Yutong Vs scania Vs ud

Napenda kutoa ushuhuda kuwa Scania kwa upande wa mbio ni Mnyama mwingine kabisa.
Leo tumeondoka Mbeya saa 12 asubuhi na gari zikawa kama hivi Nganga nilopanda (Scania,), Happy Nation Galaxy (Scania), Mbeya Express (Nissan Diesel) na New Force (Yutong)
Hizo ndio zilianza ligi pamoja from Nane nane ila hadi kufika Mafinga zilibakia Happy Nation na Nganga zikichuana vikali.
Kumi na moja na robo tumeshuka Ubungo.
so I vote for Scania in terms of speed.
 
Attachments

  • 1407597751538.jpg
    1407597751538.jpg
    125.6 KB · Views: 502
  • 1407597772560.jpg
    1407597772560.jpg
    108.9 KB · Views: 447
Nijibu kwenye speed,

Ni kweli Yutong ni mepesi sababu ukiacha bodi la nje, ndani ni plastic tu hivyo kuyafanya yawe mepesi. Hii ni hulka ya xinhua products kwani hata simu zao si waziona ni kubwa but nyepesi??!!

Ila usichanganye na ile topic yetu ya speed, zile factors zinabaki palepale kua at 120Kms/hr, yote yatakua Na kasi sawa.
Afadhali umetoa angalizo maana kuna watu wangeibuka na hoja 120Km/hr ya Yutong ni kubwa kuliko 120Km/hr ya Scania
 
hapa kuna kitu sijaelewa hasa kuhusu speed mana kuna wengne wanasema yutong ina 120km/hr mara wengne zaid mara wengne wanadai scaniad ndo 120km/hr so nashindwa kuelewa

Yutong ina Speed 160kph, nimeona mimi mwenyewe! Dereva aliniambia ukiifuatisha inakuua kwa kuwa ni nyepesi kuliko Scania, so kwa speed toleo la sasa la Yutong ni hatari wakuu! Ila kuhusu kuvumilia mbilinge mbilinge ilo liko Obviuos kwamba haliwezi kuvumilia kwa muda mrefu
 
Iko wapi hiyo barabara hapa Tz zilizojaa mbuzi na waendesha baiskeli ya kwenda hiyo spidi ? ?
 
Mkuu ni kweli ulichosema ila naomba nikurekebishe kidogo twende sawa... mosi katika scania namba ya mwisho huwa ni toleo ie series , namba zinazofatia ni ujazo wa engine in litres (cc) kwa maana hiyo 94 ni engine ya cc9000 (9litres ) toleo la nne, katika series one kulikuwa na option ya engine tau tu 81 ,111na 141 (v8) seies two kulikuwa na option nne 82 ,92 112, na142(v8) , series three zlikuwa option tatu 93 ,113 na 143(v8) series four kulikuwa na engine option tano 94 ,114, 124 ,144(v8),164(v8). Baada ya series four waliamua kubadilisha naming format kulingana na cabin types na uwezo wa engine (hp) that is P ,R, G,& T series kwa maana hiyo hakuna R524 bali ipo R500, R580 n.k hope nimesaidia..

Mkuu salute kwako yaani unayafahamu magari ya scania utadhani wewe ndo technical engineer wao,if so hongera.
Ninachoomba ebu tuweke wazi kitaalamu nini tofauti kati ya yutong na scania based on durability na mengine mengi.
Shukrani nazitanguliza
 
Haha, hapana mimi mtaalam wa scania, ila huwa napenda sana magari. ..
Kwa bahati mbaya huwezi kulinganisha yutong na scania kirahisi, scania ni watengenezaji wa engine na magari makubwa, yutong ni mtengenezaji wa body za mabasi, ambaye ana outsource kuanzia engine mpaka diff ,mfano yutong anatumia engine za kimarekani Cummins, a cheap to maintain ,durable and offer good fuel economy.
Fair competetion inatakiwa labda kulinganisha yutong na irrizar, au marcopolo, au zhongtong
Bus builders wa kichina wako rough sana na wanatumia outdated configuration ,mfano mpaka leo yutong mpya bado ni steel suspensioned..!!!, marcopolo na irrizar za leo ni either ,partial (air suspension za nyuma) or, full air ride (air suspension mbele na nyuma) chunguza utaona kuna baadhi basi za scania zina air suspension ,nyuma , hizi kwenye bumps huwa hazirushi, na hata kama sari ni ndefu unafika bila kuchoka .

