Yuko wapi mtangazaji nguli Dotto Emmanuel Bulendu?

Yuko wapi mtangazaji nguli Dotto Emmanuel Bulendu?

washa

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2007
Posts
626
Reaction score
370
Kwa muda sasa Mtangazaji huyu mweledi na makini hajaonekana katika vipindi vyake alivyokuwa akiviongoza kwa ustadi wa hali ya juu huku akibainisha upeo wake mpana katika masuala kadhaa.
Kuna mdau yeyote mwenye taarifa za bwana huyu?, Star TV imepwaya sana; vipindi vyake vya jumamosi asubuhi na jumatatu usiku vimetoweka!...
 
Ni kweli hajaonekana siku nyingi. Kipindi chake cha Jicho letu ndani ya habari alikuwa akikiendesha vizuri sana. Hata hivyo siku hizi Star TV na yenyewe imekuwa kama TBC, kwa hiyo imepoteza sana mvuto. Hata akiondoka sawa tu..
 
Atakuwa amerudi kwenye kazi yake ya Ualimu
 
Minamtakia safari njema ndg doto blendu maana huku star sasa hakufai.jiurize pacha wake siku izi yuko bbc anakula bata bila shida!
 
Kwa muda sasa Mtangazaji huyu mweledi na makini hajaonekana katika vipindi vyake alivyokuwa akiviongoza kwa ustadi wa hali ya juu huku akibainisha upeo wake mpana katika masuala kadhaa.
Kuna mdau yeyote mwenye taarifa za bwana huyu?, Star TV imepwaya sana; vipindi vyake vya jumamosi asubuhi na jumatatu usiku vimetoweka!...
Doto Bulendu ni Kichwa sana na sijui walimpata wapi maana watu kama wale hupatikana BBC,CNN,VOA sasa hawa makanjanja wa Star Tv sijui walimnasa wapi yule jamaa..Yule ni zaidi ya Mwanahabari
 
doto bulendu ni kichwa sana na sijui walimpata wapi maana watu kama wale hupatikana bbc,cnn,voa sasa hawa makanjanja wa star tv sijui walimnasa wapi yule jamaa..yule ni zaidi ya mwanahabari

hivi unadhani mtu unaanzia kufanya kazi bbc tuu kabla ujapitia kwenye vyombo vidogo vidogo kama vya kwetu??? Star tv ndio inaweza kumkuza haive na aweze kuonekana kwenye vyombo vikubwa kama ulivyovitaja, hata hawa watangazaji walioko bbc wamepitia huko, na kwa taarifa yako bulembo anawakilisha sauti ya ujerumani hapa tz, kama uamini fungua radio free saa saba mchana utamsikia
 
Minamtakia safari njema ndg doto blendu maana huku star sasa hakufai.jiurize pacha wake siku izi yuko bbc anakula bata bila shida!

FaizaFoxy uko wapi ? Pita hapa kuna mteja wako! Kiswahili kinanajisiwa umeuchana tu ! "Jiriuze" na wewe siku "izi" "blendu" yuko wapi !
 
Last edited by a moderator:
Doto Bulendu ni Kichwa sana na sijui walimpata wapi maana watu kama wale hupatikana BBC,CNN,VOA sasa hawa makanjanja wa Star Tv sijui walimnasa wapi yule jamaa..Yule ni zaidi ya Mwanahabari

Alipatikana Chuo Kikuu Pendwa Na Kizuri Tanzania, Afrika Mashariki, Sub Saharan Africa, Africa Na Duniani Kote Cha Saint Augustine University Of Tanzania ( SAUT ). Vichwa Venye Akili Na Upeo Mkubwa Kama Hivyo HUPIKWA na KUTENGENEZWA Hapo.......Akhsante SAUT Kwa Kutufanya TUTAMBE MITAANI HUMU Kwa Kujua Kufanya Vizuri Sana TAFAKURI TUNDUIZI ( Critical Thinking ) Na Kujua Kujenga Hoja Za Msingi Na Kuzisimamia. Dotto Bulendu Ni Balozi Wetu Mzuri Sana Wana SAUT Wote Achilia Mbali Wale Wengine Wote Waliopo ktk Taasisi Mbalimbali Ambao Pia Wapo Very Competent. '' We Build The City Of God " and I am Proud Of SAUT, I Love SAUT and Long Live SAUT.
 
Mkuu mussolin umetupa habari hii kwa kifupi sana, hebu funguka zaidi...
 
Yahaya alifanya kazi nzuri sana na Dotto ktk vipindi vyao star tv, na ninajua kuwa Yahaya yumo jamvini humu; unaweza kuwa na habari za Dotto utujuze?
 
Huyu jamaa kukosekana kwenye kipindi cha Jicho letu ndani ya habari kumenifanya nione jumamosi asubuhi tatizo kwangu.

Hiki kipindi kilinifanya kila jumamosi kuamka mapema kuwahi ilinipate habari na uchambuzi motomoto kwa muongozo na

umahili wa huyu Nguli wa Habari. Doto Bulendu nijabari la habari.
 
Yahaya alifanya kazi nzuri sana na Dotto ktk vipindi vyao star tv, na ninajua kuwa Yahaya yumo jamvini humu; unaweza kuwa na habari za Dotto utujuze?

Mara ya mwisho Yayha Mohammed alikuwa Azam Media kama sikosei. Sijui bado yupo huko au amehama?!
 
Yahaya alifanya kazi nzuri sana na Dotto ktk vipindi vyao star tv, na ninajua kuwa Yahaya yumo jamvini humu; unaweza kuwa na habari za Dotto utujuze?

Kiswahili kinawatambua mapacha wawili kwa jina la DOTO na KURWA...Hivyo, mtangazaji huyo haitwi DOTTO bali DOTO...Acha kuharibu majina ya watu....

Lugha ya Kiswahili haitumii double consonants...Punguzeni ulimbukeni wa kutawaliwa kifikra na wazungu, majina ya kibantu yaandikeni kibantu..

Tafakari...
 
Fani moja, lkn unakuta mmoja au wawili kama vile wame specialize katika kipindi fulani, sa unakuta eti siku hizi mwanafunzi kamote, anaonekana hakiwezi kabisa kipindi hicho cha jmosi ata mkongwe huyu mzee mpendu akiwezi kama doto.
 
Back
Top Bottom