Zaidi ya wakimbizi 50 wauawa Ituri, Congo

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,009
9,874
1643820930286.png

Wakimbizi zaidi ya 50 wameuawa usiku wakuamkia leo Jumatano katika kijiji cha Ngujona wilayani Djugu katika mkoa wa Ituri. Yamefanyika wakati juhudi zinaendelea za kuwahamasisha waasi kuzisalimisha silaha zao

Akizungumza na DW kwa njia ya simu, kiongozi wa utawala wa Bahema Badjere Jean-Richard Dedha alisema, kuwa waasi wa CODECO walijipenyeza kwenye kambi ya wakimbizi Savo katika kijiji cha Ngujona,saa nne za usiku na kuwauwa wakimbizi pamoja na kuwakeruhi wengine wengi.

Chifu Jean-Richard Dedha anatuambia jinsi walivyouawa wakimbizi hao zaidi ya hamsini, pale akitupatia hali inayojiri katika kijiji cha Ngujona, baada ya shambulizi hilo ( O-ton Chifu)

Mauwaji haya kwa mara nyingine yanafanyika, wakati mikoa ya Kivu ya Kaskazini pamoja na Ituri ikiwa katika hali ya dharura, viongozi wa jeshi wakiwa waliteuliwa na rais Félix Tshisekedi, ili kukabiliana ipaswavyo na makundi ya waasi katika mikoa husika.

Kusuasua kwa operesheni za kuwatokomeza waasi katika mkoa wa Ituri pamoja na mauwaji ya kila mara, John Kabwa mmoja wa wazee wa busara wa kabila la Bahema, pamoja na kulaumu mauwaji ya wakimbizi, anatoa mwito huu kwa rais Félix Tshisekedi

Aidha waasi wa CODECO wanawauwa wakimbizi, wakati pametumwa Bunia tume ya viongozi wa zamani wa makundi ya waasi, ilikuwahamasisha wapiganaji wa makundi ya waasi kuzisalimisha silaha zao. Wajumbe wa timu hiyo inayoongozwa na Thomas Lubanga kiongozi wa kundi la zamani la uasi UPC,wamekuwa wakikutana kwa mazungumzo na wajumbe wa makabila mbalimbali ya Ituri pamoja na mashirika mbalimbali ili kuwahamasisha kuhusu amani.

Na huko hayo yakiwa namna hiyo, askari wa jeshi la Uganda UPDF wamepelekwa katika wilaya ya Irumu mkoani Ituri, kukabiliana na waasi kutoka Uganda ADF, wanaowauwa wakaazi katika wilaya hiyo,kuteketeza vijiji, kuchoma moto magari pamoja na pikipiki.

Kutumwa huko kwa wanajeshi hao wa UPDF katika operesheni za pamoja na jeshi la Congo FARDC, kunadhaniwa na wengi kwamba kutachangia pakubwa katika kuwatokomeza waasi katika wilaya hiyo.

DW
 
Hivi mtu unaenda kuua wakimbizi wanakosa gan?

Huku wakimbizi 50 wanauawa,huku wananchi 27 wanapigwa shoti ya umeme na kufariki,poleni sana DRC
 
Dah!..Drc inavuja damu isiyotaka kukauka.
Nj i wazungu tu waondoke,
Mbona wataishi vizuri tu,
Wazungu si watu wazuri wanaiba sana mali hapo huku wakichochea vurugu kwa jina la misaada
Wazungu hawahusiki chochote pale -kwa ninihujiuluzi inakuwaje mauuaji ya mara kwa mara yanatokea katika majimbo yanayo pakana na Rwanda!! Je,hawa wanao itwa wakimbizi wanatoka nchi gani na wana asili ya kabila gani - ukisha gunduwa ukweli ndio utajuwa kinacho endelea nyuma ya pazia
 
Wazungu huwa wanaenda indirect,
Ni wajanja sana huwezi kuwagundua kwa akili ya kawaida
Inabidi uwe mjanja kuwazidi🤣
Ndio utagundua ni wao wanahusika,
Wewe ni mzungu?
 
Wazungu hawahusiki chochote pale -kwa ninihujiuluzi inakuwaje mauuaji ya mara kwa mara yanatokea katika majimbo yanayo pakana na Rwanda!! Je,hawa wanao itwa wakimbizi wanatoka nchi gani na wana asili ya kabila gani - ukisha gunduwa ukweli ndio utajuwa kinacho endelea nyuma ya pazia
Distance from Ituri Hadi kwny mpaka wa Rwanda Ni km 500.Sijui Ituri inapakana vipi na Rwanda hapo.Lkn hayo Ndio matatizo ya kutumia kichwa kufugia nywele.
 
Distance from Ituri Hadi kwny mpaka wa Rwanda Ni km 500.Sijui Ituri inapakana vipi na Rwanda hapo.Lkn hayo Ndio matatizo ya kutumia kichwa kufugia nywele.
Tangu miaka ya 1996 mpaka Sasa Rwanda na Uganda wanatajwa kama (aggressors) na ripoti mbali mbali za UN hivyo hata kama hawahusiki ni raisi sana kunyooshewa kidole sababu ya rekodi zao za nyuma.
 
Tangu miaka ya 1996 mpaka Sasa Rwanda na Uganda wanatajwa kama (aggressors) na ripoti mbali mbali za UN hivyo hata kama hawahusiki ni raisi sana kunyooshewa kidole sababu ya rekodi zao za nyuma.
Then wakishawanyooshea kidole hua wanawafanya Nini?
 
Back
Top Bottom