Ila kama ukisema scania na cummins ipi inadumu, hapa mimi nadhani scania ni zaidi ya cummins.
 
Mkuu nimekuwa nakufuatilia sana,namie nakubaliana na wadau kwamba unaenda kitaalam zaidi.Maana wapo wanaopenda Speed na kurushwa,wapo wanaopenda speed na kutulia njiani.Mie kwangu Gari yenye mziki mkubwa ndio napenda hata kama ni Layland Daf.

Hembu tuje kwenye Seriouse issue.
Bei ya haya magari.
Scania ni kiasi gani na hesabu yake kwa Tajiri kwa routes za kawaida ni kiasi gani.Mfano Dar - Mwanza - Dar

Nataka nijue bei ili 2025 ninunue namie,ila suala la Mganga wa Kienyeji niachie mwenyewe,maana hizi biashara lazima gari ifungwe Hirizi.

Halafu ningependa kujua,hivi Uimara wa Bodi ya Scania na Yutong upi ni bora zaidi.Na Je Engine ya Scania inaingia kwenye Youtong kwa kuihamisha
 
Iko wapi hiyo barabara hapa Tz zilizojaa mbuzi na waendesha baiskeli ya kwenda hiyo spidi ? ?

Sijasema anakimbia kwa speed hiyo, ila nmeona pale kwenye dash board speedometer ikionyesha 160km/m kama maximum speed ya basi husika, siyo kwamba dereva alikuwa anatembea kwa mwendo huo. Hapa nilikuwa nafafanua maoni ya awali ya thread kwamba Yutong speed yake ni 110-120kph. Hiyo ilikuwa ni zamani, siku hizi wameongeza capacity. Suala la life span bado hawajafika quality ya Scania tena board za Marcopolo kama zile za Scandinavia zilitengenezwa kwa fibrous material ni imara lakini ni xtremely very expensive. Ni ghali hasa!
 
Nadhani mkuu ulikuwa na maana ya 160km/h na siyo 160km/m maana hiyo speed ni kama ya mwanga vile.
 
Tulien kwanza,, nenda ubungo terminal kaulize kitu HAPPY NATION (sauti ya manka,) scania,, then ndo ufanye ulinganifu na yutong
 
Mkuu nimekuwa nakufuatilia sana,namie nakubaliana na wadau kwamba unaenda kitaalam zaidi.Maana wapo wanaopenda Speed na kurushwa,wapo wanaopenda speed na kutulia njiani.Mie kwangu Gari yenye mziki mkubwa ndio napenda hata kama ni Layland Daf.

Hembu tuje kwenye Seriouse issue.
Bei ya haya magari.
Scania ni kiasi gani na hesabu yake kwa Tajiri kwa routes za kawaida ni kiasi gani.Mfano Dar - Mwanza - Dar

Nataka nijue bei ili 2025 ninunue namie,ila suala la Mganga wa Kienyeji niachie mwenyewe,maana hizi biashara lazima gari ifungwe Hirizi.

Halafu ningependa kujua,hivi Uimara wa Bodi ya Scania na Yutong upi ni bora zaidi.Na Je Engine ya Scania inaingia kwenye Youtong kwa kuihamisha

Hata mimi nipo curious kujua hii kitu hasa in monetary terms.

Mkuu t blj tusaidie kwenye haya.

-Bei ya Scania, Nissan Diesel na Youtong
-Revenue and Cost of Operations per route mfano Dar-Mwanza-Dar au Dar-Arusha-Dar au Dar-Mbeya-Dar
 
Last edited by a moderator:
Kwenye upande wa ubora refernce ni GreenStae, Prncess Shabaha & muro! Wanvyolaza watu njiani
 
mimi si mtaalamu wa magari lakini kwa hapa sudun mabasi yao mengi ni Yuton. Ukipita kwenye barabara yao kuu kutoka Mji wa kartoum kwenda mji wa El obeid utakutana na yuton za kutosha zilizoungua moto na zilizotelekezwa barabarani kwa ubovu. endeleeni kujadili
 
Asee zile marcopolo za andare class tu zinatosha kuhemesha viyutong tena saanaa.. Mfano mzuri bac za kilimanjaro wana andare zinakimbia balaa.. Kina ngorika na viyutong vyao wanaachwa huko..
 
Back
Top Bottom