Zaidi ya watu 10 wauawa Mashariki mwa DR Congo

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Machafuko mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu kumi katika siku tatu, vyanzo vya kijeshi na vya eneo hilo vimesema Jumapili.

Zaidi ya makundi ya wanamgambo 120 yamesambaa mashariki mwa DRC, na kuna mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya raia.

Wanajeshi 2 ni miongoni mwa waliouawa tangu Ijumaa.

Kiongozi wa kijeshi katika jimbo la Kivu Kaskazini amesema Jumapili “Tumempoteza mwanajeshi shujaa katika shambulio dhidi ya ngome yetu katika kitongoji cha kaskazini mwa mji wa Butembo lililofanywa na wanamgambo wa Mai-Mai”.

Kiongozi huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe, amesema wanamgambo wawili wa kundi hilo waliuawa.

Katika jimbo la kaskazini mashariki la Ituri, wachimba dhahabu 6 wameuawa Jumapili na kukatwa vichwa na waasi wa kundi la CODECO, Prince Kaleta, ambaye ni kiongozi wa shirika la kiraia huko Lodjo, Ituri ameliambia shirika la Habari la AFP.

CODECO ni kundi la kisiasa na kidini ambalo linadai kuwakilisha maslahi ya watu kutoka kabila la Lendu.

Linachukuliwa kama moja ya makundi ya wanamgambo yanayofanya ukatili, na linashtumiwa kwa mauaji ya kikabila huko Ituri.

Raia watatu waliuawa Jumamosi usiku katika shambulio lilofanywa na waasi wa kundi la ADF huko Kivu Kaskazini, amesema Flavien Kakule, mkuu wa mtaa katika eneo la utawala wa Bashi, wilaya ya Beni.

---------------------

More than a dozen people dead in eastern DRC violence

Attacks by militias across eastern Democratic Republic of the Congo leave over a dozen people dead since Friday, including six miners who were decapitated by CODECO group rebels, officials say.

Violence in eastern Democratic Republic of Congo has left more than a dozen people dead in three days, military and local sources said.

Sunday's statement included two soldiers, who were among those killed since Friday.

Over 120 militias roam the country's volatile east and there are frequent attacks on civilians.

A military leader in North Kivu province said on Sunday: "We have just lost a brave soldier killed in an attack on our position in the northern outskirts of the city of Butembo by Mai-Mai militiamen".

The leader, who did not wish to be named, said two members of the militia were killed.

On Sunday in northeastern Ituri province "six gold miners were killed and decapitated by rebels from the CODECO group", Prince Kaleta, civil society president in Lodjo, Ituri said.

Deadliest militias
CODECO, the Cooperative for the Development of the Congo, is a political-religious sect that claims to represent the interests of the Lendu ethnic group.

It is considered one of the deadliest militias, blamed for ethnic massacres in Ituri.

Three civilians were "killed in an attack by the Allied Democratic Forces (ADF)" in North Kivu on Saturday night, said Flavien Kakule, head of a locality in the Bashu chiefdom, Beni territory.

Daesh terror group claims the ADF as its regional affiliate.

During protests against the United Nations in southern North Kivu on Friday and Saturday, "there was a death among the demonstrators, who carried bladed weapons and threw stones at a base of the Blue Helmets" in Kiwanja, Jason Ntawiha, mayor of the Rutshuru commune, said.

A soldier who "had just killed a civilian in Kimoka" was "killed and lynched by the angry population", Saturday, commander of the Congolese Army regiment in Sake Colonel Philemon Kakule said.

Source: trtworld
 
Dunia ikikaa kimya bila ya kuifanya chochote Nchi inayo chochea mgogoro huu - hata siku moja Congo DRC hisitegemee kwamba itakuwa na amani ya kidumu - wahusika wanafanya unyama huu kwa kujua hivi sasa attention zote zinaelekezwa huko Ukraine na wao wanatumia opportunity hiyo kufanya mambo yao.

Labda niwakumbushe jambo dogo lakini lenye maana sana - Uingereza na Merikani ndiyo wanachochea mgogoro/vita nchini Ukraine - sasa angalia ni Taifa gani la Afrika mashariki na Afrika ya kati ambalo limetembelewa sana na top officials wa Serikali za Uingereza na Merikani ndani ya muda mfupi - what does that tell you?

Kitakacho fuata baadae utasikia wanalazima azimio la kutaka Congo DRC igawanywe kwa kisingizio kwamba Congo DRC is too big a country - yafanyike yaliyo fanywa huko Sudan - nawambieni lengo kubwa la kuchochea vurugu kwenye jimbo la kivu wanataka liwe annexed, watatoa visingizio mbali mbali lakini lengo lao kuu ni hilo na wanajua watapata support kubwa kutoka Uingereza na Merikani - haya si mambo madogo hata kidogo, Tsishekedi anapaswa kuwa makini sana sana kwa kile kinacho endelea huko jimboni Kivu - jamaa wamekwisha lifanyia mahesabu makali jinsi ya kulipora.

Wakongomani wakitaka kunusu jimbo la KIVU lisimegwe waombe msaada kutoka kwa Putin, hawana jinsi - wawaige wenzao wa Africa ya kati walio omba msaada kutoka Russian special forces ku-deal na ujeuri wa Ufaransa na Merikani katika taifa lao - bila Tsishekedi kutumia mbinu hizo jimbo la Kivu litaendelea kuwa pasua kichwa kwa Utawala wa Kongo

Kumbukeni kwamba viongozi waliokuwa na uwezo mkubwa wa kukomesha ujinga huu walikuwa ni akina: Robert Mgabe, Jacob Zuma, Dos Santos, Mkapa na Sam Nujoma - bahati mbaya majority wamekwisha tangulia mbele ya haki.
 
Back
Top Bottom