Yule dada wa kumfumania dada yake na mumewe kanywa sumu

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MWANAMKE anayetambulika kwa jina moja la Fatuma amelazimika kunywa sumu kwa aibu baada ya dada yake kumtamkia kuwa anaujauzito aliopewa na mume wake.
Mwanamke huyo ni ili habari iliyochapishwa wiki mbili zilizopita katika mtandao huu aliyeweza kumfumania mume wake na dada yake chumbani kwake.
mtandao huu ulipata habari y a kunywa sumu kwa mwanamke huyo jana majira ya usiku na asubuhi hii ilifika nyumbani kwa mwanamke huyo na kukuta tayari alishakimbizwa zahanati kwa msaada zaidi

Imedaiwa kuwa mwanamke huyo juzi katika sikukuu ya Muungano dada yake ambaye alimfumania na mume wake wakati alipokwenda safari ya kumsalimia mama yake alimfata mdogo wake na kumuambia kuwa amsaidie kutafuta daktari ili aweze kutoa ujauzito aliokuwa nao

Imedaiwa kuwa mdogo wake huyo alijaribu kumuuliza ni kwanini autoa ndipo dada huyo alipoanza kulia na kumuomba radhi kwa mara nyingine na kumueleza alipewa na shemeji yake ambaye ni mume wa mwanamke huyo

Ndipo mwanamke huyo alianza kilio kwa mara nyingine na kwenda kwa shangazi yake aishio karibu naye kumueleza tukio hilo na kudaiwa majira ya saa moja usiku Aprili 26 alitafuta sumu ya kuulia panya bila wana familia kujua na alikoroga na kunywa
Hata hivyo imedaiwa kuwa dakika chache baadae alikutwa kitandani akiwa hoi na hatua za awali za kutoa povu zilianza kujitokeza na kudaiwa kukimbizwa hospitali

Hadi leo asubuhi mwanamke huyo anaendelea na matibabu katika zahanati moja ya karibu na maeneno hayo
Awali mwanamke huyo alimfumani mume wake na dada yake na aliweza kuacha nyumba hiyo na kwenda kwa shangazi yake lakini baadae maongezi ya kifamilia yalifanyika na kumalizika na kusameheana kwa pande zote mbili ana alirudi nyumban I kwake bila wanafamilia kutotambua kwamba alipewa ujauzito na yeye mwenye alikuwa hafahamu

Ndipo juzi jambo hilo lilijitokeza baada ya dada yake kujigundua kuwa mjamzito na kumfata mdogo wake wasaidiane kutoa ujauzito huo bila wanandugu kujua

Nifahamishe itaendelea kuwajuza kitakachoendelea kuhusiana na mtafaruku huu wa kifamilia
 
Huyo punguwani wa akili na kama una namba zake wapatie jeshi la polisi wamshugulikie kwani mimba nini ..na uhai..demn aache ujinga yeye cha kufanya kama na huyo dadake ana mume abadislishane wawe draw watu tunatafuta dawa za sumu ya panya atuzioni kumbe wamezificha kujinywea wakati wa majaribu....fatty noma bana mbona hivyo
 
naona ameogopa alipoambiwa juu ya mimba ila wanawake always wana hasira za haraka sana hii ishu ilikua sio ya kujiua!
Huyo punguwani wa akili na kama una namba zake wapatie jeshi la polisi wamshugulikie kwani mimba nini ..na uhai..demn aache ujinga yeye cha kufanya kama na huyo dadake ana mume abadislishane wawe draw watu tunatafuta dawa za sumu ya panya atuzioni kumbe wamezificha kujinywea wakati wa majaribu....fatty noma bana mbona hivyo
 
sanguinistic kind of character.........(ten second decision making)
 
Duh haya ndio yale yasiyovumilika mweee! hawa ndugu zetu tunawapenda lakini.....?
 
Ohh masikini, namuonea huruma sana ila uamuzi alichukua sio sahihi. Pole zake nyingi sana.
 
Halafu angekufa huyo dada mtu asingetoa mimba, angeenda kuolewa na huyo mume. kaazi kweli kweli. Si aachike tu, ya nn kujitoa uhai bana...
 
infidelity is an act of murder. Waweza kuua au kujiua aisee. Achana kabisa na ili neno "love"
 
Sisi kama spectators tutakuja na theory zote. Kwa nini hakufikiria?, mjinga, angedai talaka etc. Ila jibu analo mwenyewe. Na ukitaka kujua uzuri wa ngoma ingie ucheze.
 
Halafu akipata nafuu mume wake na dada yake wanaenda kumjulia hali! Wauaji wakubwa. Kama halijakukuta huwezi jua ametoa wapi guts za kunywa sumu. Huyo dada yake amemtonesha kidonda. Asali sana Mungu atamvusha salama.
 
PHP:
Duh haya ndio yale yasiyovumilika mweee! hawa ndugu zetu tunawapenda lakini.....?

Dawa ni yeye kuachia ngazi......na kuanza maish amapya mbali na hao wapenzi wapya..lakini alichukua hatua za haraka haraka bila ya kutafuta ukweli...anajuaje kama aliyomweleza ni ukweli?
 
PHP:
 		 		 		 		[B] 			[IMG]https://www.jamiiforums.com/images/icons/icon1.png[/IMG] Re: Yule dada wa kumfumania dada yake na mumewe kanywa sumu 		[/B]

 		 				 				 		 			 				 					Halafu akipata nafuu mume wake na dada yake wanaenda kumjulia hali!  Wauaji wakubwa. Kama halijakukuta huwezi jua ametoa wapi guts za kunywa  sumu. Huyo dada yake amemtonesha kidonda. Asali sana Mungu atamvusha  salama.

Tususingizie watu kuua.hivi ni nani kamtuma aone mumewew anathamani kuliko uhai wake? Huo si uendawazimu wajamani?
 
Lesson numero uno: Usitembee na mme wa mtu.
Lesson numero duo:Wivu waweza ua.
 
Back
Top Bottom