Zaeni mapema acheni ubishoo

Ahahaaaaaa. Nilichogundua hapa wengi ni vijana wa hotpot,sasa hili swala la kuoa linawaudhi kweli kweli. Mdau Anamaanisha japo 26 uwe umeshaoa.
Hawataki kuelewa hawa, watalea watoto wakati wameshakuwa vikongwe.
 

Kwi kwi kwi kwi!! Umenitukana lkn ikabidi nicheke tu badala ya kukasirika. Ni hivi bro mila zetu unapopevuka kwanza unapewa hilo wazo la kuoa na wazazi endapo wameshaona una uwezo binafsi wa kukaa na mke. Ukiafiki wazazi watakushauri baadhi ya familia ambazo wao wameshazifanyia uchuguzi kuwa zina malezi bora. Baadae katika hizo familia (mfano tatu) utachagua mwenyewe ni yupi umevutiwa nae hapo ndipo utapeleka posa na kuelezea namna utakavyoishi na huyo mchumba pindi unasoma. Ndugu usifikiri wote tumekuwa kama ulivyokuwa na kama kuna mapenzi ya kweli mke atakusubiri na atakuvumilia safari yako yote ya maisha pia naamini hata leo kuna watu wanarudi masomoni wakiziacha familia ama wake zao Aidha kwa wazazi ama ndugu. Tatizo lako ndugu yangu Zeroseventytwo umezoea kupata wachumba Badoo na Waplog sasa hapa sifikirii kama utanielewa.
Mwisho nakukaribisha kwenye familia yangu hiyo huku kanda ya ziwa.
 
Last edited by a moderator:

Aaaaaaaahah! Naomba nikupachike jina la LOGICAL THINKER.
 
kwa upande wa wanaume wengi wanaogopa majukumu na kwa upande wa wasichana wengi wanaogopa matiti yao kudondoka kutokana na kunyonyesha
 

Mimi nachojua ni kwamba hicho ulichokiandika kinapatikana zaidi kwenye familia za kifugaji. Unakuta kijana wa miaka 16 tayari ana mke na mtoto lakini bado anakaa kwa baba yake yeye na mke wake. Shughuli zote za uzalishaji anafanya na kinachopatikana ni Mali ya baba yake.

Kwa mtu ambaye ana malengo hasa ya elimu kuzaa Mara nyingi unakuwa akiwa na 30 yrs.
 
Last edited by a moderator:

Hapana kaka maisha yamebadilika hivi karibuni ila binafsi mleta uzi tukiacha matani ameongea pointi kabisa sema tu changamoto za maisha ndizo zinatufanya tuchelewe kuoa lkn mimi nilipitia njia hiyo mkuu pia ni nadra sana kwa sasa kupata mwanamke msitahimilivu. Mwaka huu Mdogo wangu kamaliza mafunzo ya ukunga huko Bombo Hospital Tanga lakini tayari alikuwa ameoa na watoto wawili na sasa yupo anaishi na watoto wake kwani tayari ameshaajiriwa ktk hospital ya mtu binafsi.
 
You are 100% right. Wote waliopitia vyuoni miaka mitatu au minne wengi wanaoa baada ya 30. Majority 32 na 33. Kwa hiyo hesabu wengi wanaangukia hapa. Uko 50 mtoto wa kwanza ndio anamaliza form 4.

Walibahatika kupata watoto obvious nje ya ndoa, wakiwa chuoni utakuta wana watoto wakubwa wakiwa 50s. Shida ndio hiyo kuoa ukiwa chuoni, kuoa baada ya chuo, kuoa kabla ya kujiandaa hata kwa kibarua, etc etc ndio changamoto za ukweli. My be sio ubishoo. Ni hali halis
 
Twapaswa kuzaa na kulea. Malezi ya kimwili, kiroho na kijamii. Sio kuzaa au kuzalisha tu kisha tuna ujenga ufalme imara wa shetani. Hivyo umri wa kuzaa wapaswa kuwa ni ule ambao wazazi wameamua na kuwa tayari kiakili, kiuchumi na kiroho. Nawasilisha. Mm nilipata mwanangu wa kwanza nikiwa na miaka 26, ni kweli kwa sasa ninatamani ningeoa nikiwa na miaka 23! Ila maandalizi ya malezi hayakutosha muda huo.
 

????ASANTE nadhani ameelewa
 

Inawezekana mkuu mbona mm nna 25yrs na nna mke na mtoto and we both have a good job
 
Ungesema vijana wajipange kimaisha mapema, ili waweze kuzaa na kutunza watoto wao vizuri na mapema ningekuelewa. Wengi wa wanaozaa mapema ndio wanatupa watoto, na kusababisha watoto wa mitaani.
 
Daah kwa mawazo haya maendeleo tutazidi kuyaona kwa wenzetu
 


Yote maisha, kuwahi au kuchelewa kila mtu aonavyo, formula ya maisha si ya kuigana
 
Mim nlioa nkiwa na miaka 23 baada tu ya kumaliza chuo i thankd God sijawahi kujuta kuwa kwnye ndoa hii na nimeona mafanikio mengi sana kiakili na kiuchumi lkn wenzngu ambao walinishangaa sana kipindi hcho ambao wengine bado wako wanaishi na wazaz wao mpka leo hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…