Yoweri Kaguta Museven

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,740
215,926
Yoweri Kaguta Museveni alizaliwa 19 September 1944, ni mwanasiasa wa Uganda ambae amekua rais wa Uganda tangia 29 January, 1986.

Museverni alijiunga na majeshi ya uasi ambayo yamtoa aliyekua rais wa Uganda Idi Amin (1971-79) na Milton Obote (1980-85). Mafanikio ya Museveni Uganda ni pamoja na kukuza uchumi wa nchi, utulivu na pia ameweza kusimamisha mapigano ya vikund vya waasi pamoja na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Ugana.
220px-Yoweri_Museveni_September_2015.jpg

Alizaliwa Ntungamo, eneo linalolindwa na Uganda, Museveni ni kutoka kabila la Banyankole, jina la Museveni maana yake ni mtoto wa mwanaume mwenye watoto saba. Kwa heshima ya kikosi cha Saba cha Battalion cha Jeshi la Kiafrika la Mfalme ndani ya Vita Kuu ya Pili ya dunia. Museveni amerithi jina lake la katikati kutoka kwa baba yake Amos Kaguta, mfugaji wa ng'ombe. Kaguta pia ni baba wa kaka zake Museveni Caleb Akandwanaho, maarufu anajulikana Uganda kama Salim Saleh na dada yake Violet Kajubiri.

Museveni alisoma Kyamate Elementary School, Mbarara High School na Ntare School. Mwaka 1967, alikwenda University ya Dar es Salaam Tanzania. Kule, alisome economics na siasa ya jamii na akawa Marxist. Alijuhusisha sana na siasa za Umoja wa Africa. Akiwa chuo kikuu alianzisha Umoja wa wanafunzi waleta Mapinduzi wa Kiafrika, shughuli za chama hicho kilipelekea kwenda na ujumbe wake FRELIMO ambayo ilikuwa koloni la Wareno ambayo ni Msumbiji. Kule alipata mafunzo ya kupigana nyikani na mkufunzi wao alikuwa Walter Rodney. Katika insha yake ya kumaliza shule Museveni alitetea (thesis) juu ya uwezo wa hoja za Frantz Fanon katika kuleta vurugu ya mapinduzi ndani ya Afrika huru.

Mwaka 1970, Museveni alijiunga na kikosi cha upelelezi katika serikali ya rais Milton Obote. Wakati Meja Generali Idi Amin alipopindua serikali na kuchukua madaraka January 1971, Museveni alikimbilia Tanzania pamoja na wengine pamoja na raisi aliyepinduliwa. Mvutano wa nguvu na mdaraka kati ya Amin na Obote ulikuwa mkubwa na matokeo yake ni vita vya kati ya makabila. Obote alikuwa kutoka kabila la Lango kaskazini mwa Uganda wakati Amin alikuwa kutoka kabila la Kakwa kaskazini ya kusini ya nchi. Wakati wa ukoloni wa Mwingereza madaraka ya ndani yalipangwa kuwa makabila ya Lango na Acholi yawe ni wa wanajeshi na watu wa kusini wawe wafanyabiashara. Hali hii iliendelea mpaka pale Amin alipochukua madaraka kwa kijeshi. Amin aliajiri wanajeshi wa vyeo vya juu kutoka kabila la Kakwa na Lugbara na kwa mateso aliwakandamiza makabila ya Lango na Acholi.

Makundi ya waasi yaliyokimbilia Tanzania kutoka Uganda yalipanga jaribio la kumtoa Amin madarakani mwaka 1972, walipigwa vibaya sana na wengi walipoteza maisha. October Tanzania ilitia saini mkataba wa Mogadishu ambao unakataza waasi kutumia aridh ya Tanzania kupiga serikali ya Uganda. Museveni alijitenga kutoka kwenye kundi na kuunda kundi lake alilolipa jina Majeshi ya Mstari wa Mbele ya Ukomboza wa Taifa mwaka 1973. Mwezi August mwaka huohou alimuoa Janet Kataha.

Museveni alirudi kwa wafuasi wake vijijini kusini na kusini magharibi kuunda Popular Resistant Army (PRA). Hapo alipanga mashambulizi kwa serikali ya pili ya Obote mashambulizi hayo aliyaita Obote II, na jeshi la Uganda National Liberation army (UNLA). Mashambulizi yalianza katikati ya wilaya yaMubende 6 February 1981. PRA baadae iliungana na majeshi ya Yusuf Lule kupiga Uganda Freedom Fighters na kuunda National Resistance Army (NRA) na chama chake cha siasa.
 
Ukimaliza utupe historia ya sajent doe na Charles Taylor wa Liberia.
 
Yoweri Kaguta Museveni alizaliwa 19 September 1944, ni mwanasiasa wa Uganda ambae amekua rais wa Uganda tangia 29 January, 1986.

Museverni alijiunga na majeshi ya uasi ambayo yamtoa aliyekua rais wa Uganda Idi Amin (1971-79) na Milton Obote (1980-85). Mafanikio ya Museveni Uganda ni pamoja na kukuza uchumi wa nchi, utulivu na pia ameweza kusimamisha mapigano ya vikund vya waasi pamoja na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Ugana.
220px-Yoweri_Museveni_September_2015.jpg

Museveni amerithi jina lake la katikati kutoka kwa baba yake Amos Kaguta, mfugaji wa ng'ombe. Kaguta pia ni baba wa kaka zake Museveni Caleb Akandwanaho, maarufu anajulikana Uganda kama Salim Saleh na dada yake Violet Kajubiri.

Museveni alisoma Kyamate Elementary School, Mbarara High School na Ntare School. Mwaka 1967, alikwenda University ya Dar es Salaam Tanzania. Kule, alisome economics na siasa ya jamii na akawa Marxist. Alijuhusisha sana na siasa za Umoja wa Africa. Akiwa chuo kikuu alianzisha Umoja wa wanafunzi waleta Mapinduzi wa Kiafrika, shughuli za chama hicho kilipelekea kwenda na ujumbe wake FRELIMO ambayo ilikuwa koloni la Wareno ambayo ni Msumbiji. Kule alipata mafunzo ya kupigana nyikani na mkufunzi wao alikuwa Walter Rodney. Katika insha yake ya kumaliza shule Museveni alitetea (thesis) juu ya uwezo wa hoja za Frantz Fanon katika kuleta vurugu ya mapinduzi ndani ya Afrika huru.
Story hii mkuu inatupa funzo gani?
 
Sasa ni wakati wa M7 kuiacha Ikulu na kwenda kuchunga ng'ombe, sijui naye kama analima mananasi.
 
Safi, ingawa sijawahi kusikia upande unaitwa "Kaskazini kusini". Ndiko linakopatikana kabila la nduli Amin.
 
Back
Top Bottom