Yu wapi Rais Samia? Baada ya matukio haya, ni vema aongee na Taifa

Ukweli ni kwamba, yanayoendelea kwenye hii nchi yanaumza.

Lakini kabla hatujatupa lawama kwa Amiri Jeshi mkuu lazima tujue kwanza alipo na tujue nini msimamo wake kwenye mambo yanayowafanya wananchi wake wanong'one chinichini kama makinda yasiyo na watoto.

Tangu tumepandishiwa miamala hatujamsikia ila tumemsikia waziri wake akitukejeli wananchi kwamba tuhamie Burundi.

Tangu kiongozi wa chama kikuu cha cha upinzani Mh. Mbowe alipokamatwa na kuhusishwa na ugaidi hatujasikia sauti ya rais wetu.

Kuna matamko mbalimbali ya viongozi wa uma kuhusu covid19 lakini hatujamsikia mama! Yuko wapi?

Je, tangu ameapishwa kuna wakati amewahi kupiga kimya namna hii ukizingatia kuna update ya matukio mbalimbali yanayohitaji kauli yake?

Kwenye miamala tuliambiwa amesikia kilio chetu lakini mpaka muda huu sio miamala imerudi kawaida wala sauti yake. Hii sio kawaida!

Mwanzoni vifurushi vilipanda bei akatokea fasta na ile kauli yake ilifanyiwa kazi ndani ya siku mbili vifurushi vikarudi kwenye bei ya awali.

Nikiwa raia wa Tanzania naomba rais aongee na taifa
Mama yupo ila ki ukweri kashaingizwa chaka na kundi moja hatari ambalo alijawahi kutokea nchini mwetu sukuma gang.
 
Ccm wanamvuruga sana huyu mama yote haya na mabadiliko yake baada ya siku 100 yalibadilishwa na kikao cha dharura au cha kikanuni cha ccm pale Dodoma baada ya hapo tu mama amebadilika kabisaaa sijui wamemfanya nn au wamemtisha nn
Vimerudi tena vimekuwa nafuu kuliko awali.
Labda sijui kwa wenzangu
 
Kwa chanjo nasimama na Gwajima. Ni lazima uwe na self determination sio kujiendea endea tu eti kisa flan kasema na wewe ufuate kila kitu. NO NO
Ni lazima uwe na self determination sio kujiendea endea tu eti kisa flan kasema na wewe ufuate kila kitu. NO NO
 
Ukweli ni kwamba, yanayoendelea kwenye hii nchi yanaumza.

Lakini kabla hatujatupa lawama kwa Amiri Jeshi mkuu lazima tujue kwanza alipo na tujue nini msimamo wake kwenye mambo yanayowafanya wananchi wake wanong'one chinichini kama makinda yasiyo na watoto.

Tangu tumepandishiwa miamala hatujamsikia ila tumemsikia waziri wake akitukejeli wananchi kwamba tuhamie Burundi.

Tangu kiongozi wa chama kikuu cha cha upinzani Mh. Mbowe alipokamatwa na kuhusishwa na ugaidi hatujasikia sauti ya rais wetu.

Kuna matamko mbalimbali ya viongozi wa uma kuhusu covid19 lakini hatujamsikia mama! Yuko wapi?

Je, tangu ameapishwa kuna wakati amewahi kupiga kimya namna hii ukizingatia kuna update ya matukio mbalimbali yanayohitaji kauli yake?

Kwenye miamala tuliambiwa amesikia kilio chetu lakini mpaka muda huu sio miamala imerudi kawaida wala sauti yake. Hii sio kawaida!

Mwanzoni vifurushi vilipanda bei akatokea fasta na ile kauli yake ilifanyiwa kazi ndani ya siku mbili vifurushi vikarudi kwenye bei ya awali.

Nikiwa raia wa Tanzania naomba rais aongee na taifa
Aaaah hayo matukio unayoyataja ni matukio ya KAWAIDA SANA na hakuna haja ya Rais kuibuka na kuyazungumzia. Hayo yatazungumziwa na wenye "sekta" husika; wa akina Mbowe na hamu yao ya kutafuta umaarufu wa kisiasa yupo Waziri Simbachawene na kwa wengine wote wapo wahusika mahsusi; tusimsumbue Rais kwani ana mambo nyeti na ya maana kuliko haya ya akina Mbowe.

Hili la vifurushi, wana sisas uchwara ndio wana livalia njuga sasa, mbona lilipokuwa likizungumziwa Bungeni, hata kabla halijawekwa kwenye Sheria hawakulizungumzia!? Au walikuwa wamelala? Kimsingi, hili la vifurushi linahitaji ufafanuzi tu wa kina ili tuelewe nafasi na wajibu wetu katika kujiletea maendeleo kupitia KODI mbalimbali kama hizi! Wewe unadhani hao Wamarekani, Wajapani, Wachina, Wafaransa na wengine wote watuleteao MISAADA wao hizo pesa wanazidondosha kutoka kwenye MITI!? Hapana hayo ni makusanyo ya kodi za wananchi wao! Sasa na sisi tufike mahala tuanze kujitegemea, na hilo litatokana na kodi au tozo au michango, kadri utakavyo penda kuliita! Lakini ukweli ni kwamba nchi yoyote duniani inaendeshwa na kodi za wananchi wake vinginevyo ni UTEGEMEZI MPAKA BASI!
 
KUENDESHA NCHI SIO LAHISI MAGUFULI ALIFANYA MAMBO YAENDE VIZURI KWA KUFANYA KAZI USIKU NA MCHANA BILA KULALA SASA HIVJ MAMBO MENGI YAMEANZA KUHALIBIKA NAFIKIRI MNAEREWA KWA NINI TULISEMA TUONGEZE UKOMO WA UONGOZI WAKE RIP JPM
 
Watendaji wake wanamgomea wanamdharau check ishu ya tozo mwigulu ndo kwanza yupo kwenye kampeni ya kujipigia debe uraisi 2025 keshaanza drama tunduma za kukusanya watu kuzuia misafara.
Ile ni sheria tayari hauitengui tu kienyeji kama unavyodhani
 
Wewe unachuki binafsi na hao jamaa.
Chuki humdhuru mwenye kuibeba.
Kwanini baadhi ya watu mnapenda kuhusudu ukabila?
Tujifunze kujadili kwa hoja na siyo watu au matukio.

Wapende tu maana huwezi jua ndugu yako anaweza kuoa au kuolewa nao.

Je utajisikiaje moyoni mwako?!

Great minds discuss idea/issues
Average minds discuss events
Small minds discuss people/tribes
Anateseka na watu ambao hawana habari nae 😅😅
 
Back
Top Bottom