Zaidi ya watoto milioni 2 wakosa msaada Tigray

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Maelfu ya watu kutoka Tigray, Ethiopia wamekimbilia Sudan. Umoja wa Mataifa umesema kuwa zaidi ya watoto milioni mbili katika jimbo la Tigray nchini Ethiopia wamekatizwa na misaada ya kibinadamu huku ghasia zikiendelea.

Licha ya makubaliano ya yaliyofikiwa na serikali ya Ethiopia, mashirika ya kutoa misaada yanalalamikia kuzuiliwa kuingia Tigray ambako vikosi vya serikali vimekuwa vikikabiliana na wapiganaji wa Tigray Liberation Front kuanzia mapema mwezi Novemba.

Shirika la watoto la Umoja wa Mataifa, Unicef, linahofia kadri linavyochelewa kuwafikia watoto katika eneo holi ndivyo hali yao wanaohitaji msaada wa dharura itaendelea kuzorota. Mapema mwezi huu wanajeshi waliwaelekezea marisasi wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Tigray.

Serikali imesema wafanyakazi wa UN hawakuwa na ruhusa ya kusafiri katika eneo hilo na kuwalaumu kwa kuvuka vizuizi vilivyowekwa barabarani.
 
Back
Top Bottom