Yu wapi Cheusimangala? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yu wapi Cheusimangala?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kashaijabutege, Jan 24, 2011.

 1. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #1
  Jan 24, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  :A S-heart-2:Ninamsaka Cheusi, Cheusi wangu Mangala,
  Mtoto kama mdosi, asopenda masihala,
  Naona kama kaasi, sioni zake makala,
  Ni siku kenda sijala, kwa kumkosa Cheusi.

  :A S-heart-2:First Ladi nahisi, umemficha mahala,
  Ninazo pia tetesi, kwa Preta analala,
  Rose mtingisha nyusi, yu wapi wangu Mangala?
  Ni siku kenda sijala, kwa kumkosa Cheusi.

  :A S-heart-2:Kila mlo ukakasi, sipati hamu ya kula,
  Cheusi njoo upesi, niepe huu msala,
  MadamT mkwasi, ni yupi kwangu mbadala?
  Ni siku kenda sijala, kwa kumkosa Cheusi.

  :A S-heart-2:Nakuuliza Demsi, ijibu hii makala,
  Ninagona kama fisi, usiku nianapolala,
  Chapachapa mikamasi, nalowesha matambala,
  Ni siku kenda sijala, kwa kumkosa Cheusi.

  :A S-heart-2:Mangala wangu Cheusi, nijuze pako pahala,
  Nachekwa kandamnasi, mapenzi yanifanya ****,
  Nitajitwanga risasi, nipumzike kwa Mola,
  Ni siku kenda sijala, kwa kumkosa Cheusi.

  :A S-heart-2:Kaditama yangu pasi, kwako Cheusimangala,
  Una utamu wa tasi, laini kama salala,
  Sukari kama fenesi, sehemu gani walala?
  Ni siku kenda sijala, kwa kumkosa Cheusi.
   
 2. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #2
  Jan 24, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hewaaa!!!:shock: wakola muno!!!
   
 3. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #3
  Jan 24, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Keshaijabutege mbona umeweka malav lav ?
  Ina maana moyo unaumia kumkosa Binti Cheusi
  Huyu huwa anatokea kama mvua za masika
  Kesho tu utamuona hapa
   
 4. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #4
  Jan 24, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Naumia sana.

  First Ladi nahisi, umemficha mahala,
  Ninazo pia tetesi, kwa Preta analala,
  Rose mtingisha nyusi, yu wapi wangu Mangala?
  Ni siku kenda sijala, kwa kumkosa Cheusi.
   
 5. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #5
  Jan 24, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  What a creativity? senksi! Ila frankly speaking huyu mamangu huwa anapotea sana au kuna jamaa lishamtia ndani linambana asiguse nje?
   
 6. Desidii

  Desidii JF-Expert Member

  #6
  Jan 24, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 1,212
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Good Boy!!!!

  wewe ni kiboko
   
 7. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #7
  Jan 24, 2011
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  yuko hanemuni...imikulwa kwako!
   
 8. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #8
  Jan 24, 2011
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  dah,,,,Kashaijabutege..technically speaking,, we ni noma! kha!
   
 9. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #9
  Jan 24, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Duh!!! Phewww!!!!!
   
 10. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #10
  Jan 24, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mama mkwe upo???
   
 11. msandawe

  msandawe Member

  #11
  Jan 24, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pole sana kijogoo, hata mi namkumbuka sana huyo binti aliyejazia
   
 12. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #12
  Jan 24, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  duh sie rangi ya chungwa tutajibeba juu ya hii post
   
 13. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #13
  Jan 24, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  kweli umeishampenda, bila kujali weusi,
  sasa watoa tenda, asakwe kama muasi,
  huku wadondoka denda, kama mpanda farasi,
  cheusimangala aja, kaa mkao wa kula

  heri uketi kitako, ajapo iishe hamu,
  sio urande makoko, asijekukuta homu,
  kisha useme mnoko, eti kakupa pumu,
  cheusimangala aja, kaa mkao wa kula

  nasikia yuko mahali, hanemuni ndo shughuli,
  tena hataki maswali, ya jaji wala wakili,
  hawezi hata kuswali, yuko bize kama kuli
  cheusimangala aja, kaa mkao wa kula

  ngoja nitakurudia, kukujuza yalomsibu,
  ikiwa ataridhia, kumchombeza kibabu,
  majuto nitamtia, jamvini aje atubu
  cheusimangala aja, kaa mkao wa kula
   
 14. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #14
  Jan 24, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Alikuwa safari siku mbili tatu atakuwepo hapa nimeongea nae juzi.Hayo mengine atajibu mwenyewe.
   
 15. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #15
  Jan 24, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 160
  Hapo kwenye nyekundu ulikuwa unamaanisha mimi au????
   
 16. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #16
  Jan 24, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,033
  Trophy Points: 280
  hihihi...pole sana ndugu Kashaijabutege....ukweli ni kwamba Cheusi na Uporoto01 walikuja kunitembelea hapa Yaeda wiki iliyopita na walinieleza wanaelekea Mang'ola....sasa anachosema hapo juu huyu Uporoto01 ni mapya....labda atueleze zaidi yu wapi huyu kimwana
   
 17. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #17
  Jan 24, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hahaha! sawa mdogo wangu,ulitaka niseme nini haya si yale ya 'niitie mkeo' ?
   
 18. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #18
  Jan 24, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Dah hapa napo mama umenigusa, natamani ungenitungia na mimi. Nasuburi mama!
   
 19. Fisherscom

  Fisherscom JF-Expert Member

  #19
  Jan 24, 2011
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,425
  Likes Received: 239
  Trophy Points: 160
  Kweli tumekumiss Cheusi hasa avatar yako. P'se popote ulipo jitokeze :-D
   
 20. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #20
  Jan 24, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Genekai wanitega, mataani waniacha,
  Heri ningekuwa mboga, jokofuni singechacha,
  Sasa najaa woga, wa fani hii kukacha
  Vipi nitakutungia, nawe humo tenzini?

  Shairi lake mdau, linayo tele manjonjo,
  Pamoja nazo nahau, zavikoleza vionjo,
  Hata pasipo limau, hutasahau muojo,
  Vipi nitakutungia, nawe humo tenzini?

  Kwa kuwa umenirai, nami sifanyi hiyana,
  ili usijekinai, japo ni-bado kuchina,
  lete hata mayai, tele tupate jichana,
  Vipi nitakutungia, nawe humo tenzini?

  Najua bado wataka, vingi vina shairini,
  Hata vigeuzwe taka, pia vichorwe katuni,
  Daima utavitaka, tele vimo moyoni
  Vipi nitakutungia, nawe humo tenzini?
   
Loading...