ASFC: African Lyon 0-3 Simba | Benjamin Mkapa Stadium

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,444
7,792
Michezo ya kombe la shirikisho inaendelea na sasa ni klabu ya soka ya African Lyon dhidi ya Simba SC kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

======

00' Muamuzi anapiga filimbi kuashiria mwanzo wa mchezo

09' Ibrahim Hajibu anaweka kamba ya kwanza kwa Simba, African Lyon 0-1 Simba

17' Bwalya anajaribu shuti kali kuelekea lango la African Lyon lakini linaishia kwa walinzi

18' Medie Kagere anajaribu na kipa wa African Lyon anafanya kazi ya ziada kuupangua

20' Chikwende anawekwa chini na mlinzi wa African Lyon, Simba inapata Penalt

22' Medie Kagere anakosa mkwaju wa penalt kwa kupiga nje

29' Mwashiuya anajaribu shuti kubwa nje ya 18 katika harakati za kusawazisha lakini mpira unapaa juu ya goli

39' Dilunga anamlamba chenga golikipa wa African Lyon lakini kasi ya mpira inamzidi na kupiga nje ya lango

43' Ibrahim Ajib Migomba anaweka goli lake la pili baada ya kupiga shuti kwenye mpira unaoambaa kutokana na mlinda mlango kuokoa shuti la Bwalya, African Lyon 0-2 Simba

45+2' Mwamuzi anapuliza filimbi kuashiria mapumziko, Ibrahim Ajib anakuwa shujaa wa kipindi cha kwanza kwa kuipa Simba goli mbili za kuongoza

UMILIKI WA MPIRA, AFRICAN LYON 37% - SIMBA 63%

45' Mpira unarejea kutoka mapumziko

47' Mwashiuya anapiga kona pacha kuelekea lango la Simba lakini zote zinakuwa hazina manufaa

62' Chikwende anaweka goli maridadi kwa upande wa Simba baada ya kupokea pasi maridadi kutoka kwa Miraji Athumani

65' Simba wanacheza mpira wa gonga lakini juhudi zao zinaishia kwa Gadiel Michael kuwa 'Offside'. African Lyon 0-3 Simba SC

68' Rehani Kibingu anajaribu kuitafutia African Lyon lakini shuti lake linaishia nyavu za pembeni

70' Saidi Khamis anaingia kuchua nafasi ya Rally Bwalya kwa upande wa Simba

71' Saidi Kipanga anatumia vizuri makosa ya mabeki wa Simba kuupoka mpira lakini shuti lake linapaa Juuu

75' Emmanuel Daudi analamba kadi ya njano kwa kumvuta ili kumpunguza kasi mchezaji wa Simba

81' John Bocco anachukua nafasi ya Meddie Kagere

87' Mwalami Abdalla anamdondosha Chikwende nje kidogo ya 18, anapewa kadi ya njano

FT' African Lyon inakubali kichapo na kuondoshwa kombe la shirikisho. Sasa Simba kukutana na Kagera Sugar hatua ya 16 bora. African Lyon 0-3 Simba.
 
Back
Top Bottom