Dotto Bulendu: Tathmini yangu juu ya mahojiano kati ya BBC na Rais Samia Suluhu

blance86

JF-Expert Member
Aug 31, 2016
2,081
5,450
Tathmini yangu ya juu ya mahojiano kati ya BBC Na Rais Samia Suluhu Hassan.

Na Dotto Bulendu (MwanaPuge).Nikiandika kutoka kijijini Puge.
@@@@@@

BBC wamefanikiwa kuongeza umaarufu wao Kwa Siku ya jana Kwa Maana ya Idadi ya watu wanaowasikiliza na kuwatazama kupitia Vyombo vyao vya Redio,TV na Mitandao ya kijamii,kwani kwenye kujenga umaarufu na kuaminika Kwa chombo na Mwandishi, tunaambiwa Moja ya mbinu ni kuhakikisha unawafikia watu wenye ushawishi Mkubwa ama nafasi kubwa Kwenye jamii, na ndivyo akina Tim Sebastian, Christian Amanpour, Steven Sucker, Tido Mhando n.k walivyofanya Kwa kulenga zaidi nyakati zao kuwahoji watu wakubwa.

BBC wamefanikiwa kujua hitaji Na takwa la wasikilizaji Na watazamaji wao Kwa wakati huu(Audience needs and wants),jamii ya watanzania Kwa muda Sasa wamekuwa Na hamu ya kuona chombo ama Mwandishi anamhoji Rais wa nchi na hii Ni kutokana Na mambo yanayoendelea nchini.BBC wamekuwa wa kwanza kumpata Rais Samia,kimkakati wamefanikiwa mbele ya Vyombo vya ndani vikiwemo Vyombo vya Chama Na Serikali.

BBC wamefanikiwa kukidhi matarajio ya watazamaji,wasikilizaji Na wafuatiliaji wa Vyombo vyao(Audience expectation),Kwa mahojiano yaligusa maeneo yote ambayo mtazamaji Na msikilizaji alitarajia aulizwe Rais Samia, mfano, Tozo,Demokrasia,Corona, Sakata la Mbowe na Suala la Watanzania wanaoishi nje.

Sehemu ambayo BBC walipata changamoto ni kwenye kumridhisha msikilizaji/mtazamaji (Audience satisfaction).

Kwa kawaida mahojiano Kama hayo yana misingi yake Ili ufike Kule anapotaka "audience" wako Na kutoaacha maswali .

Mahojiano mazuri yanaanza Na maswali ya msingi(Basic questions),na Hapa Mwandishi ama Mtangazaji huuliza maswali yanayolenga 5W+H Kwa Maana ya What, Where, When, Why, Who and how.

Na inashauriwa kuanza interview Hivi Ili kujenga kujiamini Kwa mgeni wako asije akaamini mahojiano hayo ni vita na yanaweza kuniangusha.

Wabobezi wa mahojiano wanasema,sehemu hii hupambwa na maswali yanayotokana Na majibu(Follow up questions),Mahojiano ya BBC Bahati mbaya yalikosa "Follow up" questions"

Kwa mfano Samia aliulizwa kuhusu Sakata la Mbowe,ambalo kiufundi Samia alitakiwa alikwepe kwani lipo mahakamani.Kwenye majibu yake Samia alisema Kesi ya akina Mbowe ilianza tangu Mwaka Jana mwezi Sept Na wenzake Mbowe washahukumiwa.

Swali lilitakiwa Ni akina Nani hao?maana taarifa zilizopo Ni Kuwa katika waliokamatwa Baadhi DPP aliwafutia mashtaka,Na wengine wapo Rumande Na Bado Jamhuri haijaanza kupeleka ushahidi,hao anaosema Rais Samia Kuwa wameshahukumiwa Ni akina Nani?BBC wangemuuliza.

Samia alisema Vyama vya Siasa nimekuwa vinafanya maandamano Kwa kuchoma magari Na kuharibu mali,BBC wagemuuliza,Ni Lini Na wapi jambo hilo lilifanyika.

Eneo lingine muhimu Kwenye mahaojiano Ni kuulizwa "Packaging questions" haya Ni maswali ambayo yana nukuu ya Katiba,Sheria, Sera, Kanuni, Taratibu, matamko, takwimu, tafiti Na ripoti.

Bahati mbaya,maswali yote ya BBC hayakuwa Na rejea ya
1. Katiba
2. Sheria
3. Kanuni
4. Sera
5. Takwimu
6. Tafiti

Na hii ilimpa nafasi Rais Samia kujibu maswali kikawaida mfano Swali kuhusu Mikutano ya vyama vya siasa,Swali lilitakiwa kutengenezwa Kwa kutumia rejea Na Katiba Na sheria ya vyama Vya siasa.

BBC wangemuuliza Samia,kinachotakiwa kusubiri Kipindi cha Uchaguzi Kwa mujibu wao sheria Ni "Civic education" ama "Voters education" ?

Swali Kwa Samia kuhusu Uhuru wa Vyombo vya Habari lilitakiwa Kuwa Na rejea ya sheria ambazo zimekuwa zinalalamikiwa Na Serikali haijazitanyia marekebisho,mfano sheria ya Takwimu,Huduma za Vyombo vya Habari,makosa ya mtandao,Maidhui ya Utangazaji,Usalama wa taifa,Utangazaji,Magazeti,Magereza,Jeshi la polisi,Makosa ya adhabu n.k.

Swali kuhusu Vyombo vya Habari Kuwa huru,lilihitaji rejea ya Kwa nini Mpaka Sasa magazeti ya Mawio,Mseto Na Mwanahalisi ambayo yenyewe hayakufutiwa Usajili Na yalishinda kesi mahakamani hayajatejeshwa Na kuwekwa kapu Moja Na gazeti la Tanzania Daima ambalo lilifutiwa Usajili?

Sehemu ya Mwisho ya mahojiano ambayo ndiyo imewafanya akina Tido Mhando,Tim Sebastian,Aman Pour,Kopp,kuendelea Kuwa magwiji Kwenye mahojiano.

Na inawafanya watangazaji wa Sasa akina Mnete,Chilumba,Khelef,kuna nyakati namuona Nyanda,Yupo Nyoni wakati Fulani nilimuona Mahela Sam Ni sehemu ambayo tunasema Mwandishi ana chunguza (Probe).

Hapa maswali yote yanayoulizwa yanatakiwa kutokana Na nyaraka ulizonazo,mara nyingi utamuona Mwandishi anasema "Hii Ni ripoti ambayo inaonesha" huku akimuonesha mgeni wake Na watazamaji wake.

Wakatibiwa sakata la Escrow,aliyekuwa Mtangazaji wa Star TV Joyce Mwakalinga,alifanya Hiki,alifanya mahojiano Na Prof Tibaijuka,kila Prof alipojaribu kukataa alioneshwa ushahidi.

Eneo hili wengi huwa hatufiki tu napokuwa tunawahoji wageni wetu Na Bahati mbaya jana BBC hawakufika pia.

Mwisho wa yote kumhoji Rais tena Ikulu siyo Kazi Rais ina taratibu nyingi.Hongereni BBC.

Asubuhi njema.
 
Wanaouliza kwa nini Mbowe amekamatwa sasa na si vinginevyo wanasahau kuwa Mbowe, Lema, Meya wa zamani Ubungo Boniface walikamatwa mara baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu kutangazwa na kabla Rais hajaapishwa kwa kuchochea maandamano yasiyo na kikomo kupinga matokeo. Mambosasa alihojiwa na vituo vya ITV na TBC na kutoa madai hayo hayo ya ugaidi.
 
Mtaweza kuprove mahakamani kuwa Mbowe ni gaidi? Shame on you
 
Salimu aluwahiwa na Mama, "WEWE NI MUANDISHI WA HABARI?" hahaahhha kwisha habari yake, akapotea mazima! Sijui lile swali lililenga kumkumbusha mini Kikeke!! Dah.

Ni sawa uwe unatetea Wizi, then ghafla atokee MTU aseme "hata wewe unatetea?"
 
Lazima tuelewe mahojiano yale ni baada ya Raisi kama Taasisi kukubali kufanya mahojiano, ili akubali ni lazima aonyeshwe au aelezwe anaenda kuulizwa nini na hapo ndipo tatizo linapoanzia. Kunakuwa na editing ya maswali.

