YouTube channels 10 bora kwa Tanzania mwaka 2019

Johnny Sins

JF-Expert Member
Nov 4, 2019
2,538
3,826
Wakati ikikaribia mwisho wa mwaka 2019, hapa Tanzania Tech huwa na taratibu ya kurudi nyuma na kuangalia yote tulio yapitia kwa mwaka mzima. Kwa siku ya leo tunaenda kuangalia channel 10 bora za YouTube kwa hapa Tanzania kwa mwaka 2019.

Kumbuka channel hizi zimepatikana kuwa bora kutokana na kuwa na subscribers wengi kuliko channel nyingine kwa hapa Tanzania. Kama ilivyokuwa kwenye list ya mwaka 2018 , list hii imewezeshwa na data kutoka kwenye tovuti ya Socialblade.

Pia kumbuka inawezekana idadi ya subscriber iliyotajwa kwenye list hii ikiwa imeongezeka kulingana na muda utakao soma makala hii.

10. MBOSSO

Subscriber 712K – Hadi Tarehe 9-12-2019
Channel hii Haikwepo kwenye List ya Mwaka 2018 !new

Mbosso ni msanii wa kimataifa wa muziki wa bongo flava kutoka hapa Tanzania na ni mmoja wa wasanii walio sajiliwa chini ya kampuni ya Wasafi ambayo inaongozwa na Msanii Diamond Platnumz. Channel hii imeanzishwa mwaka 2016 na ina idadi ya video 402 hadi kufikia siku ya leo.

9. AZAM TV

Subscriber 759K – Hadi Tarehe 9-12-2019
Channel hii Haikwepo kwenye List ya Mwaka 2018 !new
Azam TV ni channel ya chombo cha habari cha Azam TV Tanzania, channel hii inakupa habari na makala mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania kwa lugha ya kiswahili. Channel hii ni sehemu ya vituo mbalimbali vya habari kutoka kampuni ya Bakhresa Group.

8. BINGO ONLINE TZ

Subscriber 768K – Hadi Tarehe 9-12-2019
Channel hii Haikwepo kwenye List ya Mwaka 2018 !new
Bingo Online TZ ni channel ya hapa Tanzania ambayo inakuletea habari mbalimbali za wasanii na udaku kutoka Tanzania, Channel hii ni maarufu zaidi kwa matukio ya Live pamoja na udaku pamoja na matukio ya kila siku. Channel hii imeanzishwa mwaka 2017 na ina idadi ya zaidi ya video 3000 hadi kufikia leo.

7. JAMVI ONLINE TV

Subscriber 922K – Hadi Tarehe 9-12-2019
Channel hii Haikwepo kwenye List ya Mwaka 2018 !new
Jamvi TV ni channel ya matukio mbalimbali kutoka Tanzania, channel hii inakuapa habari na makala mbalimbali kutoka ndani na nje ya Afrika na Tanzania kwa ujumla. Channel hii imeanzishwa mwaka 2012 na ina idadi ya video 2,058 hadi kufikia siku ya leo.


6. WASAFI MEDIA

Subscriber 1.01M – Hadi Tarehe 09-12-2019
Channel hii Haikwepo kwenye List ya Mwaka 2018 !new
Wasafi Media ni sehemu ya chombo cha habari cha msanii na mfanyabiashara Nasibu Abdul au Diamond Platnumz, channel hii inaweka video za makala mbalimbali za habari, mchezo, burudani, vichekesho pamoja na mambo mengine mengi. Channel hii imeanzishwa mwaka 2018 na ina idadi ya video 2,937 hadi kufikia siku ya leo.


5. RAYVANNY

Subscriber 1.22M – Hadi Tarehe 09-12-2019
Channel hii Imepanda ilikuwa namba 6 mwaka 2018 ^imepanda
Rayvanny ni msanii wa kimataifa wa muziki wa bongo flava kutoka hapa Tanzania na ni mmoja wa wasanii walio sajiliwa chini ya kampuni ya Wasafi ambayo inaongozwa na Msanii Diamond Platnumz. Channel hii imeanzishwa mwaka 2016 na ina idadi ya video 460 hadi kufikia siku ya leo.

4. HARMONIZE

Subscriber 1.35M – Hadi Tarehe 9-12-2019
Channel Hii ilikuwa namba 4 mwaka 2018=Sawasawa
Harmonize ni msanii bongo fleva wa kimataifa na pia ni mmoja wa wasanii waliokuwa chini ya lebo ya Wasafi ambayo inaongozwa na Diamond Platnumz. Channel hii ilianzishwa mwaka 2015 na kuanzia kipindi hicho hadi sasa ina idadi ya jumla ya video 329 hadi kufikia siku ya leo.

3. GLOBAL TV

Subscriber 1.98M – Hadi Tarehe 9-12-2019
Channel hii ilikuwa namba 3 mwaka 2018
=Sawasawa
Global TV au Global TV Online ni Channel inayokupa habari mbalimbali za kila siku kutoka ndani na nje ya nchini. Channel hii ilianzishwa mwaka 2011 na ni moja kati ya sehemu ya huduma zinazotolewa na Global Publisher, channel hii ina idadi ya video 26,536 hadi kufikia siku ya leo.

2. MILLARD AYO

Subscriber 2.34M – Hadi Tarehe 9-12-2019
Channel hii ilikuwa namba 2 mwaka 2018
=Sawasawa
Millard Ayo ni mmoja wa watangazaji maarufu wa kituo cha Clouds Media Group, kupitia channel yake hii utaweza kupata habari mbalimbali za kutoka ndani na nje ya nchi kila siku. Channel ya Millard ayo ilianzishwa mwaka 2012 na kwa muda wote hadi sasa channel hiyo ina idadi ya video 21,947 hadi kufikia siku ya leo.

1. DIAMOND PLATNUMZ

Subscriber 2.75M – Hadi Tarehe 9-12-2019
Channel hii ilikuwa namba 1 mwaka 2018
=Sawasawa
Channel ya kwanza maarufu zaidi kwa hapa nchini Tanzania ni channel ya mwana muziki wa kimataifa na msanii wa bongo fleva Diamond Platnumz. Channel yake iliyoanzishwa mwaka 2011 ina idadi ya video 609 hadi kufikia siku ya leo.
Na hizo ndio YouTube channel 10 bora kwa hapa Tanzania, kama unataka kujua channel bora duniani hadi sasa unaweza kusoma hapa kujua channel 10 bora zenye subscriber wengi kuliko channel zote kwenye mtandao wa YouTube .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom