You vs you

You vs you

Dr leader

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
1,065
Reaction score
1,413
Kitu hatari zaidi kuhusu low self-esteem si kujiamini kidogo.

Ni jinsi inavyoweza kutawala maisha yako kimya kimya bila hata wewe kugundua.

Low self-esteem inaweza kumfanya mtu mzuri ajione hastahili kupendwa.
Mtu mwenye kipaji ajione hana thamani.
Mtu mwenye akili ajikute anajitilia mashaka kila siku.

Huonekana kwenye mambo madogo ya kila siku kama:

• Kuomba msamaha kupita kiasi
• Kukubali kutendewa chini ya kiwango unachostahili
• Kunyamaza wakati unatakiwa kuzungumza
• Kujilinganisha na kila mtu unaowaona mtandaoni
• Kujihisi mwenye hatia unapopumzika
• Kutafuta uthibitisho wa watu kabla ya kufanya maamuzi yako

Watu wengi hudhani low self-esteem inaathiri confidence pekee, lakini ukweli ni kwamba inaenda mbali zaidi.

Inaathiri:

• Mahusiano
• Fursa za maisha
• Utulivu wa akili
• Muonekano wa mwili
• Nguvu na energy yako
• Namna watu wanavyokuchukulia

Usipojithamini wewe mwenyewe, bila kujua unawafundisha wengine wasikuthamini pia.

Sehemu ya kutisha zaidi ni kwamba watu wengi wameizoea hali hiyo.

Wanacheka huku wanaumia ndani.
Wanajificha nyuma ya “niko sawa.”
Wanapost confidence mtandaoni lakini ndani wanapambana na kujiona hawatoshi.

Kupona low self-esteem si kuwa na kiburi wala majivuno.

Ni kufikia hatua ya kutambua kuwa:

• Unastahili heshima
• Unastahili mapenzi yenye afya
• Unastahili kusikika na kuonekana
• Unastahili fursa nzuri
• Unastahili amani bila kulazimika kuthibitisha thamani yako kila wakati

Confidence haianzi siku maisha yanapokuwa perfect.

Inaanza pale unapoacha kujiongelea vibaya wewe mwenyewe.

Linda thamani yako.
Maisha yako yote hubadilika pale unapokubali kweli kwamba wewe ni wa muhimu.

Abuuabdillah ✍️
 
Back
Top Bottom