- Thread starter
- #21
Pole mpenzi kama ni mpenzi wako wa kwanza ni ngumu sana aseee kwani nakumbuka hata mimi ilivyonitokea nilikua siamini na hata mtu alipokuwa akinishauri nilikua simuelewi lakini nashukuru mungu yalipita na yaliisha. Cha msingi kazana kumuomba mungu akupunguzie maumivu kama sio kuyaepusha kabisa, na amini ipo siku utabaki na amani moyoni ingawa kwa sasa unaumia. Jitahidi kujichanganya na watu unapiga piga stori ili usiwe unawaza sana. Yaani ni ngumu sana nakuombea uweze kuyashinda haya yakukutayo sasa ila usijilazimishe kumpenda kama unaona kabisa hakupendi kwani atakuja kukuumiza zaidi ya hapo.
Asante my dear,
umesema ukweli, maana ninakoelekea ni kujilazimisha kumpenda... mtu akikukosea mara nyingi na habadiliki, upendo unaweza kuzimika taratibu na ukaishia kuwa unajilazimisha kumpenda... The first tym nilivomwambia kuwa I cant handle this anymore, I want to walk away, alinikumbusha mengi sana tuliyopitia, na kunihakikishia ananipenda, na tukaongea sana, nikamweleza kuwa hata mimi nampenda ila inabidi hivi vitu anavovichukulia kama mzaha aache, akaniambia sometimes he acts that weird because he loves me... yaani sasa hiyo kali mtu unampenda mpaka you act weird, thats really weird!!! He says he cannot do without me, he wont be able to survive... anataka tu muelewane mfurahi, mcheke...ila hataki ma-confrontations, wala hataki kuachana...sasa unamuelewaje mtu wa hivo....