Yuko wapi mzee huyu, wanaJF??

Rhobi1961

JF-Expert Member
Nov 4, 2015
890
1,000
Habari wakuu!

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu, huyu mzee anaitwa Fabian samo maarufu kama (mzee samo) leo nimemkumbuka huyu mzee, mwaka 2004 aliwahi kunisaidia nikiwa na mgonjwa wangu pale Mwanza Airport siku hiyo huyu mzee ndo alikuwa kama Mungu wangu,. Aliwahi kunisaidia kiasi cha 240000tsh nikawa nimeachwa na ndege harafu mgonjwa alikuwa na hali mbaya sana huyu akayabeba matatizo yangu kwa siku hiyo mpaka napanda ndege usiku mida ya saa 3 Mungu ambariki sana huko aliko, baada ya kurudi kutoka kwenye matibabu ya mgonjwa nilimtafuta sana huyu mzee bila mafanikio lakini watu niliowauliza kwa jina hili walisema ni mwenyezi wa huko musoma na sina mawasiliano nae kwa sababu simu nilipoteza kwenye harakati za kumuuguza mgonjwa.

Kama kuna mtu anamjua sehemu alipo anisaidie jinsi ya kumpata nataka nimpe asante yangu!!!!
 

Kaveli

JF-Expert Member
Dec 4, 2012
3,849
2,000
Duniani bado wapo wenye moyo safi. Hongera sana mkuu kwa kuwa na moyo wa shukrani. Ipo siku utampata tu huyo mzee.

-Kaveli-
 

Rhobi1961

JF-Expert Member
Nov 4, 2015
890
1,000
Laki mbili na arobaini kwa mwaka 2004 sio ndogo asee, Mzee alikusaidia sana

Hongera sana kukumbuka wema, wengi huwa hatujali tukishasaidiwa
Mkuu nafikiri siku ile nisingepata msaada kama ule leo ningekuwa naongea mengine kabisa!!
 

karume kenge

JF-Expert Member
Mar 9, 2016
573
500
Mungu atakujaalia utamuona japo wema huwezi kuurudisha kwa thamani yake ile ile hata ukikutana nae leo u kampa ml10 haina thamani kama ile laki 2 alokupa kipindi unashida mkuu
 

Nyaka-One

JF-Expert Member
Oct 27, 2013
3,437
2,000
THE incumbent Chairman of the Football Association of Mara (FAM), Fabian Samo managed to retain his post during the body's general elections recently.


Tanzania Football Federation (TFF), Information Officer Boniface Wambura said on Thursday that the election was conducted in Rorya district by FAM election committee last Sunday under the supervision of the federation's election committee.

Mkuu nimeiona hii mahali. Hiyo ilikuwa ni November, 2011. Anzia hapo.
 

Nyaka-One

JF-Expert Member
Oct 27, 2013
3,437
2,000
Na July, 2012 kukawa na habari hii kumhusu huyo mzee:

Rais wa shirikisho la soka hapa Nchini (TFF) Leodiger Tenga ameongoza maelfu ya waombolezaji katika mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha soka Mkoani Mara (FAM) na mjumbe wa kamati ndogo ya mahesabu ya (TFF) Fabian Samo yaliyofanyika nyumbani kwake maeneo ya Nyakato katika Manispaa ya Musoma.

Samahani najaribu kuweka link ila inanigomea.
 

Rhobi1961

JF-Expert Member
Nov 4, 2015
890
1,000
Na July, 2012 kukawa na habari hii kumhusu huyo mzee:

Rais wa shirikisho la soka hapa Nchini (TFF) Leodiger Tenga ameongoza maelfu ya waombolezaji katika mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha soka Mkoani Mara (FAM) na mjumbe wa kamati ndogo ya mahesabu ya (TFF) Fabian Samo yaliyofanyika nyumbani kwake maeneo ya Nyakato katika Manispaa ya Musoma.

Samahani najaribu kuweka link ila inanigomea.
Mkuu ulichoandika hapa kina ukweli wowote!!!!??
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom