Zaidi ya watu 700 wamekufa wakiwa mikononi mwa maafisa wa polisi nchini Kenya tangu mwaka 2007

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Zaidi ya watu 700 wamekufa wakiwa mikononi mwa maafisa wa polisi nchini Kenya tangu mwaka 2007. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa na mashirika ya kutetea haki za binadamu.

Hata hivyo, msemaji wa polisi nchini humo Charles Owino amekanusha ripoti hiyo akisema kuwa maafisa wa polisi huzingatia sheria wanapotekeleza majukumu yao.

Takwimu kwenye tovuti la Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Missing Voices, linaloijumuisha Tume ya Kutetea Haki za Binadamu nchini Kenya, zinaonesha kuwa mauaji yaliyotekelezwa na polisi mwaka 2020 ni ya pili yakilinganishwa na kipindi cha ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007. Ripoti hiyo inaeleza kuwa watu 144 waliuawa na maafisa wa polisi mwaka huu.

Inasemekana kuwa asilimia 59 ya mauaji hayo yalitokana na polisi kuwaua washukiwa kwa kuwapiga risasi. Mauaji mengine yalitokana na mateso na kurushiwa mabomu ya machozi.

Kufikia Juni watu 15 walikufa mikononi mwa polisi. Baadhi ya vifo hivyo vilitokea wakati polisi walipokuwa wakitekeleza amri ya kutotoka majumbani.

Hata hivyo, msemaji wa polisi Charles Owino amesema mauaji yaliyotokea yalifanyika kwa bahati mbaya wala hayakukusudiwa.
 
Back
Top Bottom