Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

hamis77

hamis77

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Messages
448
Points
250
hamis77

hamis77

JF-Expert Member
Joined Aug 20, 2013
448 250
 
Shadeeya

Shadeeya

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2014
Messages
31,459
Points
2,000
Shadeeya

Shadeeya

JF-Expert Member
Joined Mar 12, 2014
31,459 2,000
20190816_101846-jpg.1182638
Msafara wa kikosi cha Yanga unatarajiwa kuondoka nchini August 20 kuelekea Botswana kwa ajili ya mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers Mchezo huo utapigwa August 23, jijini Gaboronne Yanga imeweka kambi Moshi ikijiandaa na mchezo huo Mabingwa hao wa kihistoria wataunganisha moja kwa moja kutoka Moshi kuelekea Botswana baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya AFC Leopards ambao utapigwa Jumapili, August 18 Leo Ijumaa Yanga itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Polisi Tanzania #sisihao✈ - Yangafulldoz
 
Shadeeya

Shadeeya

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2014
Messages
31,459
Points
2,000
Shadeeya

Shadeeya

JF-Expert Member
Joined Mar 12, 2014
31,459 2,000
20190816_112410-jpg.1182680

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema kurejea kwa beki Juma Abdul ni habari njema kwa kikosi chake kinachojiandaa na mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers

Abdul alikosa mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar es salaam, akiweka ngumu kuingia kambini hadi alipwe madai yake

Abdul ana nafasi ya kuanza mchezo utakaopigwa Botswana August 23 baada ya Boxer kupata majeraha

Zahera amefichua kuwa anataka kumtumia Abdul kwenye mechi hiyo ya ugenini kumimina krosi zenye macho ambazo zitakuwa zikiwafikia mastraika wake watakaokuwa na kazi ya kufunga tu, baada ya kubaini kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita walizikosa krosi hizo. "Kikosi chetu kilikuwa kikimtegemea zaidi Boxer ambaye atakuwa nje kwa muda baada ya kuumia goti kwenye mchezo wa awali ulioisha kwa sare ya 1-1, lakini hata wale ambao niliwatumia kuziba nafasi yake hawakufiti ndio maana nimefurahi Abdul kurejea," Zahera amenukuliwa na Mwanaspoti

Zahera alisema kwa jinsi alivyowasoma wapinzani wake amegundua ni wabovu kwenye mipira ya krosi, hivyo ujio wa beki huyo anayefanya vizuri eneo hilo inaweza ikawa dawa dhidi ya wapinzani wao kuweza kupata matokeo katika uwanja wao wa ugenini

Kuhusu Yondani, Zahera alisema pia ana nafasi ya kucheza itategemea na mfumo atakaoutumia, huku akiwamwagia sifa mabeki Ally Mtoni ‘Sonso’, Lamine Moro jinsi walivyocheza kwa kuelewana hawakuwa na makosa mengi kwenye mchezo huo.

Alisema kwa mfumo wa kuchezesha mabeki watatu Yondani anaweza kufiti kwa kukaa kati huku Sonso na Moro wakiwa pembeni yake, lakini alisisitiza mchezo unaofuata unahitaji mawinga wenye kasi sambamba na mabeki wa kupanda kupitia pembeni.
#sisihao✈ - Yangafulldoz
 
severinembena

severinembena

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2018
Messages
2,109
Points
2,000
severinembena

severinembena

JF-Expert Member
Joined Jun 2, 2018
2,109 2,000
Iyo sale lazima iwa cost,maana kama mmeshindwa kufua dafu nyumbani ugenini mtaweza?
Mara ya mwisho tulipokutana na hao jamaa kabla hatujacheza nao msimu huu mechi ya kwanza walitufunga 2-1 uwanja Wa taifa,marudiano kwao tukatoka sare, so lolote lawezekana
 
T

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2019
Messages
1,781
Points
2,000
T

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2019
1,781 2,000
Hongera Yanga kwa ushindi dhidi ya AFC Leopalds. Wachezaji wamecheza kwa kujituma ili kurudisha imani kwa mashabiki. Changamoto ni safu ya umaliziaji. Kiukweli washambuliaji wa kati wanatakiwa waongeze bidii na uchu wa kufunga.

Pengo la Makambo liko wazi kabisa! Inashangaza kocha kumuuza mchezaji kirahisi tu na wakati bado alihitajika kwenye timu. Achilia mbali Gadiel Michael.
 
kishumbaz

kishumbaz

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2015
Messages
487
Points
500
kishumbaz

kishumbaz

JF-Expert Member
Joined Jul 29, 2015
487 500
Papa Zahera timu imemshinda...mtu una banka, makame, fei timu linabutua butua tu...he has to leave
 
Kurunzi

Kurunzi

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2009
Messages
5,100
Points
2,000
Kurunzi

Kurunzi

JF-Expert Member
Joined Jul 31, 2009
5,100 2,000
Tuweke ushabiki pembeni Mchezo wa Yanga na Township Rollers huenda ukaamua hatima ya Kocha Mwinyi Zahera.

Baada ya kufanyika usajili makini, jambo pekee ambalo mashabiki wa Yanga wanataka kuona, ni timu yao ikifanya vizuri

Ukiachana na michezo ya kirafiki ambayo Yanga imecheza, matokeo ya mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers hayakuwafurahisha wengi hasa ikizingatiwa mchezo huo ulipigwa ardhi ya nyumbani

Tayari baadhi ya mashabiki wameanza kuhoji uwezo wa kocha Zahera katika kuipa mafanikio timu hiyo msimu huu

Ni jambo la kawaida hasa pale timu inapokuwa haipati matokeo ingawa bado ni mapema sana, lakini hali hiyo ilitarajiwa

Kwa misimu miwili Yanga haikuwa katika ubora wake wa miaka mingi, hivyo baada ya usajili wa nyota wengi wapya, mashabiki walitarajia kuiona Yanga mpya

Kocha Mwinyi Zahera anafahamu kama Yanga itaondoshwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa hatua hii ya awali, basi atakuwa kwenye wakati mgumu

Na pengine hiyo ndio sababu iliyomfanya achukizwe na ziara ya timu yake mikoa ya Arusha na Kilimanjaro ambapo alibainisha kuwa haikuisaidia timu kwa kuwa walicheza kwenye mazingira ya viwanja ambavyo haviendani na mazingira watakayocheza huko Botswana

Hata hivyo uongozi wa Yanga umesema ziara hiyo iliikuwa na manufaa na iliandaliwa kwa matakwa ya benchi la ufundi

Lakini jambo la msingi kwake ni kuhakikisha Yanga inashinda ugenini ili kuweza kusonga mbele raundi ya kwanza

Matokeo tofauti na ushindi, yatamuweka kwenye wakati mgumu mbele ya mashabiki wa timu hiyo ambao wengi wameendelea kumuunga mkono licha ya kutoridhishwa na matokeo ya michezo ya hivi karibuni

Katika moja ya mahojiano yake, Zahera alisema wamedhamiria kushinda ugenini, lengo likiwa kupata bao mapema ili kuwaweka kwenye presha Township Rollers watakaokuwa wakicheza nyumbani

Pengine huu ndio mchezo ambao Wanayanga wataishuhudia ile timu yao halisi wanayoitaka

Lakini kama mambo yakienda 'kombo', mchezo huo utazidi kumpunguzia imani Zahera

Kwani siku zote, makocha wanaajiriwa ili wafukuzwe pale inapotokea timu haifanyi vizuri
 

Forum statistics

Threads 1,334,838
Members 512,138
Posts 32,488,557
Top