Ni sahihi kumsaidia mpenzi wako wa zamani akikwama?

kitalembwa

JF-Expert Member
Jul 12, 2014
2,866
7,156
Wakuu, salaam!

Ni muda kidogo sijaweka andiko hapa, lakini Mimi Ni msomaji mzuri wa hapa jukwaani!

Nilikuwa na mpenzi wangu kipindi Cha nyuma nikiwa nikiwa na miaka 21-24, Ni msichana tulietoka Kijiji kimoja, japo shule Ni tofauti! Mapenzi yetu yalianzia chuoni!Nilimpenda Sana , mapenzi yalishamiri Sana kipindi hicho tupo chuo, na nikiri wazi kuwa hata boom langu amelila Sana, achilia mbali kumsaidia kazi za kitaaluma!

Nikiri wazi, mm ndiye nilikuwa nampenda kuliko yeye alivyonipenda, Ni mtu flani Alikuwa ananata Sana, akishasema kitu amesema , pia mnaweza kuwa na outing akaja kui-cancell dakika za mwisho kisa Jambo la kijinga tu ! Kufupisha story hapa tulipitia ups na downs nyingi tu , tulishaachana Mara kadhaa lakini nakuwa mpole Tena tunarudiana! Na Ni mtu Alikuwa na dharau Sana, kidume najipinda namtoa kidizaini pesa ya kujikimu lakini wapi !!!

Tukamaliza chuo, tukarudi mtaani, hapa nilisota kidogo yeye akawa Kuna mahali anajishikiza japo kwa muda, dharau zikaanza , Mara hajibu sms on time , Mara WhatsApp hajibu (anasoma lakini anapotezea) , unaweza kumpigia Mara kadhaa asipokee baadae akija kuona simu Wala hakutafuti hata ile kinafki kwamba alikuwa busy,,,, tukaachana rasmi ,!!

Mimi nikabahatika kupata kazi mkoa mwingine , nilivyohama ndo chansi ya kumsahau kabisa, nilikuwa naambiwa tu habari zake kwamba kibarua kiliisha na yupo yupo mjini tu anaunga unga ,,,,(anadanga)

Tokea kipindi tunaachana miaka mitano imepita, juzi Kati kipindi covid 19 inapamba Moto nikaja kijijini kusalimia (mind that sio kwamba sijawahi kuja nyumbani Ni kwamba sikuwahi kuja nikamkuta, nahisi tulikuwa tunapishana ), sasa bwana nikaambiwa mchumba wako anamtoto (baadhi ya wanangu wa kitaa walikuwa wanayajua mahusiano yetu) !!

Eeeh bwana eeh nikafunga safari kwenda kwao na jamaa yangu kumsalimia na kumsabahi,,, kwao pana kiduka, nilimkuta yeye ndiye anauza hapo! si mnajua Ni Yale maduka (vioski) vya kijijin vinavyouza mahitaji muhimu tu,,,kwa haraka haraka hapawezi kuwa na mauzo ya 50k per day, labda 25-30!

Alivyoniona alihamaki Sana , hakutegemea na hatukuwa na mawasiliano , nikamkuta ana mtoto wa kike ana miezi 7(kwa mujibu wa maelezo yake) na Alikuwa kapauka mno, ile rangi ya biscuits haipo Tena, kavaa mgauni mkubwa sijui ndio wanaita madela, ziwa linaning'inia tu huko hana habari !! nikampa hongera kea kupata mtoto, akanikaribisha kwa aibu sana, full kujistukia akawa Hana amani kabisa, Mara anajiweka busy lakini wapi !

Nilienda na mshikaji wangu tukaagiza vinywaji akatuletea, tukanywa tukasepa, maana hata jamaa yangu aliniambia huyu Hana amani Bora tuondoke tu,,, akaniomba namba nikampa !

Yeye ndiye alianza kunitafuta maana sikuchukua namba zake, tukachati kidogo akaniomba niende kwake Tena lakini nikiwa peke yangu ! Nikaenda kesho kutwa yake, tukapiga story, akaanza kuongea kwa uchungu, machozi yanalenga lenga blah blah kibao, Mara nilikukosea Sana , mda huo namsikiliza tu, mwishoni nikamuambia kwa hio unasemaje ? Unataka turudiane ama ??

Akasema hpn, japo napenda ila mimi sio type yako Tena ! Akaniambia jamaa alomzalisha kamkimbia, hajui chochote kuhusu mtoto na hampi sapoti, mjini palimshinda kujigharamikia na mtoto akaona arudi kijijini ! Nikwambia poa, akawa kama ana shauku ya kuniambia Jambo lakini anaogopa, nikamuaga nikaondoka !!

Likizo ikaisha nikarudi job, akawa ananitafuta Sana, nikawa simpi chansi ya kujenga ukaribu nae,,, Mara ananiomba hela, siku akanambia anaomba nimlipie bili ya maziwa ya mtoto 18000, means sh 600 per day kwa mda wa mwezi ! Nikamtumia, Mara nataka hiki Nampa, mtoto anaumwa Nampa helA!

Nikaja kukata mawasiliano nae na kumblock , anatafuta namba mpya ananicheki ! Siku nikampa mchumba wangu akaongea nae akamtukana pia akamwambia usimzoee mume wangu,,,, akaja kutuma msg Mara ooh unaringa umefanikiwa, maisha Ni haya haya na kelele nyingi, nikamjibu simpo tu ulichezea shilingi kwenye tundu la choo, nataka nimkomoe

Kuna mdogo ake yupo chuo,nataka nikatafune nishaseti mipango na siku ya kuja kwangu tumeshapanga! nitamtumia nauli aje nikae nae Kama wiki alafu ndio arudi ,pia nitajitahidi dada mtu ajue ili akili imkae sawa, kanisumbua Sana huyu mshenzi

Funzo kwa vijana ambao hamjaingia kwenye ndoa na mlioko vyuoni ukipendwa pendeka, hata Kama humpendi mwenzio usimuonyeshe dharau !
 
Kiongozi
Punguza Jazba Na Visa Kwenye Haya Maisha
Kama Nafsi Yako Inakutuma Kumsaidia Fanya Hivyo
IwapoUna Nia Ya Kutomsaidia Achana Naye!!

Unakosea Kumpa Simu Mchumba Wako Amtukane
Kumbuka Mliongea Akakuomba Msamaha Kuhusu Yaliyotokea. Usimkomoe Maana Ndiyo Kapoteza Uelekeo
Kutmbea Na Mdogo Wake Ni Unfair. Kuwa Muungwana
Atajuta Zaidi
 
Sioni utofauti wa tabia ya dharau kati yako na huyo x wako,utofauti ni muda tu,yeye alifanya mwanzo na wewe unafanya sasa,Wanaume hatuko hivyo,kama unamsaidia msaidie tu na malipo yako utayapata hapa hapa Duniani na kesho kwa Mungu,kumbuka unamsaidia mtoto ambaye hana Baba,huwezi jua huyo mtoto atakuja kua nani na atakusaidia vipi wakati wewe umri utakua umeshakwenda,

Unampa mkeo simu amtukane halafu unataka kutoka na mdogo wa x wako eti umkomeshe x wako! hapo huoni kua unamsaliti Mkeo? huoni kua unamshushia hadhi yake kama x wako akijua?

Maisha ni kama Gwaride kua muangalifu sana,Mungu anaweza kumuinua huyo x wako kisha akakushusha wewe,kama aliomba msamaha kulikua na ulazima gani wakumpa simu mkeo amtukane? yeye hakuomba kurudiana bali aliomba msaada,ulikua na uhuru wakumsaidia au kutomsaidia,msaada hua hautangazwi,narudia tena,Kua muangalifu sana na haya maisha,sio lazima kibaya ukilipe kwa ubaya.
 
Umachofanya sio sawa hata kidogo. Wewe msaidie bila kumkomoa. Haya ni maisha tu huwezi jua kesho utakuwaje. Usishangae huko mbeleni ukaja kuchakaa kuliko alivyo sasa na yeye akaja kufanikiwa zaidi yako. Hii ni dumia na maisha yanageuka wakati wowote bro!!
 
Aliniringia Sana kibao kimemgeuka
 
you sound like, you are uncivilized, elimu yako haijakusaidia sana. kama mmeachana sahau, huna sababu ya kulipiza kisasi, na hauna sababu ya kufurahia urofa alionao, you dont know what 2moro will bring
Nilimsaidia kwa Hali na Mali lakini akanioma lofa ,,now Mambo yamejipa anajileta
 
Sioni utofauti wa tabia ya dharau kati yako na huyo x wako,utofauti ni muda tu,yeye alifanya mwanzo na wewe unafanya sasa,Wanaume hatuko hivyo,kama unamsaidia msaidie tu na malipo yako utayapata hapa hapa Duniani na kesho kwa Mungu,kumbuka unamsaidia mtoto ambaye hana Baba,huwezi jua huyo mtoto atakuja kua nani na atakusaidia vipi wakati wewe umri utakua umeshakwenda,

Unampa mkeo simu amtukane halafu unataka kutoka na mdogo wa x wako eti umkomeshe x wako! hapo huoni kua unamsaliti Mkeo? huoni kua unamshushia hadhi yake kama x wako akijua?

Maisha ni kama Gwaride kua muangalifu sana,Mungu anaweza kumuinua huyo x wako kisha akakushusha wewe,kama aliomba msamaha kulikua na ulazima gani wakumpa simu mkeo amtukane? yeye hakuomba kurudiana bali aliomba msaada,ulikua na uhuru wakumsaidia au kutomsaidia,msaada hua hautangazwi,narudia tena,Kua muangalifu sana na haya maisha,sio lazima kibaya ukilipe kwa ubaya.
Ni mengi alinifanyia sijayaeleza,,,
 
Umachofanya sio sawa hata kidogo. Wewe msaidie bila kumkomoa. Haya ni maisha tu huwezi jua kesho utakuwaje. Usishangae huko mbeleni ukaja kuchakaa kuliko alivyo sasa na yeye akaja kufanikiwa zaidi yako. Hii ni dumia na maisha yanageuka wakati wowote bro!!
Mkuu hizi jinsia za "ke" Zina dharau Sana hasa pale anapogundua anakuzidi kitu mfano kipato,,, akigundua unampenda pia utanyanyasika sana
 
Mkuu samehe tu mi pia nimekutana na scenario kama yako ila nilisha samehe na huyo x alienisumbua kipindi ndo naingia chuo amebaki tu kuwa rafiki wa mbali ambae kama ana msala huwa na support mana amenifanyia mengi pia mazuri wakati tupo kwenye mahusiano amenifunza mengi na wala sijaona sababu ya kumlipa kisasi yeye ndio alikuwa anaona aibu na kujishtukia ila now ame relax, We are from the same village najua kuna leo na kesho hujui nani atakuzika punguza visasi kama hutaki kumsaidia ni bora usimpe nafasi hata ya chatting kuliko kuendelea kumuumiza ivo just mute na yeye atacool tu
 
Back
Top Bottom