Kwa hakika kuna kitu hakiko sawa! Yuko wapi
barafu mchambuzi nguli wa mambo ya anga katika dhana nzima ya vyombo vinavyoruka angani?
Huyu hakuwa mwanasiasa bali mtaaluma aliyefahamu kindakindaki elimu na maarifa ya usafiri adhimu wa anga...kupitia yeye wengi tuliweza kufaidika na elimu ya bure na ujuzi wa hali ya juu kwenye hii kaliba
Akiwa ni mzalendo mwenye uvumilivu mkubwa daima alisimama upande wa kutetea nia ya serikali kwenye dhana nzima ya kutaka kulifufua shirika letu la ndege ATCL kwa kununua ndege mpya aina ya bombadia...kamwe hakuchoka kutoa elimu ya bure kwa wakosoaji....
Kutokana na ujuzi na elimu yake hiyo kubwa ilifika wakati alikuwa rejeo popote palipokuwa na ubishi juu ya usafiri huo wa angani....na neno lake liliheshimika na kumaliza ubishi husika...kuna baadhi ya maeneo alitoa ushauri serikalini na serikali ikaufanyia kazi ushauri wake
Lilipokuja suala la kununua ndege nyingine kubwa ambayo ni ukoo tofauti na bombadia, nguli huyu hakuunga mkono kabisa na akaweka post ndefu ya kitaalam kupinga uamuzi huo.....ni katika post hiyo aliweza kuongea kwa undani sana mpaka maswala ya mafundi wa ndege zetu mpya kutoka nje ya nchi...akaonya na kutahadharisha....kwa mara ya kwanza
barafu akafanya kinyume na mazoea...akakosoa kwa weledi uamuzi huo
Ni baada ya post hiyo mwanaJF huyu akatoweka jukwaani....
Natambua kuna maisha nje ya JF na kuna baadhi yetu tunafahamiana mpaka makazi yetu. Basi mfikishieni taarifa kuwa kuna post nyingi huku za dreamliner zinapwaya na zinahitaji neno lake