Hahahaaa hao wanigeria walishawahi kutengeneza mpango wa kunipiga kama tsh1.5m mwaka 2010.......pona yangu ilikua ni kwamba nilikua na hela pungufu....ilipelea kama laki nne hivi kukamilika tsh1.5m , sasa nilipoenda kwa washkaji kuwaazima ile kuwapa na story jinsi mwenzao ninaenda kuwa milionea baada ya week chache.....ndo jamaa kunifungua ubongo aisee.
Inshu ni kwamba walinitumia msg via email kwamba simu yangu ya tecno p5 imekua moja ya simu zilizo kwnye matumizi ambazo zimejishindia USD 500,000... na droo ilifanyika huko kwenye one of the main company of Tecno manufuctures,,,, na email yao ilionesha hvo na hata nilipo search mtandaoni niliona hicho kitu na ni kweli droo hyo ilifanyika na ni kweli watu kibao walishinda kwnye droo hyo ingawa nilipocheki, wengi waliishia USD 40000,
Sasa kuja kucheck mim nimeshinda USD 500,000 afu sipo kwnye list pale,,,, nikawacheck jamaa,, wakanambia wajaniexpose for security purpose mana nimeshinda hela nyingi sana ingekua rahisi hata kuvamiwa na kutekwa.......Nikaamini.
Basi yakafata mainshu ya kuwatumia vitambulisho, Status zangu zote,,, kuanzia full name, address, mpka nationality na vitu vingine vingi.
Yani kwa kifupi ilikua ni busy week kwangu kwa kuhakikisha naupokea utajiri wangu kisawasawa kwa tabasamu na bashasha....
Jamaa wakanicontact kwamba wanakuja kunihand over huo mkwanja personally kupitia arusha wakiongazana na waandishi wao wa habari...
Nikajisemea ((Huu ndo wakat wa kuwanyoosha mademu walionitosa kudadeki)))
Kweli baada ya week nikashangaa napokea simu namba ngeni,,,,,ile kupokea tu nakutana na lafudhi ya kibritish kabisa aisee basi nikaulizwa pale nikajitambulisha...wakathibitisha kuwa ni mimi,,,
KIMBEMBE,,, Wakanambia wamekwamba pale airport Arusha kwa madai kuwa wameambiwa hawawezi kuvuka kuingia tanzania wakiwa na hundi kubwa ya fedha zote zile za kigeni pasipo ulipaji wa kodi kabisa....sasa kodi walitakiwa kulipa ni Tsh 1.5 mil.
Nikashangaa et wananicontact mim ndo niilipe hiyo hela wakati hapo bado wana mamillion yangu.....tena wananambie niharakishe kuwarushia kwa namba flan walionipatia ilikua ya tigo. Wakanambia yakizidi masaa 24 wanarudi zao sweden na kurudisha ushindi wa fedha zangu huko HONG KONG. Nilichanganyikiwa aisee kuona utajiri nlouwaza zaidi ya week mbili na kutengeneza bajeti kabisa ya matumizi unataka kuniponyoka kirahisi kiasi hiki.
Nikaenda ATM mashine nikadroo hela yote Tsh 1.1m nakuunga moja kwa moja mpka kwa rafiki yangu mmoja hivi aniongezee.....huko nikawakuta washkaji wengine watatu.....daaah nikaongea na jamaa na kumpa full story.....jamaa kabla hajanijibu shida yangu akawaambie wenzie. "" Oya hebu msikilizeni huyu"" na kuniamuru mimi "" haya wasimulie na hawa""
Basi nikawasimulia washkaji huku nikiongea haraka mana naona wananichelewesha.......looooll.....kilichofata hapo mmmmmhhh.....jamaa mpka leo huwa wananicheka.........
TULIPOWAFATILIA VIZURI TULIGUNDUA NI WANIGERIA.....SHENZI TYPE