Kikeke hakuwa na uwezo wa kuuliza hayo uliyashauri sababu everything there was pre-planned, publicity stunt.
 
Nakubaliana na wewe kwanza alikuwa anatetemeka vibaya sn asije pigwa ugaidi
 
Salimu aluwahiwa na Mama, "WEWE NI MUANDISHI WA HABARI?" hahaahhha kwisha habari yake, akapotea mazima! Sijui lile swali lililenga kumkumbusha mini Kikeke!! Dah.

Ni sawa uwe unatetea Wizi, then ghafla atokee MTU aseme "hata wewe unatetea?"
Kikeke ni mtangazaji siyo mwandishi wa habari

Rais Samia alimuuliza swali muhimu sana kwa ajili ya afya ya mjadala ule!
 
Salimu aluwahiwa na Mama, "WEWE NI MUANDISHI WA HABARI?" hahaahhha kwisha habari yake, akapotea mazima! Sijui lile swali lililenga kumkumbusha mini Kikeke!! Dah.

Ni sawa uwe unatetea Wizi, then ghafla atokee MTU aseme "hata wewe unatetea?"

Lile swali lilitosha kumfanya Kikeke apoteze utulivu na kujawa hofu.

Ni kama alikua anamkumbusha kwamba yeye ni mwandishi wa habari, sio mwana siasa na ajikite kupokea anachoambiwa...kumbuka pia yule ni Rais, kuna hofu flani kufanya nae mahojiano.

Lakini kuna vitu watu wamevipata kupitia yale mahojiano.
 
Ndugu zangu tusimlaumu Sana kikeke maana Kama alivyohitimisha mleta mada kuwa Ikulu sio sehemu ambayo unaweza kuwa huru Sana katika kugonga maswali ya maana, hasa Ukizingatia Ikulu zenyewe za Africa unahoji huku umesimamiwa pembeni na jitu hata halicheki Wala nini na unajua kabisa mda wowote likipewa ruhusa ya kufanya chochote kwako linafanya bila kusita.

Naweza nikasema ile tu kupata nafasi ya kuingia hapo mjengoni inaweza kukuchanganya na kusahau maswali yote kulingana na kila kitu kinaenda kwa protocol Hadi ukaaji Sasa hapo unategemea akili zitachemka kweli!!🤔🤔🤔🤔
 
Ikulu mawasiliano haina mtu/mshauri wa Rais aliyesomea sheria?

Kabla ya mahojiano Kikeke alipaswa achambuliwe script za kumhoji Rais na kisha Rais apewe mwongozo wa baadhi ya maswali kujibu kisheria kama taasisi.

Hali iliyokuwepo,wandani wabobevu wa kauli ya Rais wangeipitia hiyo news wangemwomba BBC asiirushe kwanza.
 
Salim alikuwa anaonyesha hofu kuu

Pili yeye ni mtangazaji kwa maana kile anachotangaza mara nyingi huwa ameandaliwa

Yule Mzungu Sucker aliemuhoji Tundu Lissu alitakiwa afanye mahojiano na SSH
 
Ikulu mawasiliano haina mtu/mshauri wa Rais aliyesomea sheria?
Kabla ya mahojiano Kikeke alipaswa achambuliwe script za kumhoji Rais na kisha Rais apewe mwongozo wa baadhi ya maswali kujibu kisheria kama taasisi.
Hali iliyokuwepo,wandani wabobevu wa kauli ya Rais wangeipitia hiyo news wangemwomba BBC asiirushe kwanza.
Hapana sijui edit kwanza yani vitu vinatakiwa viende live live kama kule kwa biden
 
Tathmini yangu ya juu ya mahojiano kati ya BBC Na Rais Samia Suluhu Hassan.

Na Dotto Bulendu (MwanaPuge).Nikiandika kutoka kijijini Puge........
@@@@@@

BBC wamefanikiwa kuongeza umaarufu wao Kwa Siku ya jana Kwa Maana ya Idadi ya watu wanaowasikiliza na kuwatazama kupitia Vyombo vyao vya
"JPM tutamkumbuka" kuna mtu kasema huyu mama ni" mweupe kichwani"
 
Back
Top Bottom