Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Monsgnor

Monsgnor

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2012
Messages
505
Points
500
Monsgnor

Monsgnor

JF-Expert Member
Joined Mar 26, 2012
505 500
Bado sio sababu, simba walikua wanapigwa tano tano lakini bado walikua wanajaa uwanjani, kiufupi wananchi tumezingua.
Kiwango kibovu watu hawawezi kujaa uwanjani...wachezaji wanatuangusha..mechi na Kariobang Sharks walitakiwa kushinda kwa kishindo..watu wangejaa jana
 
doup

doup

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2009
Messages
2,026
Points
2,000
doup

doup

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2009
2,026 2,000
Walikuwa kwenye TV kufatilia timu zao pendwa za EPL, Wazo lankizushi tff waweke screen pale taifa kuonesha zoka la epl ratiba ikigongana na mechi zetu, kama kwenye vibanda umiza unakuta screen hadi 3 mechi tofauti
 
zipompa

zipompa

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2014
Messages
5,423
Points
2,000
zipompa

zipompa

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2014
5,423 2,000
Ukiwa unaangalia mpira jifunze kuangalia vitu vya msingi.Mfano Ali Ali alipiga krosi ngapi ambazo zilifika? Alipoteza mpira mara ngapi kila alipojaribu ku drible? Sio kuangalia mchezaji anavyokimbia kimbia uwanjani ukazani ndo kucheza vzr.Kwa mpira wa sasa kazi ya beki wa pembeni ni pamoja na kushambulia hasa kupiga krosi mujarabu na makini zinazofika.
tatizo uliangalia mpira ukiwa na vipimo vyako flani (gadiel mbaga hakupiga cross wala hakuwa na blocking za maana) ila siwez sema hakucheza vzr kisa kapombe alikuwa anapanda kupiga cross (wakati mwingine alikuwa ana sababisha mashambulizi kwa kuchelewa kurudi)


kwa mtazamo wangu ally ally alicheza vzr 80%
 
N

ndiga

Member
Joined
Jan 28, 2014
Messages
76
Points
125
N

ndiga

Member
Joined Jan 28, 2014
76 125
Iyo sale lazima iwa cost,maana kama mmeshindwa kufua dafu nyumbani ugenini mtaweza?
Hata nyie hamko salama kama mnavyodanganyana, mwaka huu siyo mwaka Jana , kila timu inaweza kupata matokeo bila kujali iko home au away cha msingi ni kujipanga kuliko mpinzani wako tu.
 
KUCH KUCH

KUCH KUCH

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2015
Messages
419
Points
250
KUCH KUCH

KUCH KUCH

JF-Expert Member
Joined Dec 18, 2015
419 250
Hata nyie hamko salama kama mnavyodanganyana, mwaka huu siyo mwaka Jana , kila timu inaweza kupata matokeo bila kujali iko home au away cha msingi ni kujipanga kuliko mpinzani wako tu.
POLE WEEE. Yanga sio SIMBA
Ndio mana hta uwanja MLIUOGOPA. SUBIRI UONE MUZIKI WA WANAUME
 
Shadeeya

Shadeeya

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2014
Messages
31,462
Points
2,000
Shadeeya

Shadeeya

JF-Expert Member
Joined Mar 12, 2014
31,462 2,000
Mpira hauna ugenini wala nyumbani baka alishinda tatu akapigwa nne

Kwahyo usikalili katika soka hatuna formula ya ushind unapigwa hata kwako

Kwahyo Simba kupata droo kule na ud songo ndio unategemea atashinda kwa urahis hapa taifa unajua timu pinzani inakuja na plan gani?ΒΏ??????
Manara kawaharibu hawa. Teh teh
 
Shadeeya

Shadeeya

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2014
Messages
31,462
Points
2,000
Shadeeya

Shadeeya

JF-Expert Member
Joined Mar 12, 2014
31,462 2,000
20190813_093735-jpg.1179916

TETESI ZA AFISA HABARI YANGASC

Uongozi wa Yanga huenda ukafanya mabadiliko katika kitengo chake cha habari ambapo Mwanahabari Antonio Nugaz huenda akamrithi Dismas Ten

Nugaz amekuwa akisimamia matukio makubwa yote ya klabu ya Yanga akiwa 'MC'

Aidha Ten ambaye sasa anakaimu nafasi ya Katibu Mkuu, huenda akarithi moja kwa moja nafasi hiyo iliyoachwa na Charles Boniface Mkwasa

Kumekuwa na presha kubwa kutoka kwa mashabiki ambao wanataka mabadiliko kwenye kitengo hicho kutokana na kukosekana kwa hamasa

Siku ya tukio la Kubwa Kuliko, Rais Mstaafu awamu ya nne Mh Dk Jakaya Kikwete alishangazwa na kutokuwepo kwa hamasa miongoni mwa mashabiki wa Yanga kujitokeza uwanjani tofauti na watani zao Simba

Hali hiyo imejitokeza juzi kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers ambapo mashabiki wachache walijitokeza uwanjani

Wengi wanadhani hakuna hamasa ya kutosha ya kuwafanya mashabiki watoke majumbani kwao kuelekea uwanjani - Yanga_soccer
 
Shadeeya

Shadeeya

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2014
Messages
31,462
Points
2,000
Shadeeya

