Energy & Frequency

Energy & Frequency

Dr leader

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
1,077
Reaction score
1,444
Watu wengi huchanganya, FREQUENCY NA ENERGY

Ngoja nikueleze hapa kwa lugha rahisi :

Energy ni nguvu.

Kila kitu duniani kina energy.
Mwili wako una energy.
Maneno yana energy.
Mawazo yana energy.

Hata sehemu unazotembelea inaweza kuwa na energy nzuri au mbaya.

Ndiyo maana:

Kuna watu ukikaa nao dakika 5 tu unahisi amani.

Na kuna wengine ukitoka kwao unahisi umechoka bila sababu.


Energy yako huonekana kupitia:

Hisia zako

Namna unavyoongea

Confidence yako

Mood yako

Presence yako

Mtu mwenye energy kubwa:

Huwa na mvuto

Ana kujiamini

Watu humsikiliza kirahisi

Anaonekana “ana nuru”


Mtu mwenye energy mbovu:

Huwaza sana

Ana hasira au huzuni muda mwingi

Hukata tamaa haraka

Huvuta mazingira mabaya

Frequency ni kiwango au mtetemo wa hiyo energy.

Kisayansi, kila kitu kinatetema kwa kiwango fulani.

“Everything is vibration.”



Mfano : Radio ikitaka kushika station fulani lazima iwe kwenye frequency sahihi.

Na maisha ni hivyo hivyo.

Ukijaa:

hofu,

chuki,

wivu,

stress,


unakuwa kwenye “low frequency”.

Lakini ukijaa:

amani,

shukrani,

upendo,

kujiamini,

malengo,


unakuwa kwenye “high frequency”.


Frequency yako huathiri:

Namna watu wanavyokupokea

Maamuzi unayofanya

Nafasi unazovuta kwenye maisha

Hata mahusiano yako


Ndiyo maana:

Watu wenye mawazo yanayofanana huvutana.

Mtu mwenye negativity nyingi huvuta drama nyingi.

Mtu mwenye utulivu mara nyingi huvuta opportunities nzuri

“Unakuwa kile unachokitafakari kila siku.”


Ukijaza akili yako giza, utaliishi giza.

Ukijaza akili yako nuru, utaiishi nuru.

Ukiwa na watu mwenye low energy mawimbi ya mtetemo yataivuta low energy kwako pia

Kila kitu kina energy halafu frequency ni njia ya kusafirisha hiyo energy kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine

Attena yako ikikaa kwenye Frequency sahihi itashika channels bila chenga utaona HD
Na kinyume chake ni hivyo hivyo.

Abuuabdillah ✍️
0744 883 353
 
Back
Top Bottom