katika masuala ya elimu. Jamii ingekuwa proactive katika kuchangia elimu, kufanya tathmini ya viwango na kutoa ushauri sahihi na kujitolea kufundisha vijana wetu pale ambapo kuna pengo la waalimu. Jamii ya Kenya, Ghana-ime institutionalize zoezi la kuchangia elimu over and above serikali inavyofanya (harambee), wakati wenzetu wana fundraise kwa ajili ya kupata fees za kusomesha watoto sisi tuna fundraise kugharimia harusi za watoto. Ukiachilia NGO chache kama Haki elimu, wanajamii hatuna utamaduni wa kutoa constructive criticism/ideas juu ya kuboresha elimu na pia kama. Jamii hatujaweza kujitolea kuwasaidia wanafunzi wetu...while tumekazania kuwataka makondakta wawasaidie wanafunzi kusafiri kwenye mabasi,sijawahi kusikia wanachama wa chama cha mainjinia kikijitolea kufundisha hesabu kwa wanafunzi wetu katika kipindi cha likizo, sijaona tukijitolea as community service ku spend 20hours per year kwenda kufundisha shule ya kijijini kwetu au mtaa wetu. Laiti kila msomi Mtanzania angejitolea masaa 20 tu kwa mwaka kuwafundisha vijana wetu...walau tungepiga hatua. Ukiangalia masaa tunayotumia kwenye vikao vya harusi,kitchen party,sherehe zenyewe, misiba, socializing kwenye vilabu kwa wastani kwa mwaka yanazidi masaa ishirini tunayoongelea. Hatuhitaji kusubiria volunteers kutoka Korea na Peace Corps waje, tuanze wenyewe...

  Kundi la mwisho ni la wazazi. Hivi kweli mzazi unahitaji serikali ije nyumbani kwako kusimamia homework za watoto wako? Wangapi tuna spend muda nyumbani kukagua maendeleo ya shule ya watoto wetu na kutoa mwongozo? Katika hili twaweza kuwasamehe wale wazazi ambao hawakupata fursa ya kusoma, lakini wapo wasomi wengi tu ambao hawana muda wa kusimamia watoto wao?

  Kwa hali hiyo tatizo la viwango vya elimu linatokana na sababu pana zaidi ambazo sote tuna wajibu wa ku play our part.

  Kama unadhani wale vijana wa Arusha uwezo wao mdogo, subiria miaka 12 ijayo, mtakapowaona vijana walio product za hizi shule za kata zenye waalimu walioandaliwa kwa mfumo wa fast-tracking...huko kutakuwa worse zaidi.

  My worries sio vijana hao kushindwa kushiriki katika competition ya ZAIN, bali nahofia kama watamudu ushindani katika fursa za kazi,pale watakapokuwa wanashindana na wenzao wa Afrika Mashariki
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...