Hapa wanamuongelea askari lakini.Mambo ya Daslam, nimekumbuka wauza minazi pale ubungo mataa pamoja na soko kubwa tu la bidhaa mbalimbali(ilipo stendi ya daladala), kulikuwa na hoteli opposite na Olicom pale Tanesco wale Wapemba walikuwa wanauza Kashata na kalimati balaa.
sawa sawa mkuu,nakumbuka maeneo ya kariakoo alikuwa hakosekani katika michiriku.
ILIKUWA FULL MIZENGWE KWA WALE TULIYOKUWA TUNAISHI KIMAZABE...hahahahaha......dar ilikuwa tam ingawa nilikuwa mdogo na hata ustaarabu bado ulikuwepo....
Yule dada nuksi.....wanamuita Cynthia rothrockSiku hizi pale Kituo cha Polisi Magomeni kuna Mdada mmoja anaitwa Cynthia anatembea na Difenda za doria, nae anajitahidi sana.
"Kisomo" wa magomeni wapiSiku hizi pale Kituo cha Polisi Magomeni kuna Mdada mmoja anaitwa Cynthia anatembea na Difenda za doria, nae anajitahidi sana.
nenda ubungo kibangu utamkutaKuna mwingine aliwahi kuvuma miaka hiyo mikoa ya Kaskazini aliitwa 'Saba-Sita' mwenye taarifa atujuze tafadhali
Daah, I wish ningemuona enzi za uhai wake.Kwa wale wahenga wenzangu waliokuwa wapenzi wa kuhudhuria michezo kama mpira wa miguu na ngumi Bila Shaka si wageni wa jina hili
Mkama sharp alikuwa polisi mwenye mbwembwe za Aina yake huku akiwa na sifa ya ubabe na uwezo mkubwa wa kutuliza fujo
Ilikuwa ukimuona tu lazma uvutiwe kumuangalia maana anatembea kibabe,kiunoni Ana bastora mbili,pingu,kirungu nk.
Ilikuwa akionekana tu watu wenyewe wanatulia na alikuwa na uwezo WA kutuliza uwanja mzima.kwa wanaofahamu alipo huyu polisi wanijuze
Oh Mungu amrehemu kwa kweli nilikuwa namfikiria sana huyu askari kwa kuipenda kazi yake ,hope wengine wangejifunza,
Wewe ndio hauna uhakika,huyu jamaa alikufa mwaka 2007,tena alikufa akiwa na kesi ya rushwa!!
Wewe kqma hujui kaa kimya. Eti alikuwa hahongeki. Ni miongoni mwa wala rushwa wakubwa waliopata kutokezea . Tuulize sisi tuliokuwa tunaishi nae mitaa ya Kibambawe, kariakoo DSM.Kwa wale wakazi wa Dar kuanzia miaka ya mwishoni mwa `1980 na mwanzoni mwa miaka ya 1990 pale kituo cha polisi Msimbazi kulikuwa na askari mmoja mkakamavu kwelikweli ambaye alikuwa kiboko cha makonda na madereva jeuri na sugu wa daladala,wakati wote alikuwa akitembea na vitendea kazi vyake muhimu kama vile bastola,pingu na rungu huku buti zake zikishine na uniform zake zikiwa safi na zimepigwa pasi kwa kutumia wanga,hata inzi alikuwa anaogopa kutua kwenye nguo zake,yuko tofauti na askari wa siku hizi ambao wanavitambi,uniform chafu na sifa yake kuu ilikuwa ni UKAKAMAVU NA KUTOCHUKUA KITU KIDOGO,alikuwa ahongeki.