Yule binti hamnazo akakicharaza ya kipare na kuniharibia dili…!

Yule binti hamnazo akakicharaza ya kipare na kuniharibia dili…!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,443
DSCN2543.JPG


Nilikuwa nimekula pozi katika viunga vya Ccoco Beach......


Mimi ni suriama wa makabila matatu, yaani Mmasai, Mpare na Mnyamwezi, mnaweza kushangaa lakini nitawafafanulieni. Baba yangu anatokana na makabila mawili, yaani baba yake ni mmasai na mama yake ni Mpare na mama yangu ametokana na kabila la Wanyamwezi.

Nimezaliwa upareni katika kijiji cha Kirinjiko kilichopo wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, nilisimuliwa kwamba babu yangu mzaa mama ni miongoni mwa Wanyamwezi waliochukuliwa Manamba na kuletwa mkoani Tanga kulima mkonge, hao mababu zangu wa Kinyamwezi walizaana na kutawanyika katika maeneno ya upareni katika vijiji vilivyokuwa vikilimwa mkonge kuanzia Mombo mpaka same.

Baba yangu alizaliwa na kulelewa upareni kwa wajomba zake ambao walikuwa ni wafugaji maarufu katika ukanda huo wa Kirinjiko, kwa hiyo mila anazozifata baba yangu ni za kipare ingawa kwa kabila yeye ni Mmasai. Baba alikutana na mama yangu wakati huo akiwa ni mtoza ushuru wa masoko katika vijiji vya upareni ndipo wakaoana.

Sisi wote yaani mimi na ndugu zangu tumekuzwa katika mila za kipare na hata majina yetu wote ni ya kipare, kwa mfano mimi jina langu la kipare naitwa Sengasu, na watu wengi wanaonifahamu wanashangazwa na urefu wangu kwa saabu wanaamini kwamba wapare ni wafupi lakini ni vile tu hawajui kwamba nimechukua mwili wa Kinyamwezi na urefu wa Kimasai.

Wakati nilipokuwa shule ya msingi hapo kijijini Kirinjiko, kulikuwa na binti mmoja aliyekuwa anaitwa Namsemba, huyu binti alikuwa akili zake kidogo hazimtoshi, yaani hata darasani alikuwa ni mbumbumbu kabisa, kwa hiyo tulimgeuza kama kituko kwa kumkejeli na kumtania. Lakini kwa upande wa baadhi yetu alitusitiri, kwani baada ya kubalehe tulimgeuza kama sehemu ya kujifunzia mambo ya kikubwa kwa ile staili ya niangusage ya wenyeji wa kule Iringa (Thank God Ukimwi ulikuwa bado haujashika kasi kipindi hicho), kwa hiyo kwa sisi vijana ambao damu zetu zilikuwa zinachemka kutokana na balehe ilikuwa kila ukikutana naye machungani wakati wa kuchunga Mbuzi ilikuwa kama mazingira ya yanaruhusu unajimegea kiulaini.

Naam hayo ndiyo maisha niliyokulia…………….

Baada ya kumaliza darasa la saba na kufaulu niliendelea na masomo ya sekondari katika shule moja iliyoko kijijini Mbaga huko milimani upareni na huo ukawa ndiyo mwanzo wa kuondoka pale Kijijini. Nilipomaliza kidato cha nne na kuangukia pua nilikuja jijini Dar mwaka 1988 na kufikia kwa kaka yangu maeneo ya Mwananyamala Kwa Kopa. Nilipofika Dar nilibadilisha jina langu kwa sababu niliona ni kama la kishamba nikawa najiita Senga badala ya Sengasu na hivyo vijana wengi pale mtaani wakadhani mimi ni Mchaga.

Nilianza kujifunza ubitozi wakati huo, na maeneo yangu ya kutembelea yalikuwa ni maeneo ya Victoria na Mikocheni maeneo ilipo Hospitali ya Dk. Kairuki. Nilijipenyeza katika maeneno hayo na kufanikiwa kupata marafiki kadhaa, mmojawapo akiwa ni mdau mkuu wa Jamii Forum (naomba nisimtaje).

Kaka zangu wawili walikuwa ni madereva wa malori ya masafa marefu na huyu kaka mkubwa niliyekuwa nikiishi naye yeye alikuwa ni mtumishi serikalini. Hawa kaka zangu wawili madereva ndiyo walioniharibu, kwani walikuwa kila wakirudi kutoka safarini nje ya nchi, wananikatia vijisenti vya kusumbua mtaani.

Nilikuwa najitwalia vibinti vya Kizaramo na Kimakonde pale mtaani nitakavyo kwa sababu mfukoni nilikuwa niko vizuri wakati huo. Hata hivyo niliona nibadili mikakati na kuanza kuwania mabinti wa geti kali, hivyo mawindo yangu yakahamia katika viunga vya Victoria na Mikocheni.

