Yupo Njiapanda, mpenzi anaumwa!

Yupo Njiapanda, mpenzi anaumwa!

kitalembwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2014
Posts
8,273
Reaction score
22,062
Wanabodi, wasalaam!

Ni muda kidogo sijaweka bandiko hapa, Mara nyingi nimekuwa msomaji wa nyuzi mbali mbali zinazowekwa hapa!

Twende kwenye mada! Nina jamaa yangu ana mpenzi wake, mwakani anataka wafunge ndoa rasmi, walishatambulishana pande zote mbili, na Mungu akipenda mwezi April anaenda kumlipia mahari!

Hawa watu wanaishi mikoa tofauti kutokana na changamoto ya kikazi, wanatembeleana wapatapo muda, huyu mpenzi wa kike hapa majuzi alimwambia jamaa yake kuwa huwa anasumbuliwa na pumu, jamaa alishtuka Sana japo hakumuonyesha Kama kashtuka, jamaa anaomba nimpe ushauri amchukue au vp ? Huu ugonjwa Ni wa kurithi, pia jamaa analaumu muda wote wamekuwa wapenzi (3yrs) kwa nn hakumwambia?

Huyu mpenzi wake anaishi mkoa wa baridi Sasa mara kwa Mara anaumwa kifua, pia Kuna muda sauti inabana jamaa alikuwa anahisi ni Hali ya kawaida tu kumbe Ni pumu!

Katika kumdodosa, bidada kakiri kosa, na pia kasema Kuna vidonge huwa anavitumia siku nyingi tu ndio vinamsaidia !

Jamaa yupo njia panda hajui Cha kufanya, kaniomba ushauri, hata wazazi na ndugu hajawaambia!

Ushauri wenu utakuwa msaada mkubwa kwake na kwa wengine hapa jamvini !


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aachane nae akatafute mkamilifu na natumai atampata!
Anaweza kutana na yeyote huko mbele haumwi lolote ghafla inaibuka kansa wanahesabu miaka ya kuishi..
Na anaweza akampata asie na lolote akafa mapema huyo mwenye pumu akafika uzeeni.
Kama anahofia kuzaa mtoto mwenye pumu kurithi kutoka kwa mama.. Sawa
Anaweza kwenda huko akazaa albino akaanza kumlaumu mke kwanini hakumwambia..

Namshauri tu akimuacha huyo dada akampata mpya ahakikishe anatambulishwa kwa ndugu wa ukoo mzima na hadi mababu wa kale na health status zao.. Sababu genes zinatembea bado!

Rafiki ako ni bogus na hana utu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kosa ni kuwa huyo mwanamke alificha ugonjwa jambo ambalo si sawa katika mahusiano.
Mahusiano mazuri inabidi kuwekana ukweli na uwaz kwa kila kitu. Kama anamuoa aoe tu ila akiona hataweza kuishi nae bas maamuzi ni sasa ila ajue akishafunga ndoa tayari hapo atakuwa ameingia kwenye kifungo kingine ambacho hakuna wa kukitenganisha bali kwa mapenzi ya Mungu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kosa ni kuwa huyo mwanamke alificha ugonjwa jambo ambalo si sawa katika mahusiano.
Mahusiano mazuri inabidi kuwekana ukweli na uwaz kwa kila kitu. Kama anamuoa aoe tu ila akiona hataweza kuishi nae bas maamuzi ni sasa ila ajue akishafunga ndoa tayari hapo atakuwa ameingia kwenye kifungo kingine ambacho hakuna wa kukitenganisha bali kwa mapenzi ya Mungu

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakika upo sawa,, mwanamke amekosea pia nikosa mwanaume kumwacha mwanamke coz kaona anashida fulani.Wamedate 3years akiwa na pumu yake na maisha yakawa poa.Why amuache sasa,,No one is perfect.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anataka amuache kwa sababu ya pumu?haya amuache akutane na mwenye ukimwi kuna watu wanajiona wakamilifu sana leo anawaza kumuacha shida pumu je kesho ataweza ishi nae ikitokea bi dada amekatwa miguu yote
 
Back
Top Bottom