Yu wapi Dkt. Masumbuko Lamwai?

Yu wapi Dkt. Masumbuko Lamwai?

Masumbuko Lamwai?Ohh yule mwanasheria wa Ikulu. Kwanini CCM waliogopa kumpambanisha na Tindu katika kesi ya Ubunge wa Lema?
 
Jamani hivi huyu mwasheria aliyewahi kuwa Mbunge siku za nyuma nadhani kupitia NCCR kama sikosei, yuko wapi siku hizi?mbona hasikiki ...
MWENYE HABARI ZAIDI JUU YAKE AZIMWAGE HAPAJAMVINI...
mimi nichofahamu ni Walid Kaburu, kutoka mbunge wa afrika mashariki mpaka mwenyekiti wa ccm kikoma
 
Lamwai anafundisha Tumaini University ndo dean faculty of law, pia anafundisha law school of tz na anafanya shughuli zake za uwakili maisha yanaenda. Alosoma kasoma tu

Alinyang'anywa leseni ya uwakili siku mingi jo.
 
Mkuu ni vyema utambue Dr. Masumbuko Lamwai alikuwa ni mhadhiri pale UDSM-school of Law; Swali la kujiuliza kwa nini Dr.Lamwai haendelei na kibarua chake pale UDSM?

hivi unajua law school imeanza lini Tz?
 
Masumbuko lamwai miaka michache iliyopita alikuwa ni miangoni mwa mawakili wazuri sana na hata alipokuwa mbunge alikuwa anajua sana kujenga hoja bungeni,na aliweza kuwafanya vijana wengi wa wakati ule wasome sheria wakienda chuo kikuu,swali langu hivi huyu jamaa yuko wapi?na nini kilimpata mpaka amepotea kiasi hiki,ninacho amini nikwamba bado yuko hai,na je akirudi kwenye siasa kwa sasa anaweza akafanya vizuri kama enzi hizo?na ni chama gani kinaweza kumfaa zaidi?Naomba mwenye majibu atupie
 
Jamani hivi huyu mwasheria aliyewahi kuwa Mbunge siku za nyuma nadhani kupitia NCCR kama sikosei, yuko wapi siku hizi?mbona hasikiki tena, nilisikia habari kuwa alijiengua kutoka NCCR na kujiunga na CCM, je ni kweli?

Yuko tumain university anafundisha sheria..
 
Wakuu kama mlivyopata taarifa, Mh. Roman Shao, Diwani Kata ya Makiidi - Rombo (CCM) amefariki hivi leo huko KCMC - Moshi. Huyu ni Baba Mzazi wa Mh. Joseph Selasini, Mbunge wa Rombo (CHADEMA) na pia ni Baba Mzazi wa Dr. Masumbuko Lamwai.

Hebu kipindi hiki cha majonzi kwa familia yao tuungane nao kuwafariji, hayo mengine mtajadili baada ya msiba kama kutakuwa na umuhimu au haja wa kufanya hivyo.

Masumbuko Lamwai
Joseph Selasini
Baba: Roman Shao (RIP)
Sielewi elewi...
 
Masumbuko lamwai miaka michache iliyopita alikuwa ni miangoni mwa mawakili wazuri sana na hata alipokuwa mbunge alikuwa anajua sana kujenga hoja bungeni,na aliweza kuwafanya vijana wengi wa wakati ule wasome sheria wakienda chuo kikuu,swali langu hivi huyu jamaa yuko wapi?na nini kilimpata mpaka amepotea kiasi hiki,ninacho amini nikwamba bado yuko hai,na je akirudi kwenye siasa kwa sasa anaweza akafanya vizuri kama enzi hizo?na ni chama gani kinaweza kumfaa zaidi?Naomba mwenye majibu atupie

cdm kitamfaa sana, ila kwa sasa nitamshauri awe katika kamati ya wazee wa chama.
 
Ndugu siasa hacha kupigana ngumi kumbe watu wanakula saani moja wapi mrema wapi maalim seif wapi mbati .
 
Kwa sasa amefulia tu, yuko nyumbani kwake Ubungo Kibangu na kazi yake sasa hivi ni kukagua daftari la bili ya maziwa, biashara ya mkewe.

Aliyeko CHADEMA ni mdogo wake Joseph Selasini, yule aliyemng'oa Mramba kule Rombo.

kumbe ni ndugu hawa watu?
 
Walimfanyia kitu mbaya so alikuwa hana ujanja, kwa kipindi kile ccm walikuwa wanakubania kila kitu ukiwa kinyume nao thats what they did to the dude, labda kama anaweza kwa sasa arudi upinzani ni mtu mwenye uwezo wa kujenga na kutetea hoja. Walimmaliza ila anaweza kuwa lulu kama atahamia the dream team! Hata mahakamani pia ni jembe sana sema ndo hivyo tena kila mtu ana maisha yake.

kamanda huyu jamaa kwa sasa ni mwanasheria wa magamba
 
Poa sasa nimefahamu, lakini hawa jamaa sometimes wanatuchezea akili, siamini jinsi alivyokuwa anaikandia CCM, ati leo hii naye kesha kuwa mwanasheria wao. Kweli siasa ni MCHEZO MCHAFU!
Neither permanent friend nor permanent enemy in Politics.
 
Dr. Lamwai Masumbuko, Senior Lecturer - PhD (London), LLM 1978, UDSM, LLB 1976 UDSM.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom