Young Africans yanasa saini ya kinda Shekhan Ibrahim Khamis (18) kutoka JKU

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
9,285
9,922
Klabu Ya Yanga SC imekamilisha usajili wa kiungo Shekhan Ibrahim Khamis (18) kutoka JKU.

Yanga SC imekamilisha Usajili wa Kiungo Huyo Fundi Kutoka Zanzibar kwa mkataba wa miaka mitatu

Shekhan alikuwa sehemu ya kikosi cha Zanzibar kilichoshiriki CECAFA U18 mwaka huu 2023 Kenya.

Awali wekundu wa Msimbazi walikuwa mbele kusaka saini ya kinda huyu hata alivyotua Bongo alikuja kumalizana nao ila Wananchi Wanchi wakawa Fasta kumnasa kinda huyo.

Mazingira waliyoyajenga Yanga kwa sasa katika jamii ni rahisi mchezaji au hata familia yake au klabu kumshawishi kwenda Yanga kuliko Simba hata km Simba nao Wana nia ya kumsajili na hii sio hapa Tanzania tu hata mahali popote Africa Simba hawezi kugombea mchezaji na Yanga akampata kwakua Yanga inaonesha ni clabu inayotafuta mafanikio kwa vitendo na hicho ndio kila mchezaji anachokitafuta ktk maisha yake.
 
Back
Top Bottom