kama tukimuandaa mnyika vizuri anaweza faa kuja kuwa raisi wa nchi hii kwa sababu katulia na tundu lissu ni mzuri sana ila anajazba na uraisi unahitaji utulivu wa hali yajuu sana na zito kabwe ni mzuri ila ni mwepesi wa kugeuka geuaka na kuangalia maslai yake binafsi naye mkubali zaidi ni mnyika
ni unafiki na majungu pamoja na hali ya kufilisika kifikrahivi mtoa thread amekosa jambo lolote la maana la kutaka tujadili? sioni kama kunafaida ya kumjadili nani atakua Rais mbadala wa Dr Slaa wakati hakuna hata mmoja anaejua ataishi miaka mingapi na swala la umri kumtupa pia ni unafiki na majungu hebu jiulize mzee mandela alikaa jela miaka mingapi na aliukwaa urais akiwa na miaka mingapi? pia mugabe ambae ameshupalia Urais wa zimbambwe mara ya mwisho kugombea alikuna ana umri gani? pia mpinzani wa barack uboma bwana macain alikua na umri gani wakati wa uchaguzi wa marekani? wana jf tumpe moyo Dr Slaa na kumuombea maisha marefu na sio kuanza kuleta majungu humu jamvini, nawasilisha
tujadili wa CCM
siyo lazima ujadili .... kwani wewe ni chadema .... hujui maana ya forum wewe.... forum inatumiwa na groups mbali mbali kwa kuanzisha threads kujadili mambo yanayowakabili ..... and open to anyone .... unaruhusiwa kuanzisha thread inayohusu KAFU na wana kafu wakachangia au mtu yeyote .... wewe ni nani unakataza hii thread ... au wewe ni kamati kuu ya chadema .... ufikiri rojorojo huu
najua sio lazima kwa mimi kuchangia lakini nilazima tunapooona upotoshwaji ni wajibu wetu kuukemea, wewe mtoa mada umetumwa na waliokutuma hawana nia njema na nchi yetu ni lqazima niwe mkali kwa jambo lolote linalohusu maslahi ya nchi yangu, DR Slaa ni national symbol of changes na nilazima utambue unapomuengelea mtu huyu unawagusa wengi, kwa hiyo jaribu kua na busara na pia jaribu kufikiri kabla ya kuropoka, hunijui sikujui na iweje useme mimi ni kamati kuu ya chadema? unajua nilipo na ninafanya nini? acha majungu tunahitaji klujadili mambo ya maana na sio upuuzi wako ambao hauna mantiki wala logic. jipime mwenyewe kwanza then wapime wengine.
wavumao papa, na wengine wapo.ebu jama naomba tujadiliane ndani ya chadema nani mwingine anafaa kugombea urais maana mh slaa umri unamtupa mkono ili tumjue tuanze kumpima sasaivi