Yuko wapi Barafu?

Yuko wapi Barafu?

Kwangu barafu ni zaidi ya mtu mmoja barafu uwezo wake ni sawa na Taasisi ni mtu anaye jua vitu vingi sana vya secta tofauti tofauti kwa undani.
 
Inaonekana yupo VENEZUELA, Sa huko malaika Mkuu Si alishazima mitambo!
 
Mchambuzi wetu wa masuala ya anga jf labda Kala shavu kwenye dilimulaina

Ova
 
Mzee wa tunguri umerejea kutoka katika harakati zako ukazama JF utalala sasa ngapi sasa,

barafu watu mtaani tunaheshimika kwa elimu yako

Yaani huwa tunachukua haya madini tunakwenda kuyashusha kama yalivyo halafu tunajisifu tunasoma sana vitu
hahaa Jf ni chuo" mkuu" so unastahiki kusema kuwa huwa unasoma sana
 
Anakula zake kuku ulaya, sasa hivi anapiga pindi madogo class
afadhali umeirejesha hii avatar" ile nyingine ilikuwa na ukakasi mwingi mnooo" hatukuweza kukutambua mapema"

speaking of barafu" Barafu", ni moja ya watu wachache" makini na wenye high thinking capacity "iliyotukuka" kwa kweli" kama yupo" salama " ajitokeze". .. ilituweze kufahamu"...
kuna hati hati JF inaanza kupoteza " baadhi ya members wake" nguli' ambao kwa sisi wengine matomaso" tulikuwa tunawachukulia kuwa ni MA-lectures", wakutufunza" mambo mbali mbali ya kitaalamu zaidi''" ....kuna umuhimu kwa uongozi wa JF. kuanza kuwalinda watu hawa ili wasiweze kutoweka" kama ambavyo huwa wanalindwa faru/tembo" wasiweze kutoweka kwa ajili ya manufaa',"" ya vizazi vijavyo" vya wana JF "" .... BAK "barafu " na kuna wengine wengi " ambao hawapo kwa sasa ",Mungu",awalinde huko mlipo"
 
Kwa hakika kuna kitu hakiko sawa! Yuko wapi barafu mchambuzi nguli wa mambo ya anga katika dhana nzima ya vyombo vinavyoruka angani?
Huyu hakuwa mwanasiasa bali mtaaluma aliyefahamu kindakindaki elimu na maarifa ya usafiri adhimu wa anga...kupitia yeye wengi tuliweza kufaidika na elimu ya bure na ujuzi wa hali ya juu kwenye hii kaliba

Akiwa ni mzalendo mwenye uvumilivu mkubwa daima alisimama upande wa kutetea nia ya serikali kwenye dhana nzima ya kutaka kulifufua shirika letu la ndege ATCL kwa kununua ndege mpya aina ya bombadia...kamwe hakuchoka kutoa elimu ya bure kwa wakosoaji....

Kutokana na ujuzi na elimu yake hiyo kubwa ilifika wakati alikuwa rejeo popote palipokuwa na ubishi juu ya usafiri huo wa angani....na neno lake liliheshimika na kumaliza ubishi husika...kuna baadhi ya maeneo alitoa ushauri serikalini na serikali ikaufanyia kazi ushauri wake
Lilipokuja suala la kununua ndege nyingine kubwa ambayo ni ukoo tofauti na bombadia, nguli huyu hakuunga mkono kabisa na akaweka post ndefu ya kitaalam kupinga uamuzi huo.....ni katika post hiyo aliweza kuongea kwa undani sana mpaka maswala ya mafundi wa ndege zetu mpya kutoka nje ya nchi...akaonya na kutahadharisha....kwa mara ya kwanza barafu akafanya kinyume na mazoea...akakosoa kwa weledi uamuzi huo

Ni baada ya post hiyo mwanaJF huyu akatoweka jukwaani....
Natambua kuna maisha nje ya JF na kuna baadhi yetu tunafahamiana mpaka makazi yetu. Basi mfikishieni taarifa kuwa kuna post nyingi huku za dreamliner zinapwaya na zinahitaji neno lake

Pia kuna wafia chama fisiem akina Lizabon na Faiza Fox wamepotea kabisa!!!! Isije ndo wale walio okotwa kwenye viroba coco beach!!! [emoji17]
 
Back
Top Bottom