Nakumbuka siku moja nilikwenda Beach maeneo ya Oysterbay, siku hizi wanapaita Coco Beach, nilikuwa nimebeba magazeti yangu kadhaa ya kizungu, ambayo niliyapata kwa marafiki zangu wanaoishi maeneo hayo ya Mikocheni. Nilikuwa nimekaa ufukweni na mawani yangu miyeusi, nikijifanya nimekula pozi huku nikijisomea magazeti yangu kiuonga na kweli, kumbe niko katika harakati zangu za kuwinda mabinti wa geti kali. Mara akapita binti mmoja mrembo wa sura na umbo hatari, akanisalimia, nikajua yes, ndege mnana kanasa kwenye ulimbo, nikaona nichangamkie tenda.

Alikuwa ni binti mwenye weusi wa Kiafrika yaani rangi ya chocolate, mrefu kiasi mwenye umbo namba nane na miguu ya bia, makalio yake yalikuwa ni yale ya duara, vijana wa mjini wanaita kijungu, na yalikuwa ni malaini ambapo akitembea yanatepeta yakifuata miondoko yake ya madaha.

Aliniomba mojawapo ya yale magazeti ya Kizungu niliyokuwa nayo ili apitishe macho, sikusita kumpa kwani niliona ile ni nafasi adhimu ambayo nikiipoteza nitajijutia.

Wakati anapitishia macho hilo gazeti niliona ile ni fursa nzuri kwangu kurusha nyavu zangu, nilianzisha mazungumzo kwa lugha ya Kiingereza kwani na miye si haba nilikuwa nakijua cha kuombea maji. Nikajitambulisha kwake kwa jina la uongo la Tionge Zgambo mwenyeji wa mjini Lusaka nchini Zambia na ni nilimdanganya kwamba baba yangu ni afisa wa balozi katika ubalozi wa Zambia hapa nchini.

Nilimwambia nasoma Chuo kikuu mlimani mwaka wa kwanza na ninasomea mambo ya saikolojia. Yule binti alionekana kunikubali haswa. Aliniambia kwamba yeye ndiyo kamaliza kidato cha nne na anasubiri majibu kama akifaulu aendelee na masomo ya kidato cha tano.

Aliniambia kwamba yeye anaishi na wazazi wake maeneno ya Mikocheni na ni mwenyeji wa Mkoa wa Songea, yaani ni Mngoni. Alijitambulisha kwangu kwa jina la Agatha Nyoni na akaniambia kwamba baba yake ni afisa katika wizara ya mambo ya nchi za nje na mama yake ni mfanyabiashara anayesafiri mara kwa mara nje ya nchi.

Nilimuomba namba ya simu ya nyumbani kwao ili tuwasiliane (kumbukeni wakati huo hapakuwa na hizi simu za mkononi) lakini nilimwambia kwamba sitampa namba ya simu ya nyumbani kwetu kwa sababu baba yangu alinikataza kutoa namba ya simu ya nyumbani hovyo kwa kuhofia usalama kutokana na nchi yetu ya Zambia kusaidia wapigania uhuru walioko kusini mwa Afrika. Sikutaka niharibu dili langu la kujifanya mtoto wa kishua, nilijua kwa kupitia marafiki zangu wa Mikocheni ningeweza kupata simu za bure niwe nampigia na kupanga mipango yetu ya kungonoka.

Alinipa namba ya simu ya nyumbani kwao na kuanzia siku hiyo nikawa nampigia kupitia simu za nyumbani kwa marafiki zangu na kupiga naye stori. Ilikuwa kila ninapomtega twende zetu Geto kwa washikaji zangu ili tukale tunda, mitego yangu inapachuka, akawa ananizungusha tu kila siku, lakini sikukata tamaa, nilijipa moyo nikiamini kwamba kwa kawaida ndege wajanja hunasaga kwenye matundu mabovu, niliamini tu kwamba siku moja atakuja kunasa nijimegee kibingwa na kulifaidi toto shatashata la Kingoni.

Basi bwana, uhusiano wetu ukawa ni ule wa tega nikutege na mtoto alionekana kama vile muda wowote anaweza kuingia kingi na sikukata tamaa. Siku moja mtoto alinipa mualiko wa surprise nimtembelee nyumbani kwao ili akanitambulishe kwa mama yake, alinimbia kwamba baba yake hayupo nchini amesafiri na mheshimiwa raisi kwenda nchi za Ulaya kwa ziara ya kikazi, hivyo alinihakikishia kwamba mambo yatakuwa shwari kwa sababu yeye ni mtoto pekee wa kike katika familia yao ya watoto wanne na ni wa kwanza kuzaliwa hivyo mama yake anampenda kama mboni ya jichao lake, hivyo hawezi kuleta noma.

Kusikia hivyo kidume nikajipa moyo nikakubali mualiko. Nikiwa kama mtoto wa Afisa wa Ubalozi wa Zambia nililazimika kuazima pamba kwa washikaji zangu wa Uzunguni ili nifanane na mtoto wa kishua.

