Bundewe
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 400
- 141
Ni Takriban miaka mitatu imepita tangu mwanasheria na mwanaharakati Kainerugaba Msemakweli atoe Kitabu chake kilichopata umaarufu wa ghafla cha MAFISADI WA ELIMU VOL. 1 akiwataja vigogo mbalimbali serikalini kuwa ni vihiyo waliofoji vyeti au kudanganya elimu walizonazo. Pia aliahidi ku release vol. 2 baada ya muda mfupi.
Baada ya vol. 1 vigogo kadhaa waliotajwa akiwemo mbunge wa Segerea Mhe. Makongoro Mahanga walifungua kesi kortini kudai fidia ya kuchafuliwa jina. Hata hivyo mpaka sasa kimya kimetawala kuhusiana na mwenendo wa kesi zile au alipo mwanaharakati yule na harakati zake. Kiasi cha kujiuliza yupo kweli au naye ameshanyamazishwa. Iko wapi vol. 2 aliyoahidi? Au ilikua ni mbinu nyingine ya serikali kutuondoa kwenye mjadala mzito wa kitaifa?
https://www.jamiiforums.com/habari-...-kitabu-cha-mafisadi-wa-elimu-nakipataje.html