Yussuf Manji, Omba Toba

Mawaidha mazuri lakini Manji alikwisha kuuza hicho kiwanja kwa Mtu mwingine ambae pamoja na bakwata walimshtaki sh. Ponda sijui kwanini Manji alaumiwe peke yake wakati wauzaji bakwata wameuza viwanja kwa watu wengi tu na zaidi ya hayo wamewashitaki mashehe waliowapinga lakini hawasomewi ahlul badr, kwanini ni Manji tu?
 
Duuh tatizo la yusuph ni ujeuri kwakuwa ana hela basi anawaona wengine wote maskini tu na hawana lolote la kumfanya
 
Ishara zipi zinazoonekana kwa macho ya binadamu zinaonesha mhusika ameomba toba kwa Allah, na Allah ametoa msamaha? Hiyo toba inafanyikaje?



Kama Allah ndio anajua zaidi kwa nini usimwachie jambo hili Allah?

Ndiyo kawachiwa Allah.

Toba haina kikomo.
 

Allah hachoki kusamehe. Dhambi zote anasamehe isipokuwa shirki tu.
 
Allah hachoki kusamehe. Dhambi zote anasamehe isipokuwa shirki tu.

Samahani FF,, nifumbulie hicho kitendawili. Dhambi ya shirki ni ipi ka sio hiyo unotaka Manji aturudishiye?? Alishaombwa na kuendewa na wenye haki wakamuonya dhidi ya hii dhulma, hadi imeamuliwa kumsomea dua. Sasa, acheni dua ifanye kazi yake kwani kibri dawa yake ndo hiyo. Hatutaki tena kuishiriki hiyo dhambi yake huyu bwana Manji. Aombe mwenyewe, Maulana akimsamehe na kumrejeshea awe funzo kwa wengi. Msidhani madhulumati yameisha, HAPANA. Yamejaa tele acha Mola ayafunze kwa dawa chungu
 

Malizia basi, na waliomnyang'anya Oyster Bay? Na waliomtia ndani kwa tuhuma za madawa ya kulevya? Na ..., na...?
 

Soma vizuri post namba moja.

Lini nilikubali Ponda kuadhibiwa? Lini nilikubali Manji kuuziwa viwanja vya Waislam?

Fikiri kabla hujakurupuka.
 
Pia tuwashauri na viongozi wa BAKWATA walioshiriki kufanya biashara na Manji kuomba toba.

Tena haraka sana. Kuna waliokufa midomo ikakataa kufunga. Si ishara njema.
 

Hiyo ndiyo ukisikia irada ya mwenye kudhulumu. Hazidishiwi isipokuwa hasara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…