Shadeeya

JF-Expert Member
Joined Mar 12, 2014
31,462 2,000
20190813_094337-jpg.1179927

Beki kisiki wa Yanga Kelvin Yondani amesema amerejea rasmi kikosini na atakuwepo kwenye mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers ambao utapigwa jiji la Gaborone nchini Botswana

Yondani, Juma Abdul na Andrew Vicent walikosa mchezo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Taifa wakijiweka pembeni wakisubiri wakamilishiwe madai yao na uongozi wa Yanga

Kocha Mwinyi Zahera aliwaunga mkono wachezaji hao akiutaka uongozi umalizane nao ili warudi kikosini

Habari njema ni kuwa changamoto ya wachezaji hao imemalizwa na watakuwa sehemu ya kikosi kitakachoelekea mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Rollers "Mimi sina tatizo na uongozi, kila kitu kimerekebishwa hivyo nawaambia mashabiki wasiwe na hofu," amesema "Nitakuwepo kambini Moshi na pengine mchezo wa marudiano Botswana nitacheza"

Kurejea kwa Yondani kikosini huenda kukamlazimu Zahera kukifanyia mabadiliko kikosi chake cha kwanza

Zahera amekuwa akiwatumia Ally Mtoni na Lamine Moro katika nafasi ya ulinzi wa kati

Anaweza kumpeleka Mtoni pembeni na kati wakacheza Moro na Yondani

Katika mchezo huo wa marudiano, pia Zahera atakuwa na nyota waliokosa mchezo wa kwanza kutokana na kuchelewa kuwasili kwa vibali vyao

Nyota hao ni Farouk Shikalo, Mustapha Suleyman na David Molinga - Yanga_soccer
 
Shadeeya

Shadeeya

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2014
Messages
31,462
Points
2,000
Shadeeya

Shadeeya

JF-Expert Member
Joined Mar 12, 2014
31,462 2,000
20190813_094906-jpg.1179931

Kikosi cha Yanga jana kimeelekea mkoani Arusha kuweka kambi ya maandalizi ya mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers

Baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Taifa, Yanga inahitaji kushinda Botswana au hata sare ya kuanzia mabao mawili itawabeba hatua inayofuata

Hali hiyo inaufanya mchezo huo uwe wa kufa na kupona kwa mabingwa hao wa kihistoria

Kutolewa raundi ya kwanza kwenye michuano hiyo ni jambo amalo halitawafurahisha mashabiki wa timu hiyo ambao wengi wamerejesha imani baada ya kikosi kusukwa upya

Yanga itaelekea mkoani Arusha ikiwa na majembe yake yote wakiwemo Kelvin Yondani, Juma Abdul na Andrew Vicent ambao hawakuwa kikosini

Maproo kupata vibali

Habari njema zaidi ni kuwa kwenye mchezo wa marudiano huko Botswana Yanga itakuwa na uhakika wa kuwatumia nyota wake Farouq Shikalo, Mustapha Suleyman na David Molinga ambao walikosa mchezo wa kwanza kutokana na kukosa vibali

Kocha Mwinyi Zahera amesema wachezaji hao watakiongezea nguvu kikosi chao kwenye mchezo wa marudiano

Ikiwa Arusha Yanga itacheza michezo miwili ya kirafiki; August 16 itacheza na Polisi Tanzania mkoani Kilimanjaro na August 18 itacheza na AFC Leopards - Yanga_soccer
 
Shadeeya

Shadeeya

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2014
Messages
31,462
Points
2,000
Shadeeya

Shadeeya

JF-Expert Member
Joined Mar 12, 2014
31,462 2,000
20190813_095716-jpg.1179943


Mshambuliaji wa Yanga Patrick Sibomana amefichua kuwa mkwaju wa penati aliokosa kwenye dakika ya 30 ya mchezo dhidi ya Township Rollers, ulimuondoa mchezoni kwa muda

Sibomana mmoja wa wapambanaji wapya kwenye kikosi cha Yanga amesema walihitaji kushinda mchezo huo hivyo aliumia sana baada ya kukosa mkwaju wa penati "Ilikuwa nafasi adimu kwetu, baada ya kukosa nilisikitika sana, nilikuwa nikifikiria nitawaambia nini wachezaji wenzangu na mashabiki wetu," alisema

Hata hivyo Sibomana amesema kuwa alijipa moyo na kuendelea kuipigania timu

Kuhusu kupiga penati ya pili, Sibomana amefichua awali alimtaka nahodha Papi Tshishimbi apige lakini akamwambia apige tena "Nilimwambia Tshishimbi apige lakini naye akaniruhusu nipige tena"

Sibomana amesema wanajiandaa kikamilifu kuhakikisha wanapata ushindi kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa Botswana August 25 "Bado tuna nafasi ya kusonga mbele, sasa tunajiandaa vyema kuweza kupata matokeo ugenini"
 
Shadeeya

Shadeeya

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2014
Messages
31,462
Points
2,000
Shadeeya

Shadeeya

JF-Expert Member
Joined Mar 12, 2014
31,462 2,000
Hambebeki nyie,mmeshinda kupindua meza mbele ya mama zenu,mtapindua meza mbele ya wakwe zenu.
Yanga ikishinda ugenini natembea uchi Shadeeya
Tooooba!!!

Mtani siku hiyo utaishi kwa shida ujue. πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€.

Umeshasahau ya Makamba eee? Mana Ulibaki kukimbia kimbia tu. πŸ˜€πŸ˜€
 

Forum statistics

Threads 1,334,908
Members 512,150
Posts 32,490,423
Top