Nakumbuka ilikuwa ni siku ya Ijumaa majira ya jioni ndipo nilipotimba maguu kwa mtoto wa kishua nikiwa nimependeza hasa, nilikaribishwa kwenye kibaraza (wenyewe wanaita Lonji) ambapo kulikuwa na makochi mazuri ya ulaya na meza moja nzuri sana iliyonakshiwa vizuri kwa nakshi za kisanii. Nilikaa kwa adabu zote.

Yule mama alionekana kuwa ni msomi hasa na anaijua jiografia vizuri sana, kama nisingekuwa nimepiga vidato angeniumbua. Alianza kunidadisi kuhusu baba yangu nikamdanganya kwamba baba yangu anaitwa Mwanzil Zgambo na ni afisa wa balozi katika ubalozi wa Zambia hapa nchini. (Ukitaka kudanganya lazima kuwe na uhalisia, nilishayafanyia utafiti majina ya Kizambia mpaka nikayajua).

Wakati yule mama anaendelea kunidadisi yule binti alimuita mtumishi wao ili aje kutuletea vinywaji. Yule mtumishi alipofika pale alionekana kunitizama sana, na nilipomtazama kwa jicho la wizi nilishtuka sana na mwili wote ulikufa ganzi.

Wakati nikiendelea kujifanya niko bize nikiongea na mama wa binti, yule mtumishi alinisogelea na kuanza kunisalimia kwa lugha ya kipare na alionekana kufurahi sana baada ya kuniona.

Nikajifanya kushangaa na sikujibu kitu, lakini wapi yule binti alikomaa kunisemesha kwa lugha ya kipare akiniambia nisijifanye kumchunia wakati tunatoka kijiji kimoja.

Yule mama wa binti alimuuliza yule mtumishi kama ananifahamu na siyo kwamba amenifananisha, Aliniangalia kwa makini na kusema……

“Mama siyo kwamba namfananisha, huyu namfahamu sana, anaitwa Sengasu tumetoka kijiji kimoja”

Hebu kisieni mnadhani huyo mtumishi ni nani?

Hakuwa mwingine bali ni yule binti hamnazo wa kijijini niliyesoma naye shule ya msingi kule kijijini Kirinjiko aitwaye Namsemba, ambaye tulikuwa tumemgeuza asusa wa kujifunzia mambo ya kikubwa enzi zetu tulipokuwa vijana barubaru.

Yule binti wa Kingoni na mama yake walishikwa na butwaa, na yule mama akaniuliza kama baba yangu ni Afisa wa Ubalozi kwenye ubalozi wa Zambia hapa nchini au ni Manamba wa Kiwemba mkata mkonge mhamiaji wa huko upareni. Sikuwa na jibu na nilibaki kimya kama niliyemwagiwa maji.

Mnadhani ni kitu gani kilitokea baada ya hapo…….

Acheni umbea………..!

Kusema kweli kuanzia siku hiyo nilibadilika kabisa na nikawa mtu tofauti, yaani siku hizi mtu akiniuliza naitwa nani namwambia wazi kwamba naitwa Sengasu Kiruti Rubagwa mzaliwa wa Kirinjiko huko Upareni.
 
Dah mkuu stori yako nimeipenda sana tena sana ila ungemalizia ili tujue kama ulifanikiwa kula tunda au lah . Otherwise thanx alot.
 
Hivi kweli ulifika kunywa juice uliyoandaliwa? pole sana aisee!!!

ungebadili tu lugha kwenda kikameruni, mambo yangeenda sawa kama utelezi kwenye gentle slope!!!
 
Yani kipoozeo chako cha zamani ndo kinakurushia ndege?

HAhaha LMAO
 
yule mama akaniuliza kama baba yangu ni Afisa wa Ubalozi kwenye ubalozi wa Zambia hapa nchini au ni Manamba wa Kiwemba mkata mkonge mhamiaji wa huko upareni hahahahaha nampongeza sana huyo mama......[I said:
shem piga mzigo usiogope,nikaanza kulia kama nyau,tehethe[/I]
 
Thengathu,washinjiadhe?
Huyo mwathu mwambie ananidai kwa kukuumbua mkataa asili yako ............lol
 
Mtambuzi hatimaye binti wa kipare kakuharibia pozi na ukajikuta unanasa kwenye tundu lako mwenyewe
 
Ningetoka mbio asipate fursa ya kunijadili mbele ya mama mkwe.... Huyu binti ni noma
 
pole ya nini sasa?..mie nimpe hongera
hongera Mtambuzi kwa kusaidiwa kufupisha uongo wako..who knows,pengine ungekuja jifunza kutapeli kwa gia ya mtoto wa balozi...ashukuriwe binti hamnazo..lol.....shikamooo
Badala ya kumpa pole.mzee wa watu

Pole Mtambuzi kwa masaibu...
 
Last edited by a moderator:
So funny, Juice yenyewe hata kunywa hujanywa. Bora ungekuwa umeanza ungeigiza kupaliwa uende bafuni kumuweka sawa binti wa kipare
 
hahaaa duh hapo ilikuwa aibu kubwa sana.............

mtoto wa afisa ubalozi lol
 
Back
Top Bottom